Leo ni siku ya kuzaliwa CHADEMA. Je, CHADEMA imefanikiwa?

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,622
2,000
Wakuu kwa mujibu wa mbunge Cecilia Pareso(CHADEMA) bungeni Dodoma leo mchana akichangia bungeni ni kuwa chadema leo wanaadhimisha miaka 28 tangu kuanzishwa. Hii imekuwa surprise kwangu lakini nahisi pia wana Chadema humu JF wengi wao hawajui maana walivyo hii ingekuwa post namba moja kwa leo.

Pamoja na panda shuka ya siasa za Tanzania Chadema ilipanda sana juu na leo tunashuhudia chama kikielekea kufa kabla hakifikisha miaka 30 ya ujana wake hii inamaana kama angekuwa ni binadamu angekuwa amefariki akiwa bado kijana mdogo bila kutimiza marengo /ndoto zake.

Chadema inauwawa na adui walikuwa wanapambana naye wa rushwa, upendeleo, udikteta, ukandamizaji,na ukanda. Adui hawa waliipandisha Chadema na sasa ndio wanaitafuna kabla haija pewa nchi kwa mifano.

A) Wanao ondoka chadema wanalalamika ubabe wa viongozi
B) Wanaoondoka wanalalamikia rushwa
C) Wanao ondoka wanalalamikia mbinyo wa demokrasia chamani
D) Wanao ondoka wanalalamikia upendeleo na ukanda ndani ya chama

Happy birthday Chadema ingawa tupo kwenye tuhuma nzito.

USSR
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom