Leo ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwangu, na haya ndiyo niliyojifunza hapa duniani

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
406
1,030
2799544_PhotoRoom-20210527_234754.jpg

Leo tarehe 06/06 ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwangu, siku niliyokuja hapa duniani.

Katika kipindi hiki kifupi ambacho nimekuwa hapa duniani, nimepata fursa ya kujifunza mengi kuhusu maisha, watu na mafanikio kwa ujumla kupitia maisha niliyopitia ukiunganisha na mambo kadha wa kadha ninajiona nina bahati na nimeendelea kushirikiana na kufanya kazi na watu mbalimbali.

-irwpu8.jpg

Tarehe 25/12/2003 Nyasubi Kwa Machage Julius nikiwa na dada zangu pamoja na kaka zangu.

Kwa miaka nane iliyopita, tangu 2014 nimekuwa ni mfuatiliaji mkubwa wa makala na waandishi mbalimbali pia ni mara ya kwanza kuandika makala maalumu ya siku ya kuzaliwa kwangu, nimekuwa mfuatiriaji mzuri sana wa makala kutoka katika blog mbalimbali tangu mwaka huo nilioanza kuwa mpenzi mzuri na mfuatiliaji wa makala zinazonifua bong.

Mwaka 2014 nikiwa Kigoma kwenye kampuni ambayo sitaitaja jina na ndio nafanya kazi mpaka sasa. Kuna mengi niliyojifunza kwenye maisha na kuona mwelekeo wa jinsi watu wanavyo weza kuwa na huduma mbalimbali, ambazo zinawafanya kubadilika na kuwa wema na wengine kulewa na mabadiliko hayo pia wasiweze kujitambua wanahitaji nini ili wayabadili maisha waliyoyakuta kwao.

Mwaka huu 2021 nilipanga kujipa ujumbe muhimu sana kwangu, na ujumbe huu utani rahisishia mambo mengi sana katika utafutaji wangu. Utakaoniwezesha kuyabadili maisha yangu na kunifikisha kwenye mafanikio makubwa.

Kabla ya ujumbe huu niliojiandalia leo nichukue nafasi hii kukushukuru rafiki yangu, kwa namna ambavyo tumekuwa pamoja tangu nimeanza kutoka nje na mazingira ya nyumbani rasmi mwaka 2009.

Kila nikikumbuka nilipoanzia na jinsi mambo yalivyo kuwa magumu, najua bila kupambana na kujiwekea nia nisingeweza kupiga hatua na kufika hapa nilipo sasa.

Nilianza na kufuatilia maisha ya watu wa halibya chini niliokuwa nikiwaona na nilifanya ufuatiliaji wa watu waliopiga hatua hivyo nioijiridhisha kuwa kuna siri kubwa sana imejificha juu watu wenye navyo na wale wenye uwezo wa hali ya chini.

Hivyo kutoka ndani ya nafsi yangu kabisa namshukuru kila ambaye amewahi kunisapoti na yote niliyopitia, kwa sababu amechangia sana kukua kiakili na nimeimalika mno najiona kama niko na jeshi la watu 50 kwa sababu niliyopitia yameniimalisha sana.

Siyo kazi rahisi kutoka kwenye jamii yetu ya Kitanzania, jamii iliyojaa watu waliokata tamaa na ambao wanafurahia kuwakatisha wengine tamaa. Lakini uwepo wa wachache ambao wanaelewa maisha ya utafutaji katika mazingira magumu na kuyafanyia kazi kisha kufanikiwa inanipa moyo kuendelea na mapambano zaidi.

Kama ambavyo nimewahi kujiahidi huko nyuma, katika maisha yangu haya pamoja na magumu nayopitia na vitu nimejiapia kuja kumiliki nitaendelea kupambana ili nione ndoto yangu ikitimia ziku zijazo za lasi hivyo nitapambana na kufa kupona maisha yangu ya badilike hadi siku naondoka hapa duniani, hivyo uwepo wako unanisaidia kukamilisha azimio hilo.

