LEO ni Mwaka 1 wa Ushirikiano;kuna mafanikio? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LEO ni Mwaka 1 wa Ushirikiano;kuna mafanikio?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, May 10, 2008.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tarehe kama ya leo viongozi wakuu wa vyama vya upinzani walikutana Dar es Salaam, na mbele ya baadhi ya wanavyama vyao na mbele ya waandishi wakatamka kushirikiana. Ni yapi mafanikio? how many rivers crossed so far, how many ahead,au ni ngoma ya mduara?
  Walisema hivi:
  Tamko la Wakuu wa Vyama Juu ya Ushirikiano wa Vyama vya Siasa vya Upinzani Tanzania

  Sisi viongozi wa vyama vya siasa vya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi), NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM (NCCR-Mageuzi) na TANZANIA LABOUR PARTY (TLP) tuliokaa Dar es Salaam leo hii tarehe 10 Mei 2007:

  Kwa kutambua kuwa wananchi wa Tanzania wanahitaji mageuzi ya dhati ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii;

  Kwa kuelewa kuwa mageuzi ya dhati hayawezi kupatikana bila kwanza vyama vya kisiasa vya upinzani kuunganisha nguvu zao na nguvu za umma ili kuundoa madarakani mfumo wa chama dola ambao umezuia demokrasia, umedidimiza haki na hali za kiuchumi na kijamii za wananchi wa Tanzania walio wengi na kuongeza ukandamizaji, rushwa na ufisadi wa watawala;

  Na kwa kuelewa kwamba mfumo wa kikatiba na wa kisheria uliopo kwa sasa hautoi uhuru wa wazi wa vyama vya siasa kuungana na kuendesha shughuli za kisiasa kama mseto wa vyama vya siasa; Hivyo basi tumeamua na kudhamiria yafuatayo:


  Kwamba lengo letu kuu na la pamoja na la jumla ni kuunganisha nguvu zetu katika kukabiliana na mfumo wa chama dola uliopo sasa ambao umezuia kukua kwa demokrasia, ukiukwaji wa haki za msingi za raia, kuongezeka kwa ukandamizaji , rushwa, vitendo vya ufisadi na kuzorota kwa uchumi.

  Kwamba vyama vyetu vitafanya kazi au kuendesha shughuli zake za kisiasa kwa pamoja na kushauriana katika masuala yote makuu ya kisiasa, ya kuichumi na ya kijamii katika Tanzania;

  Kwamba viongozi wakuu wa vyama vyetu watafanya mikutano ya hadhara ya pamoja na/au ya mmoja mmoja katika sehemu mbalimbali za nchi yetu na pamoja na shughuli nyingine, kwa nia ya kuelezea haja, umuhimu na ulazima wa kuunganisha nguvu zetu na za umma;

  Kwamba vyama vyetu vitashirikiana katika masuala yote ya kisiasa ikiwa ni pamoja na kuwa na msimamo wa pamoja bungeni na/au katika vyombo vingine vya uwakilishi wa umma;

  Kwamba vyama vyetu vitashirikiana na kuwa na msimamo wa pamoja katika jitihada za kuweka mfumo mpya wa kikatiba na kisheria ambao utaruhusu vyama vyetu kushirikiana na kuendesha shughuli za siasa kimseto.

  Kwamba viongozi wakuu wa vyama vyetu watatoa maazimio na matamko ya pamoja kuhusiana na masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa pale itakapohitajika;

  Kwamba tutafanya jitihada zote kuelimisha viongozi wa vyama vyetu wa ngazi mbalimbali, wanachama wetu, na wananchi kwa ujumla juu ya haja na ulazima wa vyama vyetu kushirikiana katika nyanja mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa hadi ngazi za kitaifa. Ili kulifanya jambo hili lifanikiwe na kujengewa misingi imara ya kukubalika na kutekelezwa kila Chama kitalifikisha suala hili katika vikao vyake vya kikatiba.

  Kwamba tunaomba wanachama wetu, wananchi wa Tanzania na Jumuia ya kimataifa watuunge mkono ili tutimize malengo tuliojiwekea leo kwa faida ya Watanzania wote.

  Kwamba Chama chochote kingine cha upinzani kinaweza kukubaliwa kujiunga na ushirikiano huu kwa mujibu wa kanuni zitakazoandaliwa.

  Kwamba utekelezaji wa makubaliano haya utasimamiwa na kanuni ambazo zitapitishwa na viongozi wakuu wa vyama

  Tamko hili limetolewa na kusainiwa hapa Dar es Salaam leo hii tarehe 10 Mei 2007:

  Freeman Aikaeli Mbowe - Mwenyekiti, CHADEMA
  Prof. Ibrahim Haruna Lipumba - Mwenyekiti, CUF
  James Francis Mbatia - Mwenyekiti, NCCR-MAGEUZI
  Augustino Lyatonga Mrema - Mwenyekiti, TLP

  Nakushuhudiwa na;

  Dr. Wilbrod P. Slaa - Katibu Mkuu, CHADEMA
  Seif Sharif Hamad - Katibu Mkuu, CUF
  Polisya Mwaiseje - Katibu Mkuu, NCCR-MAGEUZI
  John Komba - Katibu Mkuu, TLP
   
 2. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Waliwa timing,ila kama watakuwa wakweli wakaondoa tamaa zao lipo jibu siku moja, wajipe moyo huku tungojea mabadiriko ya katiba siku moja.
   
 3. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwamba lengo letu kuu na la pamoja na la jumla ni kuunganisha nguvu zetu katika kukabiliana na mfumo wa chama dola uliopo sasa ambao umezuia kukua kwa demokrasia, ukiukwaji wa haki za msingi za raia, kuongezeka kwa ukandamizaji , rushwa, vitendo vya ufisadi na kuzorota kwa uchumi.

  Unaliona hilo neno jekundu, lilitakiwa lisomeke VYAMA, basi tu ilipigwa chenga ya kiaina!!! na hiyo zetu ilitakiwa iwe vyetu
   
 4. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwita,
  Hamna cha timing uanyoisema wala nini, siku kadhaa zilizopita nilikuwa Kigoma, nilijionea vyama hivi vikiliana timing nyingine kabisaa vyenywewe kwa vyenyewe.
   
Loading...