#COVID19 Leo ni siku ya Afya ya Akili, Je Watanzania tutumie chanjo ya Corona kama kipimo cha utimamu wetu?. Wapinga chanjo, sio wazima! Je ni vichaa?

Grandiosity....

Grandier delusion.....

Ni ukichaa....

Nao ni ukichaa.....

Kupenda KUONEKANA wewe ni wa umuhimu sana kushinda wengine ....wengine wote....nao ni ukichaa......
 
Baada ya pambano kati ya waliochanjwa na wasiochanjwa litafuata pambano kati ya waliochanjwa j&j na wale watakaochanja mzigo wa kichina.
 
Baada ya pambano kati ya waliochanjwa na wasiochanjwa litafuata pambano kati ya waliochanjwa j&j na wale watakaochanja mzigo wa kichina.
 
Mimi naona nyinyi mliokubali kuchanjwa ndiyo hamna akili! Kwa sababu lengo la hiyo chanjo hata halieleweki ni nini!!

Eti unaweza kuchanjwa, na bado ukapata tena hiyo Corona! Mbona kwenye chanjo nyingine hatuambiwi upuuzi kama huu?

Siku wakija na chanjo ya uhakika kwa 100%, nitachanja. Ila kwa sasa, wacha tuendelee kupigana chenga za mwili.
Kwahiyo kama wewe ukishindwa kuelewa kitu maanake hakieleweki?!
 
Wanabodi,

Leo October, 10 kila mwaka ni siku ya Afya ya Akili, kuna ule utafiti, ulioonyesha kuwa kwenye kila Watanzania 4, mmoja ana tatizo la Afya ya akili.

Matokeo ya utafiti huo, umerudiwa leo asubuhi kwenye TBC na daktari mmoja Mtaalamu wa Afya ya akili kwenye mahojiano ya kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa live kila asubuhi, leo kikijikita kwenye kuizungumzia siku ya Afya ya akili duniani.

Ili uweze kulielewa bandiko hili kikamilifu, anza na kusoma hoja za gazeti hili.

View attachment 1969920

kisha nenda bandiko hili
Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo!. Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?!.

Hivyo tunavyoendelea kuiadhimisha, ni vyema kujiuliza jee wewe ni mmoja kati ya wale wanne, ukijikuta ni mmoja wao, unaweza kujitibu kwa kujitambua tuu na kama ni serious, nenda kwa wataalamu, ila wale wenye serious critical problem, huu ni ugonjwa tuu kama ugonjwa mwingine wowote na watu wenye matatizo haya wanahitaji matibabu kama wagonjwa wengine wowote.

Kiukweli kabisa katika Jamii yetu tuna vichaa wengi kuliko tunavyojitambua. Wengi wanadhani kipimo cha kwanza kabisa cha kumjua mtu amechanganyiwa ni kuongea peke yake, hiyo ni stage ya mwisho ya ugonjwa, kiukweli kuna vichaa vichaa wengi, wanaongea vizuri tuu kama ni wazima, ila hayo wanayoongea ndio huwabainisha kuwa sio wazima!.

Miongoni mwao kuna wanasiasa, na hata viongozi wengi tuu, wakiwemo baadhi ya viongozi wetu wa dini, mtu mwenye akili timamu ukiwasikiliza kwa makini utabaini kuwa hata baadhi ya viongozi wetu wa dini, haswa hizi dini za kisasa za uchochoroni, baadhi yao sio wazima, ni vichaa kabisa, japo wana vaa very smart na kuzikusanya sana sadaka!.

Jee mnaonaje tukitumia kipimo rahisi zaidi cha kisasa cha kujipima Afya yako ya akili, ni kutumia kipimo cha chanjo ya Corona. Jiulize jee wewe unaikubali chanjo ya Corona?, ukijikuta unaikubali, then wewe ujihesabu Afya yako ya akili iko vizuri, uko sawa, hivyo kama hujachanja, nenda kachanje. Ukijikuta wewe sio kwamba huikubali na bado hujachanja kwasababu unataka kwanza kujiridhisha kuwa hii chanjo ni salama, hivyo wewe bado ni undecided, then anza kujiuliza, kama wewe ni mzima, au laa ila wale wote wanaopinga chanjo inawezekana kabisa, hawa sio wazima, ni wagonjwa wa akili, ni vichaa ila tuu hawaokoti makopo?, hivyo badala ya kuwashutumu na kuwasimanga, tunahitaji kuwasaidia ili akili zao zirudi, wote tukachanje kulinusuru taifa.

Nakutakia Jumapili njema, na siku njema ya Afya ya akili.
P
 

Attachments

  • IMG_0596.MP4
    2.5 MB
... huko Kawe patakalika? ,,, anyway, timing yako nzuri kidogo, jumapili ijayo mbali kidogo!
1f605.png
 
Zimetengenezwa chato Mkuu na si kwa BEBERUS ndiyo sababu wanameza 😜😜😜

Unamkuta mtu anaipinga CHANJO dhidi ya CORONA kwa kigezo kuwa zinatoka ULAYA kwa mabeberu....huku kila siku akimeza TEMBE DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI....sasa sijui hizo tembe zinatengenezwa Lushoto Tanga?!!! 🤣
 
Back
Top Bottom