1. IMANI 2. UWEZO 3. FANYA ni maneno matatu ninayoyafanyia kazi kila siku.

Malengo yangu makubwa mawili bado yako pale pale na sijawahi kuyumba kuhusu kuyafikia. Najua wapo ambao walinijua baada ya kuanza kazi katika kampuni moja niliyopo ila hawawezi kunijua zaidi maana na wao wamenikuta nikiwa na maisha nje na kampuni hii niliyopo.

kuyatangaza malengo hayo makubwa ni wazi kuwa kila mtu, lazima awe na ndoto hakuna mtu ambae hana ndoto ya maisha yake hivyo inanibidi kuwa na mawazo ya kunifanya niweze kuwa mtu wa tofauti kila siku ili niweze kuya jenga mazingira kadri inavyo niruhusu.

Katika watu nao share nao mambo mbalimbali huoyesha kuwa hawaamini kua inaweza kutokea na kuwa na maisha tofauti na nilivyo sasa. Nataka ni kwambie hivi hata wewe msomaji wa makala hii ingawa haikuhusu ila hakikisha maisha yasikufanye kuwa mtu wa kupangiwa itafikia hatua mpaka unapangiwa jinsi utakavyo weza kuishi wakati uwezo wa wewe kuwa unavyo taka unao. Kwa nini uwe mtu wa kuendeshwa ina maanisha hata hapo ulipo umesogezwa hujatumia maarifa yako kumbuka na hao wanao kupushi kwa namna hiyo wataondoka au watajitenga na wewe muda wowote utaendeshaje maisha kwa akili ya kushikiwa.

Ninachoshukuru sijawahi kupanga kitu nikashindwa kukitekeleza, Baada ya utangulizi huo muhimu, sasa nikushirikishe ujumbe muhimu wa siku hii ya kuzaliwa kwangu.

NAOMBA NIKUPE SIRI YA VITU VIWILI VYA KUFANYIA KAZI KWENYE MAISHA YAKO.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa na kuacha alama hapa Duniani, kuna vitu viwili vikubwa unavyopaswa kuvifanyia kazi. Nimeweza kuja na vitu hivi viwili baada ya kujifunza na kutafakari kwa kina na kuona jinsi watu wanahangaika na mambo mengi lakini hawapati matokeo yoyote makubwa.

Ukiamua kuachana na mengine yote unayoyahangaikia na kuyafanyia kazi haya mawili tu, utaacha alama kubwa hapa Duniani.

Mambo hayo mawili ni;
1. KUJUA NA KUISHI KUSUDI LAKO na
2. KUWA NA NDOTO KUBWA;
unazofanyia kazi kwenye maisha yako. Haya mawili tu ndiyo yanahitaji muda, na umakini wa nguvu zako zote ili uweze kufanya makubwa makubwa kabla ya umri kukutupa mkono na kabla ya kuondoka hapa duniani.

HILI NDIO KUSUDI AMBALO LITAIMARISHA MAISHA YAKO.

Nukuu'
Mark Twain
amewahi kusema “kuna siku mbili muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, siku ya kuzaliwa kwake na siku anayojua kwa nini amezaliwa”.

Kila mtu huwa anazaliwa, ndiyo njia pekee ya kuja hapa duniani. Lakini ni wachache sana wanaojua kwa nini walizaliwa na hao ndiyo wanaoleta matokeo makubwa na kuacha alama hapa duniani.

Bahati mbaya ni kwamba, kujua kwa nini umezaliwa ni wajibu wako mwenyewe, hakuna anayeweza kukufundisha wala kukuambia. Hata wazazi waliokuzaa hawajui kwa nini ulizaliwa. Walimu wanaokufundisha ndiyo kabisa wanaharibu wanasukuma bora liende, maana wanakulazimisha uwe kitu kingine na siyo wewe.

Tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye maisha yetu ili uweze kujua kwa nini ulizaliwa, unahitaji kuvunja mazoea mengi uliyojenga kwenye maisha yako ili uweze kuisikiliza sauti ya ndani yako na kujua kwa nini uko hapa duniani usiishie kuwa mkia, mkia sikuzote hauna habali na yanayoendelea.

