Leo ni Siku ya Matumizi ya Choo Duniani: Je, Tanzania vyoo vinatosheleza mahitaji ya wananchi wake?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,319
Swali ni hili, je unadhani Nchini Tanzania vyoo vinatosheleza mahitaji ya wananchi wake?

Mashuleni, Mahospitalini, Masokoni, Maofisini, vituo vya mabasi hali ikoje?

19.11.2021_Ni_Siku_ya_Choo_Duniani%2C_tazama_mchoro_wa_Said_Michael_na_kisha_toa_fkra_zako_kwa...jpg
 
•√√ Shida hazijawahi kuisha mpaka mwanadam anaingia kabulini, maisha yake ni shida tupu, hivyo hivyo na vyoo haviwezi kutosheleza huko shuleni ndo unakuta matundu 6 ya vyoo then wanafunzi 500 hapo unategemea nini kama siyo UTI sugu, maana usafi tu shida nyingine. Nenda sasa vituo vya mabasi huko ndo kuna kasheshe.
 
Swali ni hili, je unadhani Nchini Tanzania vyoo vinatosheleza mahitaji ya wananchi wake?

Mashuleni, Mahospitalini, Masokoni, Maofisini, vituo vya mabasi hali ikoje?

View attachment 2016335
Vyoo vya aina gani?
 
Niliwahi kuishi Umasaini (mojawapo ya wilaya za Mkoa wa Arusha) mwaka fulani. Wamasai wana mila ngumu sana. Baadhi ya mila hizo zina hatarisha hata afya zao. Mfano ni hii ya baba wa familia kutokuwa tayari kutumia choo kimoja na wanafamilia hususani mkewe na watoto. Kwao ni kinyume na mila mtoto kumwona baba anakwenda kujisaidia.

Hata serikali ikiwalazimisha kujenga vyoo hawavitumii. Wanaume wanaendelea kwenda kujisaidia vichakani. Masika moja mvua ilinyesha ya kutosha. Maji yakavipitia vinyesi vyao na kwenda kuvirundika kwenye mabwawa. Wakaanza kuchota yale maji na kuyatumia pamoja na kunywa bila kuyachemsha. Kipindupindu kikawapitia na kuwatikisa. Hali haikuwa nzuri kwa kweli
 
apa jinani wameleta gari la kunyonya ma..88*8vi yaaaniii kimba kinanuka hatariiii

watu wa dar na uhaba wa mwaji mwaishijee kwenda maliwatoooniii
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom