tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,804
- 18,231
Nipo hapa mtaa wa kati nafanya utafiti binafsi. Asilimia kubwa ya watu, hasa vijana na watu wa umri wa kati, wapo wawiliwawili (bond) na wanaonekana wapo kimahaba zaidi.
Nimepita mitaani, kwenye baa, groceries, na maeneo mengine ya kujipumzisha hali ni hiyohiyo. Kilichonitisha zaidi ni pale nilipopita kwenye guest houses zilizopo maeneo haya kuanzia mishale ya saa 7 adhuhuri na kukutana na maandishi: 'VYUMBA VIMEJAA!'. Nimefanya utafiti kwenye nyumba zipatazo 8, zijapata hata chumba kimoja cha wageni kilicho wazi! Yaani haya ni maasi ndugu zangu.
Inakuaje sikukuu hii ya kimungu inageuzwa kuwa ya kipagani kihivyo? Kama hii sio laana ni nini? Baa nazo zimejaa hakuna pa kutema mate. Ni kama vile watu walikuwa wanaisubiri siku hii kwa hamu ili wapate kulewa na kuzini.
Tujifunze kumuogopa Mungu ndugu zangu. Na tuepuke miadi yoyote ya kingono kwenye siku hii takatifu. Naona watu wa Mungu wanaangamia sio tu kwa kukosa maarifa lakini pia kwa kujitakia wenyewe.
Nawatakia krismas njema. Mungu awabariki