Wengi hawajui kusudi la maisha yao kwa sababu wameamini kile ambacho jamii na mfumo wa elimu umewalisha kwa miaka mingi. Kama shule ilikuambia umefeli kwa sababu huna akili, unaamini hivyo kwamba huna akili. Wakati shule haiwezi kupima uwezo mkubwa ulio ndani yako, kitu ambacho shule inapima ni kukariri.

Ili uweze kujua kusudi la maisha yako unahitaji kurudi kwenye maisha ya utoto wako, na kusema ndiyo kwa kila kinachokuja mbele yako. Jaribu mambo mengi uwezavyo, fanya kila kinachokuvutia kufanya na kadiri unavyofanya hivyo utaona kuna vitu unapenda kuvifanya vizuri zaidi na watu wanavifurahia unapovifanya. Hapo ndipo utajua kusudi lako lilipo na kuweza kulifanyia kazi.

Nilijua kusudi la maisha yangu baada ya njia iliyokuwa imenyooka kuzimika ghafla. Nilikuwa mzuri wa kufanya maisha yangu yabadilike na nilijiona nimeyapata maisha, kumbe bidii yangu haikuwa kitu zaidi ya kupata kazi na kufanya vitu ambavyo sikuona manufaa navyo, katika ulipwaji wangu kipindi nafanya kazi bado huwa natafakari ilikuwaje nikashindwa kufanya makubwa kipindi kile nakuja kushtuka wakati amabo sina uwezo huo. Maisha mazuri yanatokana na jitihada zako na jinsi unavyojingeza, kuna watu wamekuta kazini na sasa wamejiajiri ila mimi bado nipo nipo tu huwa najiangalia mpaka najidharau maana ni aibu kubwa kama kutanguliwa na aliye kukuta na akakuzidi.

Bidii nikapata mafanikio zaidi ya ulivyo kuwa sasa ukijichanganya utakuja kujuta, ndoto zako huwa zipo kwenye kile unachokifanya ukifanya huku unaamini sijui itatokea uwe tofauti hutoweza maana utakuwa umejijazia uwoga na hutakuwa na maamuzi yeyote ya kujiongoza mwenyewe.

Nikiwa darasa la tatu, mwaka 2005 nilijiwekea nadhili na ikawe kuazia sasa ninapoingia darasa la tatu sasa sita enda shule peku peku matokeo yake nilijipa muda na wakufanya kazi nazozimudu kulingana na umri wangu katika kipindi hicho, kazi niliyoifanya ya kwanza ilikuwa ni kuokota vyuma chakavu ili niweze kujinunulia sale za shule na hata viatu pia, kwa kipindi hicho soko la chakavu lilikuwa ni Tsh 60 kg. Nilihakikisha naweza kujiwekea msimamo kuwa kila siku na weka na kila wiki naenda gulioni kununua vifaa vya shule na iliwezekana.

Katika maisha mengine ninayoishi sasa huwa siamini kuwa nyuma siku zote nataka niweze kuwa mbele na nyakati zinavyo tutaka katika hali ya kujichanganya na maisha. Baada ya kumaliza shule ya msingi nilifanya kila kilichopita mbele yangu.

1. Nilijifunza uselemala kazi yangu ya kwanza ya uselemala nilitengeneza stuli ingawa stuli hizo nilizurumiwa na fundi wangu yaani mmoja ya walimu wangu walio nifundisha selemala.

2. Nilijifunza kudalalia wakulima wanapoleta mizigo yao mfano mpunga ndio haswa ilikuwa bishara kubwa niliyoifanya katika kiwanda cha mpunga kilichopo kahama.

3. Nilifanya kazi ya saidia fundi na baadae nikaunga humo humo kujifunza ufundi ujenzi katika muda wa mwaka mmoja wakati bado sijapata mchongo sehemu yeyote.

