Leo ni sikukuu ya kugegedana?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,478
17,676
Nipo hapa mtaa wa kati nafanya utafiti binafsi. Asilimia kubwa ya watu, hasa vijana na watu wa umri wa kati, wapo wawiliwawili (bond) na wanaonekana wapo kimahaba zaidi.

Nimepita mitaani, kwenye baa, groceries, na maeneo mengine ya kujipumzisha hali ni hiyohiyo. Kilichonitisha zaidi ni pale nilipopita kwenye guest houses zilizopo maeneo haya kuanzia mishale ya saa 7 adhuhuri na kukutana na maandishi: 'VYUMBA VIMEJAA!'. Nimefanya utafiti kwenye nyumba zipatazo 8, zijapata hata chumba kimoja cha wageni kilicho wazi! Yaani haya ni maasi ndugu zangu.

Inakuaje sikukuu hii ya kimungu inageuzwa kuwa ya kipagani kihivyo? Kama hii sio laana ni nini? Baa nazo zimejaa hakuna pa kutema mate. Ni kama vile watu walikuwa wanaisubiri siku hii kwa hamu ili wapate kulewa na kuzini.

Tujifunze kumuogopa Mungu ndugu zangu. Na tuepuke miadi yoyote ya kingono kwenye siku hii takatifu. Naona watu wa Mungu wanaangamia sio tu kwa kukosa maarifa lakini pia kwa kujitakia wenyewe.

Nawatakia krismas njema. Mungu awabariki
 
kama x mac tu vyumba vimejaa..je valentine day ikifika itakuwaje????tumuogope mungu jamani..xmac njema na kwako pia mkuu..
 
Nipo home na ma wife,my daughter yupo disco jirani natoka kumfuata sasa.!
 
Huo muda uliozurura ungekwenda kutembelea hata wagonjwa mahospitali
Naye anatafuta guest kwan yupo na mgeni!TOKA KWENYE GUEST ZA BUKU 10,TAFUTA KUANZIA 25,000/=KM SALIO HALITOSHI HYO BUKU 10
Mpe huyo mgeni wako afanye nauli then vizia km mwaka mpya atapewa ruhusa na walezi wake..!
 
niko IPINGA familia, yangu hotel niliyoshukia hostel zote zimejaa.
sasa je tuseme na huu ni uzinzi??
 
Watu wamejichanga mwaka mzima...Hiki ndo kipindi cha kutumbua mzee....

Ila kwa kiasi..Hii sikukuu ni yakifamilia zaidi..
 
Kristo yesu amezaliwa!!!!!Amezaliwa kweli kweli, Na wale wote watakao mpokea wataitwa watoto! Hii ni siku ya amani, Upendo na kutenda yaliyo mema! Mungu atubariki sana.Amen!
 
kama x mac tu vyumba vimejaa..je valentine day ikifika itakuwaje????tumuogope mungu jamani..xmac njema na kwako pia mkuu..

asante mkuu. tuzidi kumuomba Mungu atutue huu mzigo wa dhambi tuliobebeshwa na shetani na kwa kuwa Mungu ni mwema nina imani atasikia kilio chetu.
 
Huo muda uliozurura ungekwenda kutembelea hata wagonjwa mahospitali

nilikuwa nishatoka hospitali mkuu, tena niliyoyakuta huko hospitali siwezi hata kuyasimulia--yaani kinamama waliojifungua wanalalishwa kwenye sakafu eti!
 
Naye anatafuta guest kwan yupo na mgeni!TOKA KWENYE GUEST ZA BUKU 10,TAFUTA KUANZIA 25,000/=KM SALIO HALITOSHI HYO BUKU 10
Mpe huyo mgeni wako afanye nauli then vizia km mwaka mpya atapewa ruhusa na walezi wake..!

mkuu, kazi yangu ilikuwa ni kufanya utafiti tu. sikuwa na ajenda nyingine zaidi ya hiyo.
 
aisee, labba hao .ni wageni wa nje ya mji ....

ni wa hapahapa mtaani. kwenye vitabu vya wageni mtu anasaini anatokea kinondoni na anakwenda kinondoni--mgeni gani huyo?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom