Leo ni siku ya 191 kwenye mwaka huu, kitu pekee walichofanikiwa Chadema ni kuanzisha mikutano Twitter

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,426
Hamna CCM imara kama upinzani ni dhaifu, Chadema fanyeni kujitahidi hili kuleta amsha amsha ndani ya nchi.

Kwa kifupi mtu akisema Chadema imepoteza dira anakuwa yuko sahihi sana. Ebu tujikumbushe baadhi ya vitu vilivyofanywa na Chadema mwaka huu.
  1. Kuwatoa wabunge 19 bungeni (hapa chadema walifeli kwa 100%)
  2. Maandamano makubwa ya katiba nchi nzima (Hamna hata mtu mmoja amewahi kuandamana mwaka huu)
  3. Kumtoa Mbowe lupango (bado kamanda yuko ndani, tunamuombea atoke lakini)
  4. Kumchafua JPM duniani (hapa napo wameangukia pua- JPM ameendelea kuwa kipenzi cha watu Tanzania, Afrika na duniani)
  5. Kumtoa mama kwenye reli (mama amekataa kata kata kutoka kwenye mstari)
Kitu pekee Chadema walichofanikiwa kukifanya ni kuendesha mikutano kwa njia ya mitandao ya kudai demokrasia ambapo ukitoa maoni tofauti na yale ya Lissu, Maria Sarungi na Fatma Karume wanakupiga ban fasta (hawa ndio wapigania demokrasia wetu).

Lakini pia switch ya twitter anayo mama, nidhamu ikipungua kidogo nako pia anaweza kuzima bila shida.
 
Wakati wa Magufuli mbona atukuona mikakati ya kudai katiba mpya na hizi rapsha za sasa?
 
Bado unahangaika na chadema

Mwenzenu amehangaika mwisho wa siku amepotea moja kwa moja

Hayupo tena

Watu wanavaa barakoa aliowaacha serikalini

Watu wanahubiri chanjo

Watu wanafanya semina na warsha

Mama anasafiri nchi atakavyo na anatumia ndege kubwaaaa0

Maisha ni fumbo, Achana na chadema kula maisha

CCM na chadema zipo tu na utaziacha

Mwendazake huyo amepotea, Chadema na ccm kwanza wanaongelea katiba

Yeye ndio basi tena
 
CCM isipotolewa madarakani hii nchi itanaki kwenye maendeleo ya Makaratasi na kunufaisha Mabeberu walioko Madarakani tuu.

Nchi yenye Gesi matrilioni ya lita ardhini inategemea tozo za mafuta na simu. Pesa zinazopatikana kwa tabu za wananchi wa chini wanaokamuliwa kodi usiku na mchana.

Mafuta yakefika 2500 CCM Mabeberu watawala na wauaji wanashangilia kutumia magari ya kifahari na alawansi za mawasiliano kwenye mishahara yao mikubwa.

Magari Mabovu yamejaza kila idara huku yakipewa mgawo wa mafuta kila siku kama vile yanafanya kazi. Watu wanakula pesa zinazotokama na tozo kubwa za mafuta na simu badala ya kuuza magari mabovu yote kwenye idara za umma na kufuta malipo hewa ya vipuri na mafuta kwa magari yaliyosimamishwa juu ya mawe halafu CCM wanachekelea maumivu ya wananchi . Eti Mbowe ni Gaidi.! Magaidi na Wezi ni wale waliompiga Risasi Tundu Lisu na wakatokomea serikalini bila kujulikana.

Acheni kushangilia udhalimu.

Akina Polepole na kundi la Sabaya lililokua linatumia vyombo vya dola kufanya uhalifu wanampoteza mama ili wafanye wanayojua wao.

Mama asipowatimua ataangukuia pua mana muda sio mrefu watu watashindwa kupanda Bajaji,Bodaboda,kutuma 5000 kwenye simu, kupanda Daladala na hata kutembelea magari binafsi.
Hiyo tozo wataipata wapi?

Yani badala ya kufuta Ewura na kuacha TBS wanawaumiza wananchi.
REA ni nani na Tanesco ni ya nini?
Ujinga mtupu wa kuwaumiza wananchi ?