4. Wakati nimepata ajira 2013 baadae mwa mwaka wa 2014 ndipo nilianza kusoma vitabu na makala mbali mbali na baada ya hapo, nilijifunza kutengeneza blogu, mpaka leo hii bado mimi ni msomaji mzuri wa vitabu na hunisaidia kuongeza maarifa na kujifunza mengi jinsi mashujaa walivyopitia magumu ila hawakuishia kukata tamaa.

5. Bado naendelea kufanya bisahara biashara za fedha katika kampuni flani hapa Tanzania.

Katika kipindi hicho sikusema hapana kwenye chochote kilichokuja mbele yangu, nilisafiri maeneo mbalimbali kila niliposikia kuna fursa fulani huko. Nakumbuka katika hicho kipindi tuliwahi kusafiri na mjomba wangu kwenda.

Sehemu moja inaitwa Kiagata nikiwa huko Musoma nilienda kufanya kazi ya ujenzi wa kalavati kwenye mto nyarusondobhilo. Baadae tena nikasafiri ni kiwa na rafiki wa mjomba wangu kwenda semehu moja inaitwa Nyarwana pembezoi na milima ya Tarime hizi ni moja ya safari ambazo mpaka sasa nazikumbuka kwa sababu ziliingia katika historia yangu ya maisha ya utafutaji.

Ni katika kipindi hicho kilinijenga sana na niliapa kuheshimu mazingira yeyote ya utafutaji na niliona yale ndio maisha wanayoishi hata watu wengine hivyo nilishukuru kupata mafunzo ya kunijenga kiakili na kiutafutaji pia. Binafsi ndio maana nina soma sana vitabu vya maendeleo.

Nakumbuka Januari mwaka 2017 baada ya kuona hakuna mwelekeo wowote, nilijiambia sasa napaswa kushika hatamu ya maisha yangu.

Nimekuwa nikitumia msemo huu “keep the faith” ndiyo msingi wa maisha yangu, niliwezesha kuiona dunia kwa mtazamo wa tofauti na hatimaye kunijenga nilivyo leo. Mpaka sasa faidika na niliyopitia na yaliniweka kuwa mtu ambae niko imara, lakini nimekuwa nashauri yeyote anayetaka kushika hatamu ya maisha yake basi aanze kwa kuacha mambo ambayo hayana faida kwake na aangalie vitu vitakavyo mfanya yeye kupiga hatua.

Katika mengi niliyofanya katika hicho kipindi, kuuza mchele, kujenga ni vitu vitatu ambavyo nimekuwa napenda sana kuvifanya na sichoki hata kidogo kuvifanya. Naweza kutumia mpaka masaa 10 kwa siku nikisoma au kuandika na kupitia blog yangu. Na pia naweza kuandika mpaka maneno elfu 3 kwa siku moja, kuandika maneno elfu 1 na zaidi kwa siku ni kitu cha kawaida na wala sioni ni kazi.

Hivyo fanya kile kitu unaona kinakupa faida rafiki yangu, kama bado hujajua kusudi la maisha yako, chagua kipindi utakachorudi kwenye utoto wako na sema ndiyo kwa kila kitu. Kila kinachokuvutia kufanya, kifanye. Tenga muda ambao utafanya majaribio mbalimbali kwenye maisha yako na kujifunza kwenye kila unachofanya.

Baada ya kujua kusudi la maisha yako, sasa unahitaji kuweka umakini wako wote kwenye kuishi. Hupaswi tena kuhangaika na mambo mengine nje ya kusudi hilo.

Muda na nguvu zako vina ukomo, usipoteze kuhangaika na mambo mengine. Kuna mazuri yatakayokuja kwako na yenye fursa ya kunufaika zaidi, lazima uweze kusema hapana kwa hayo mazuri ili uweze kupata yaliyo bora kupitia kuishi kusudi lako.

