Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Kwa yeyote yule ambaye amekuwa akifuatilia mwenendo wa siasa hapa nchini, atakubaliana nami ya kwamba baraza la mawaziri lililotangazwa hivi leo, limekuwa ni pigo kubwa kwa wanamtandao maslahi, kwani linaonekana kuathiri mkakati uliokuwa umesukwa na kambi hiyo kwa minajili ya kumsafishia njia Lowasa ya kwenda ikulu. Ingawaje bado ni mapema, kufuatia uteuzi wa baadhi ya waasimu wake katika baraza jipya la mawaziri, baadhi ya wadadisi wa mambo wameanza kujenga hisia ya kwamba, JK uenda akajitenga mbali na kambi ya Lowasa.