Leo ni siku yangu.... Naaum

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,712
Nikiangalia nyuma yangu naona nyayo juu ya mchanga mkavuu zikianzia mbaaali ya tokomeo la kutoonekana how i started walking this far.

Nyayo hizi zimebeba kajitu fulani ka hovyo hovyo ambako kama hatosimulia undani wa maisha yake basi utabakia unabung'aa na kumuangalia akipita zake taartibu kuelekea utu uzima na uzee wake.

I have been there and I did that
Mdadisi
Mtukutu
Msanii (Arts)
Mtulivu
Mpole
Muaminifu
Mkarimu
Rafiki
Infidel
Kuchepuka
Janja janja
Kiongozi
Baba
Kidume
Chaputa
Mjasiriamali
Thinker (Positive)
N.k (Nimeshindwa kuendelea)

Haunidanganyi juu ya hayo niliyoyabandika hapo juu. Lakini kuhusu maisha walah hakuna jambo gumu kama kuelezea ladha ya maisha hasa pale unapokuwa ktk hali mbanano. Kuna wakati maisha unayaona ni msereeeko lakini here comes a time when maisha ni mwinuko mkali sana.

Mama yangu aliniusia kwamba, mwanangu ukiona maisha yako yanapanda juu bila kupitia changamoto kadha wa kadha basi ujue kuna tatizo. Ni sahihi sasa kwamba ninaleta kwenu methali kwamba UZOEFU HUJA KWA KUTATUA CHANGAMOTO....

Mzee wangu ( R.I.P), alineleza kuwa, mtu anapokushauri pokea ushauri huo kisha angalia kama unakufaa au haukufai. Lakini kama atakushauri na kukulazimisha kuufuata ushauri wake basi fahamu ushauri huo una tatizo.....

Nimewanukuu wazazi wangu kwa sababu ninawatunuku leo kwa maisha waliyonikuza. Ninawashukuru kwa kuniwezesha kuishi na watu vizuri leo. Ujasiri na ukunjufu wa moyo na kushuruku ndiyo daima dira ya maisha yangu.

Napenda kujipongeza leo kwamba ninatimiza miaka kadha wa kadhaa juu ya uso wa dunia.

Namshukuru Mungu Baba kwa kuniweka hali mpaka sasa.
Nashukuru familia yangu na mke wangu kwa kuwa nami hadi sasa

Nashukuru familia ya JF hasa ninyi mnaousoma huu uzi wangu.

Naam. Leo ni siku yangu ya kuzaliwa....
IMG-20191126-WA0056.jpeg
 

Attachments

  • IMG-20191130-WA0065~2.jpeg
    IMG-20191130-WA0065~2.jpeg
    16.4 KB · Views: 1
Kuna mtu huku yupo kwenye siku yake/zake.

Mkuu hilo beseni la Mihogo ni biashara au umemuita.

yule maza anaetembeza akukatie kipisi Uchaji betri?
 
Back
Top Bottom