Baada ya mimi kujua kusudi langu nimekuwa na nidhamu na kazi na nikotayari kutokula hata siku nzima ili niweke elf 2-3, najua najitesa ila bado naamini kuwa ninachokifanya kitaniweka mahara pazuri baadae na katiki kulifanya hivyo nimeona matunda na nimejionea mwenyewe hatua zangu ninazo pigania. Nimekuwa nasema hapana kwa mengine yote isipokuwa kusudi hili.

Baadhi ya vitu nilivyokuwa nafanya awali huwa naamini muda utaongea kutokana na mambo ambayo nimevuka na kilichonisaidia zaidi ni namna ya kuya mudu na mpaka sasa nimefika hapa nilipo, lakini kwa sababu sitaki kutoka kwenye kusudi nimekuwa nasema lazima nipambane iwe usiku iwe mchana.

Najua kuna wengi wanasema hapana sitaweza kwa sababu nafasi nilizopata kutengeneza maisha ni nyingi na wengu husema nilichezea bahati na wanaenda mbali zaidi wanasema bahati huwa haiji mara mbili. Nataka niwahakikishie kwamba, nyakati nilizopitia zimenijenga mpaka hapa nilipo nimejiona kama nimeshinda hivyo wategemee kuona muujiza ukiwaangukia mbele yangu. Mtu ambae haamini hutegemea kuona kwa macho ya nyama hivyo basi nami nataka niwaonyeshe kuwa nimepambana na nilipo sasa niko namalizia hatua za mwisho. Ndio kwa mambo haya nategemea Kunanigharimu kwa kiasi kikubwa, lakini nikisema ndiyo itanigharimu zaidi baadaye. Juhudi ninazoweka kwenye kusudi langu kwa sasa ninajua zitazalisha matokeo makubwa sana baadaye kuliko nikihangaika na mambo mengine.

Ukishajua kusudi lako, yapangilie maisha yako kwa namna ambayo unaishia na katika harakati zako pia hakikisha huishi nje ya misingi uliyojiwekea vinginevyo hutoweza kuishi kusudi hilo, ndiyo kipaumbele kikubwa kwako na ukisema hapana kwa mengine yote ambayo haya husiani na kusudi hilo utegemee kuinamisha kichwa chini yaani ukifikia hatua hiyo jua umesalimu amri.

Ni kwa njia hiyo ndiyo unaweza kuweka umakini, muda na nguvu za kutosha kwenye kusudi lako na liweze kuleta matunda mazuri kwako.

NDOTO KUBWA ZA MAISHA YETU.

Maisha yasiyokuwa na ndoto ni maisha ambayo hayana msukumo wa kuyaishi.

Kama unataka kuacha alama hapa duniani, lazima uwe na ndoto kubwa, lazima uwe na picha ambayo hakuna anayeiona na hata ukiwaambia wengine hawaamini kama inawezekana.

Ukishakuwa na picha hiyo kubwa, unapaswa kuifanyia kazi kila siku mpaka utakapoifikia. Unapaswa kuwa tayari kutoa kafara ya kila aina kwenye maisha yako ili kufika kwenye ndoto yako kubwa.

Hii sitaielezea sana kwa sababu ni mchakato mkubwa na ndiyo kitu tunachofanyia kazi, maisha yetu hayako salama kama wewe hautakuwa tayari kujiimalisha ili uweze kujitoa kama uliyojifunga.

Pia utakuwa na ndoto yako kubwa, unayopambania kila siku ili kuifikia.

Ni sehemu pekee ambapo utapata msukumo mkubwa wa kuyabadili maisha yako na kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa na kujia alama.

Nimalize kwa kukushukuru zaidi wewe rafiki yangu, uwepo wako umekuwa wajibu wa maisha yangu na karibu sana tuendelee kuwa pamoja kwenye safari hii ya mafanikio.

Rafiki yako anayekupenda sana,

© 2021 Jumanne
 
Hv mnaofurahia siku ya kuzaliwa ,hivi huwa mnafurahi kutoka moyoni au ndo upepo wa kuiga iga mambo...hivi unakuwa umefanya jambo gani la kukumbukwa hapa Duniani mpaka ufurahie siku yako ya kuzaliwa?
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom