Leo ni miaka 23 toka Museveni aingie madarakani-Wingu Jeusi EAC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo ni miaka 23 toka Museveni aingie madarakani-Wingu Jeusi EAC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Jan 26, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Rais Yowel Kaguta Museveni leo anatimiza miaka 23 madarakani baada ya kuipindua serikali ya kijeshi ya Major jenerali Tito Okello Mnamo January 26,1986. Museveni ameonyesha kila dalili ya kwamba hawezi kuachia madaraka ya kuitawala Uganda hivi karibuni kwani ameshaanza kupiga chapuo za kusimama katika uchaguzi ujao kama mgombea wa NRM.

  Hali hii ni sawa na wingi jeusi linaloifunika jumuia ya afrika mashariki. Bwana M7 moja ya mambo anayoyawazia ni yeye kuwa rais wa kwanza wa shirikisho la afrika mashariki. Binamu yake Kagame naye anapiga chepuo za kujisimika zaidi na kuifanya Rwanda iwe imaya yake binafsi.

  Kwa mtizamo huu wa hawa ndugu wawili ambao kwao utawala wa sheria ni ule unaoashiria kusimama kwa tawala zao. Je Tanzania tutayaweza ya jamaa zetu hawa. Kumbuka tuna amani japo napo siku hizi ishaanza kuingia 'kwikwi', tuna ardhi kubwa tu ( kumbuka nchi zote zilizobaki za jumuia ya A/mashariki zinamatatizo ya ardhi)?

  Mwisho leo M7 anashereheka kutimiza hiyo miaka 23, Je watanzania tuna nini cha kujifunza kutokana na yeye pamoja na siasa za afrika mashariki? je shirikisho ndio njia pekee ya kuelekea kwenye kaanani yenye maziwa na asali au ndo kujiweka reahani?

  Wakatabahu,

  Shadow.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Musevenimtu hatari sana, hasa pale watutsi wanapotaka kuitawala Afrika mashariki na kati. Kagame alipigana bega kwa bega wakati wa Uganda, akishirikiana na marehemu Rwigyema. Baada ya vita kuisha marehemu Rwigyema akashirikiana na Kagame kuichukua Rwanda, sema kwa sasa Kagame uhusiano wake kidogo na Museveni sio mzuri sababu alianza kutotii amri zake.

  Tukirudi kwa Museveni, anataka sana kuwa Rais wa kwanza wa Shirikisho la Afrika mashariki, wakati wa kura za maoni kujionesha yuko karibu na waTZ alitembelea Butiama na alikuwa aende na gari toka Butiama kupitia Kagera mpaka Uganda. Na wakati huohuo ndio chuo kimoja kikuu cha Uganda (nadhani Makerere) kilipendekeza majina ya watu wanaoweza kuwa Mkuu wa Chuo, na jina la Mkapa likiwemo. Huyu jamaa ni hatari sana kumpa kumpa uRais wa shirikisho. Lakini kwa nini tunakimbilia sana katika shirikisho?.
   
Loading...