Chadema hata kisoponya kitu hakina madhara kwa watu maskini. Wenye hofu na Chadema ni watawala waovu ,wezi, wala rushwa ,wabinafsi,wahuni, wanaoiba mali za umma ili kufanya uzinz na ulevi na kujilimbikizia mali wakati wataziacha na watoto wao waliorithi mali za wizi na damu na vilio vya watu waloumizwa na udhalimu wa baba zao wanatawala kidhalimu zitatumiwa kidhalimu kwa ulevi,bangi , madawa , umalaya, ushoga,kuua, n.k. Dhulma haina urithi mwema . Bora basi udhulumu kwa Lugha nzuri kama matapeli lakini kama CCM na dola lao linalotumia silaha za umma kuua watu na kumbika Kesi.

Mbunge wa CCM alikutwa na mabunduki mamia lakini hakuitwa hata mwizi ,mwingine silaha haye ilikamatwa akikodisha wahalifu kama alivyokua anafanya Sabaya lakini hawakuitwa magaidi.

Mwamposa alifanya ugaidi wa wazi kwa kutumia dini na kuua watu kwa makumi lakini hakuitwa gaidi kwa sababu alikua ni kada wa CCM .
Eti gaidi na Mbowe.

Magaidi ni wale walifanya wanayojua wao kwa Meko halafu wakamficha uvunguni ili wachote pesa za umma na kusema kuwa yupo bize na anawasalimia watanzania wanyonge.

Acheni Kufurahia udhalimu wa CCM na dola lake linalowaza mali na madaraka na kurithishana utawala.

Kaeni kimya msiwashike watu mikono , muendelee kula na watanzania vipofu.
 
Mhubiri 9:5-6

5 Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
 
Wakati wa Magufuli mbona atukuona mikakati ya kudai katiba mpya na hizi rapsha za sasa?
Madai ya katiba yamekuwa na nguvu sasa kwa sababu ya matokeo ya uchaguzi wa hovyo na matendo ya kihuni ambao hayajawahi kutokea Tanzania.Kiufupi meko alikuwa ni mwongo mwongo na dhulumati.Jibu la swali lako ni kwamba kibibi alisharuhusu makongamano ya ndani kwa vyama vya siasa na hicho ndicho CDM walichokuwa wanakifanya.Nothing was wrong
 
Hamna CCM imara kama upinzani ni dhaifu, Chadema fanyeni kujitahidi hili kuleta amsha amsha ndani ya nchi.
Kwa kifupi mtu akisema Chadema imepoteza dira anakuwa yuko sahihi sana. Ebu tujikumbushe baadhi ya vitu vilivyofanywa na Chadema mwaka huu.
  1. Kuwatoa wabunge 19 bungeni (hapa chadema walifeli kwa 100%)
  2. Maandamano makubwa ya katiba nchi nzima (Hamna hata mtu mmoja amewahi kuandamana mwaka huu)
  3. Kumtoa Mbowe lupango (bado kamanda yuko ndani, tunamuombea atoke lakini)
  4. Kumchafua JPM duniani (hapa napo wameangukia pua- JPM ameendelea kuwa kipenzi cha watu Tanzania, Afrika na duniani)
  5. Kumtoa mama kwenye reli (mama amekataa kata kata kutoka kwenye mstari)
Kitu pekee Chadema walichofanikiwa kukifanya ni kuendesha mikutano kwa njia ya mitandao ya kudai demokrasia ambapo ukitoa maoni tofauti na yale ya Lissu, Maria Sarungi na Fatma Karume wanakupiga ban fasta (hawa ndio wapigania demokrasia wetu).
Lakini pia switch ya twitter anayo mama, nidhamu ikipungua kidogo nako pia anaweza kuzima bila shida
Udikteta umezidi nchini watu wanashindwa hata kufanya maandamano, inasikitisha!
 
