Leo ni siku ya kukumbuka kifo cha hayati Mwalimu J.K. Nyerere

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,826
966
Habari wanajamvi.

Ninaposema leo ni siku ya kukumbuka kifo cha hayati Mwl. J. K. Nyerere sina maana kuwa watu hawajui, la hasha. Ila ninachotaka kuongelea ni juu ya sintofahamu ya ustahimilivu wa serikali yetu tukufu inayoendeshwa kwa hisia za KUSADIKIKA.

Neno hili limetumika vibaya sana katika utawala wa Rais wa awamu ya nne. Baadhi ya mifano hai ya matumizi ni: (nitaanza na mpya)
1. Inasadikika vijana wenye siraha wameandaliwa ili kufanya fujo wakati Mh. Rais atakapo wasiri shinyanga hata hivyo polisi imeimalisha ulinzi.

2. Inasadikika RPC wa Mwanza ameuwawa na majambazi.

3. Inasadikika David Mwangosi alitumwa na CHADEMA kupigana na polisi.

4. Inasadikika kijana aliyeuwawa mjini Morogoro alipigwa na kitu kizito chenye ncha kali kinachosafiri angani.

5. Inasadikika mtu aliyemteka Dr. Ulimboka ni mkenya.

6. Inasadikika wabunge wa CHADEMA waliovamiwa mwanza walivamiwa na majambazi na kujeruhiwa.

7........

Ni baadhi tu ya matukio ya KUSADIKIKA, Swali je, ikitokea siku ikaSADIKIKA kuwa nchi imeuzwa na tumekuwa watumwa napo itakuwa KUSADIKIKA?
 
Nimejitahidi kutuliza akili bado sijakuelewa.Mimi nakushauri tu lea mtoto wako achana na mambo ya kusadikika
 
Hahahaha! Jf bwana yani Asubuhi tu ndo nastuka nakutana habari za kusadikika! Haya ngoja tusubiri wenye kusadikika zingine waje!
 
Tuna muenzi kama rais wa kwanza, mafisadi leo wanacheka na kufurai kwani baba wataifa asingekubali upuuzi huu usingekuwepo wa wizi, madini yatoroshwa kili siku, hichi chama cha mwabepande mwisho wao 2015
 
'Ugonjwa huu sitapona,ninawaombea watanzania, amani idumu' Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ya Hayati,Kambarage Julius Nyerere. Kutokana na vyanzo mbalimbali vya kihistoria, jambo moja kubwa kati ya mengi aliyoyaamini ni Haki. Ni wazi sasa, baada ya kifo chake mambo mengi yamepotoshwa na baadhi wamejitosa katika mbio za kumchafua Mwl.Nyerere...sijui ni kwa maslahi ya nani? Mwl.Nyerere alipenda watanzania wapate haki ya kutawala rasilimali na kunufaika nazo. Mwl.Nyerere aliamini kwamba,endapo utawala ni wa kifisadi,uliojaa wala rushwa basi serikali hiyo (corrupted regime) haitakusanya kodi ila itabaki kufukuzana na machinga barabarani. Hakuamini katika urafiki baina ya watawala na wafanyabiashara ili kuepusha kusamehe kodi bila sababu za msingi..La sivyo tutashuhudia matajiri sana ila wachache na masikini sana wengi katika taifa...Tunamuenzije Mwalimu?
 
wewe ndio tukuulize unafanya haya kwa maslai ya nani? kila mtu mwenye akili timamu anajua Nyerere ndio chanzo cha matatizo yote tuliyonayo watanzania
 
Ndugu zangu,

Leo ni siku ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Asubuhi hii hapa Iringa najiandaa kwenda kwenye mjadala ulioandaliwa na Kigoda Cha Mwalimu pale Chuo Kikuu cha Mkwawa. Hapo kuna mada yenye kuhusisha suala la Muungano kwenye uandikaji wa Katiba Mpya. Nimeambiwa, kuwa kutakuwa na wazungumzaji mahiri, akina Zitto Kabwe, January Makamba na wengine.

Hawa ni vijana pia. Nitapenda sana kwenda kuwasikiliza na kujifunza. Lakini, tunapozungumzia Muungano kwenye kuandika Katiba mpya inahusu pia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ambao Mwalimu Nyerere aliuanzisha, aliusimamia, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Inahusu Mradi wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa. Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).

Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.

Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia. Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu.

Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Watanzania wengi sasa wanaopoteza moyo wa uzalendo kwa nchi yao.

Kuna hata wenye kufikia kutamka; 'Nchi hii ina wenyewe'. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali.

Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa. Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.

Ni hatari. Tuna lazima ya kuwa na ujasiri wa kupigania maslahi ya nchi yetu. Ni heri kufa kwa kupigwa risasi kuliko fedheha ya kufa kwa kuumwa na mbu wa Malaria katika nchi ambayo ina rasilimali za kutuwezesha kujenga uwezo wa kuangamiza malaria.

Lakini, tunakubali wachache miongoni mwetu wahujumu rasilimali zetu. Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo.

Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili. Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania.

Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.

Na hilo ni Neno la Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa,

0788 111 765
 
Umesomeka maggid, wenye kulifanyia kazi watalifanyia na wenye kulipuuza watalipuuza, binafsi huwa nasikliza hotuba za mwalimu hata kama sio siku ya kumbukumbu ya kifo chake na usemalo ni kweli umoja wa Taifa hili unaporomoka kwa kasi sana na viongozi wetu sio kwamba hili hawalioni la hasha! Wanaliona lakini hawajali bali wanaamini huo msemo unaosema hii Nchi ina wenyewe na wanaamini wao na familia zao ndio wenye hii Nchi lakini mwisho wakle nadhani si mzuri.

Jana kuna mtu kaweka Picha ya Nyumba za Mh. Yona watu wamejadili lakini si kwa nia njema maana wanajua ni kodi na rasilimali zao ndio zimemfanya huyo bwana akawa tajiri, jana yameripotiwa mauaji ya Kamanda huko Mwanza, watu wamejadili wengi wakifurahia hayo mauaji, ukiangalia sana utagundua umoja wa Kitaifa hakuna na watu ni kama wanawindana vile.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Last edited by a moderator:
Ni miaka 13 imepita tangu kuondoka kwa mzee. Nimekuwa natafakari aliyofanya na najua mengi hayakuwa mazuri. Nchi sasa imeuza kila kitu na ikulu imekuwa haikaliki rais kila siku yuko nje! Tufanyeje ili kuwe na nidhamu ikulu? maisha yamepanda aaggrr!
 
[h=5]Nuru imepotea, Nuru ambayo kwayo tulikuwa tunaona Tanzania yenye matumaini na neema mble. Kuondoka kwake kumewafanya wanyang'anyi kuchuku hatamu na kuigeuza nchi hii bidhaa na kuiuza katika soko lisilojali mwenye nancho anafaidika ama la. wametuhujumu, wameuza rasilimali, wametunyang'anya vilivyo vyetu, wanatujengea chuki (UDINI) ili uwe mtaji kuongoza watakavyo.....

Ninasema ni unafiki mkubwa kama kiongozi yeyote wa nchii hii akitokea leo na kujifanya anamuenzi MWALIMU....anastahili kupigwa mawe hadi kufa.... inasema hivi maana kwa uelewa wangu hawawezi kumuenzi Mwl siku ya leo tu,,, walistahili kumuenzi kwa kuendeleza yale mengi mema aliyoyafanya na kurekebisha pale alipokosea.[/h]NINASEMA KUWA HAKUNA KIONGOZI YEYOTE NCHI ANAYESTAHILI KUJITOKEZA HADHARANI KUMUENZI MWALIMU NYERERE. Bado tunakukumbuka sana Mwl na pengo lako ni gumu kuzibika.
 
Wakati wa Nyerere:Ujamaa na kujitegemea
Sasa hivi:Ufisadi na kuombaomba
He was my HERO.
R.I.P Mwalimu Nyerere.
 
Back
Top Bottom