Mama ameanza vizuri Sana na alikuwa anakwenda vizuri Sana,kwa kipindi kifupi Cha utawala wake,mambo mengi ambayo yalikuwa shaghala bagala,ameyarekebisha,watumishi wa serikalini wameahidiwa kupewa nyongeza ya mishahara Yao na madai Yao mbalimbali,watu ambao walibambikiwa case wamefutiwa/ wameachiliwa huru na wengine kurejedhiwa fedha zao za fine,Uhuru wa kusema sasa hivi hutuogopani kwa maana zile Noah zimepangiwa kazi nyingine ,kufungua milango ya biashara na nchi jirani,wawekezaji ndiyo alianza kufanyia kazi,wake kwa uwingi kuwekeza,vijana wetu wapate ajira,lakini tunaanza kumtoa katika reli,ni vema mama akapewa muda,mama ana dhamira mzuri kwa wananchi wake na taifa lake,lakini hawezi kufanya yote kwa wakati mmoja kwa sababu kuu mbili:1)Uhaba wa rasilimali fedha za kutekelezea mipangoyake 2).Ni lazima kila suala lifanyiwe uchambuzi na upembuzi yakinifu na wasaidizi wake kabla hajachukua uamuzi.Hawezi kumaliza matatizo yote aliyoyarithi ndani ya miezi mitano.Tuwe na Subira,mwanga unaokana mbele ya tanuri.
 
CCM wako busy kuwananga CHADEMA hapohapo wanasahau kuwa hayo yote wanavyosema wenzao wameshindwa yanasababishwa na mfumo tulionao ambapo chama tawala kimeshika kila kitu kuanzia bunge, mahakama na dola.
CCM wanajisahaulisha kuwa wao wameshindwa kuisimamisha hii nchi kimaendeleo licha ya tuna miaka karibu 60 ya uhuru lakini bado matatizo ni yaleyale umasikini,ujinga na maradhi
CCM wanajisahaulisha kuwa nchi hii iliongozana kupata uhuru na tiger economy countries ie malysia, Korea nk lakini mpaka leo nchi yetu ni ombaomba
CCM wanajisahaulisha kuwa licha ya kujikweza wameleta maendeleo kwa wananchi lakini bado wanaogopa uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari nk
Kiujumla ukisema CHADEMA wameshindwa anza kwanza na walichofaulu CCM ambacho ni kuiba uchaguzi kwa ngazi zote, kuendeleza ujinga ambao ndio mtaji wao, kutengeneza kikundi Cha mabwanyenye (rulling Elites/CCM and their collides)
 
Hamna CCM imara kama upinzani ni dhaifu, Chadema fanyeni kujitahidi hili kuleta amsha amsha ndani ya nchi.
Kwa kifupi mtu akisema Chadema imepoteza dira anakuwa yuko sahihi sana. Ebu tujikumbushe baadhi ya vitu vilivyofanywa na Chadema mwaka huu.
  1. Kuwatoa wabunge 19 bungeni (hapa chadema walifeli kwa 100%)
  2. Maandamano makubwa ya kkatiba nchi nzima (Hamna hata mtu mmoja amewahi kuandamana mwaka huu)
  3. Kumtoa Mbowe lupango (bado kamanda yuko ndani, tunamuombea atoke lakini)
  4. Kumchafua JPM duniani (hapa napo wameangukia pua- JPM ameendelea kuwa kipenzi cha watu Tanzania, Afrika na duniani)
  5. Kumtoa mama kwenye reli (mama amekataa kata kata kutoka kwenye mstari)
Kitu pekee Chadema walichofanikiwa kukifanya ni kuendesha mikutano kwa njia ya mitandao ya kudai demokrasia ambapo ukitoa maoni tofauti na yale ya Lissu, Maria Sarungi na Fatma Karume wanakupiga ban fasta (hawa ndio wapigania demokrasia wetu).
Lakini pia switch ya twitter anayo mama, nidhamu ikipungua kidogo nako pia anaweza kuzima bila shida
Kwa jinsi ulivyoiandika ni kama unainanga serikali kiaina.
Kuhususu kuwatoa hao covid 19 bungeni.kisheria ni kazi ya spika hivyo hapo ni spika aliyeshindwa kusimamia katiba na sheria za nchi na wala sio chadema.
2 kuhusu maandamano ya katiba mpya hakuna mahali chadema waliruhusiwa kuandamana halafu wakashindwa.
3.kuhusu kumchafua hayati siwezi kulisemea maana haipendezi kuongelea mambo ya MTU aliye kufa.
4.kuhusu kuanzisha mikutano mitandaoni hiyo ndio kazi haswa ya chama chasiasa kutumia kila aina ya jukwa kufanya ushawishi.maana siasa ni ushawishi.
5.kuhusu kumhamisha mama tayari kaisha ingia kwenye mtego wa kamatakamata.maana yeye alikataza kubamvikia watu kesi na kutaka Uhuru na haki za mwananchi vi heshimiwe ya ko wapi.
Ushauri wangu kwa chama changu ccm turudi kwenye misingi ya siasa za ushawishi .inapotokea kiongozi kakosea tumseme bilauoga kama enzi za kina kinana waliwaita mawaziri waliokua hamsaidi rais ipasavyo mizigo.na mambo yalienda.
 
Mama kajua kufanya diversion ya maana just imagine kama Mbowe asingekua temporary gaidi na ile speed ya kudai katiba kwa speed ile sasa hivi ingekuwa ni fukuto tu.

Kawapunguza speed kesi na kawapa sababu ya kufurahia ushindi pindi mahakama itakavyothibitisha Mbowe si gaidi. Chadema watakua happy na mama atakua happy kapata ule muda alioomba apewe

Maisha ni kuchagua
 
Hamna CCM imara kama upinzani ni dhaifu, Chadema fanyeni kujitahidi hili kuleta amsha amsha ndani ya nchi. Kwa kifupi mtu akisema Chadema imepoteza dira anakuwa yuko sahihi sana. Ebu tujikumbushe baadhi ya vitu vilivyofanywa na Chadema mwaka huu.
  1. Kuwatoa wabunge 19 bungeni (hapa chadema walifeli kwa 100%)
  2. Maandamano makubwa ya katiba nchi nzima (Hamna hata mtu mmoja amewahi kuandamana mwaka huu)
  3. Kumtoa Mbowe lupango (bado kamanda yuko ndani, tunamuombea atoke lakini)
  4. Kumchafua JPM duniani (hapa napo wameangukia pua- JPM ameendelea kuwa kipenzi cha watu Tanzania, Afrika na duniani)
  5. Kumtoa mama kwenye reli (mama amekataa kata kata kutoka kwenye mstari)
Kitu pekee Chadema walichofanikiwa kukifanya ni kuendesha mikutano kwa njia ya mitandao ya kudai demokrasia ambapo ukitoa maoni tofauti na yale ya Lissu, Maria Sarungi na Fatma Karume wanakupiga ban fasta (hawa ndio wapigania demokrasia wetu). Lakini pia switch ya twitter anayo mama, nidhamu ikipungua kidogo nako pia anaweza kuzima bila shida.
Ajabu ni kuwa pamoja na kuwa chadema wanafanyia mikutano twitter, lakini policcm wanahangaika nchi nzima kupambana na chadema.
 
Kitu pekee Chadema walichofanikiwa kukifanya ni kuendesha mikutano kwa njia ya mitandao ya kudai demokrasia ambapo ukitoa maoni tofauti na yale ya Lissu, Maria Sarungi na Fatma Karume wanakupiga ban fasta (hawa ndio wapigania demokrasia wetu).
😂😂😂😂
 
Kwahyo tumekubali kama nchi ,mzigo wa upinzani tuwakabidhi Chadema?waTZ sisi ni bipolar(mimi nikiwemo),wakiandamana tunasema Wana fujo,waki-stick na kuongea tu kwenye hoja wanazoziona (Chadema) ni sahihi tunasema wameishiwa mbinu,,,walitaka kukutana tukasema CoViD....

Hebu leo watu tushushe mawazo yetu,what is the perfect opposition party?Mnataka kiweje?maybe wanaweza kujijenga kupitia mawazo yetu.
 
Back
Top Bottom