LEO ni Miaka 15 ya Dhahabu ya damu’ ya Bulyanhulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LEO ni Miaka 15 ya Dhahabu ya damu’ ya Bulyanhulu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by lifeofmshaba, Aug 7, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  je haki imeshatengeka? na sheria za madini je?

  Dhahabu ya damu' ya Bulyanhulu
  haki itendeke kwa damu iliyomwagika  MIAKA 15 imepita, lakini sauti za wachimbaji wadogo wa dhahabu waliouawa kwa kufukiwa katika mgodi wa Bulyanhulu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, bado zinasikika katika kijiji cha Kakola, wilayani Kahama.
  Njile, Toloka, Jonathan, Ernest na Mororasa ni baadhi ya majina yanayotamkwa na wengi na kutajwa kuwa walifukiwa na magreda ya Kampuni ya Kahama Mining Corporation Ltd (KMCL) – wachimbaji dhahabu Bulyanhulu.


  Leo hii, wakazi wa Kakola, mkoani Shinyanya, wanaendelea kudai ufanyike uchunguzi huru juu ya tukio hilo ambalo linatajwa kuangamiza maisha ya watu wapatao 52.
  Miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo lililofanywa na mwekezaji katika mgodi wa dhahabu, ni Sweetbert Paul (48), kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  "Sikusimuliwa. Nilishuhudia kwa macho yangu, unyama ukifanywa na polisi," anaeleza Paul.
  Anaendelea, "Kuna vijana watatu waliokuwa kwenye duara moja wakifungua mashine yao ili kutekeleza agizo la kuhama eneo lile. Kwa bahati mbaya walikaa muda mrefu chini, hawakusikia fukuzafukuza juu; wakafukiwa na greda la kampuni."
  Paul anasema alipojaribu kuwaambia polisi kuwa katika shimo walilofukia mlikuwa na watu, "…walinitishia kwa bunduki nikakimbia. Katika shimo hilo walikuwemo Njile, Toloka na Mororasa."


  Huyu ni shahidi muhimu pindi ikiamuliwa kuwa ufanyike uchunguzi huru kuhusu mauaji yaliyofanywa na kampuni ya kigeni na kulindwa na serikali.
  Paul anasema anakumbuka pia kuona polisi wakiwavua nguo vijana 13, kuwaacha uchi na kuwaambia washikane mikono viunoni huku kila
  mmoja akiweka uume wake katika makalio ya mwingine.
  Anakumbuka kuona polisi wakichapa viboko kijana wa 13 (mwisho); na kadri aliyepigwa ndivyo alivyojisukuma mbele na kusukuma uume wake kwa aliyemtangulia, vivyo hivyo kila mmoja kwenye msululu hadi mtu wa pili.
  "Sijawahi kuona unyama kama ule maishani. Baadhi ya watu walikaidi; na mmoja wao, Mustafa Taslim alivunjwa kiuno kwa kipigo," alisisitiza.
  Hakika uchunguzi hautarejesha waliokufa, lakini utainua ukweli ambao wananchi wamesimamia tangu tarehe 7 Agosti 1996 na kuweka msingi wa uwazi kwa serikali zijazo.


  Uchunguzi utaweka wazi, ushiriki wa kampuni mama ya Sutton Resources ya Vancouver, Canada ambayo kupitia KMCL ilipewa leseni kumiliki mgodi huo, katika mauaji ya Watanzania.
  Kwa mujibu wa jarida la The Varsity and the Atkinson, Toleo la 15 Aprili 2002, Ofisa mtendaji mkuu wa Sutton Resources, James Sinclair alikuwa "rafiki wa rais wa Tanzania na mawaziri kadhaa waandamizi."


  Inaweza kuthibitishwa wakati wa uchunguzi, ni nani kati ya marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, alikuwa "rafiki" wa mwekezaji muuaji.


  Kuna madai kuwa polisi waliharibu ushahidi wa picha Kakola, huku serikali ikitoa tamko bungeni kukanusha taarifa za magreda ya Kahama Mining kufukia maduara huku wachimbaji wakiwa ndani.
  Taarifa ilisomwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Shija. Hivi sasa ni Katibu mkuu wa chama cha mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola
  Polisi waliwaziba midomo wananchi; serikali ikatoa taarifa ya "kujisafisha;" lakini kila wakazi wa Kakola wanapokumbuka tukio hilo, hujawa hasira na chuki dhidi ya mgodi na serikali yao.


  Melania Maesi (67) na mumewe John Mutemankamba, wanaendelea na msiba wa kudumu kufuatia watoto wao wawili – Ernest na Jonathan kuuawa kwa kufukiwa na magreda ya mwekezaji chini ya usimamizi wa polisi.
  Familia hiyo imelia, imelalamika, imeomba msaada wa kisheria bila mafanikio. Hata hivyo haijakata tamaa na inaomba ufanyike uchunguzi nje ya vitisho vya polisi.
  "Siku hiyo, 7 Agosti 1996 majira ya saa 10.00 hivi alasiri, alikuja rafiki yetu Mafuru Butondo. Alitupatia taarifa kwamba watoto wangu Jonathan na Ernest wamekufa," anaeleza Melania. Alisema wamefukiwa wakiwa hai na mabuldoza ya kampuni ya Kahama," anasimulia Melania.


  Melania na mumewe walikuwa wanamiliki maduara mawili ambayo yaliwawezesha kupata fedha na kujenga nyumba wilayani Muleba mkoani Kagera. Dhahama ya Bulyanhulu imewaacha patupu na nyumba waishio Kakola imekandikwa kwa udongo.
  Wiki moja mapema, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na polisi walikuwa wamekwenda Kakola na kuwaambia wananchi waondoke katika eneo la machimbo "zibaki zinasikika sauti za ndege tu" kwa ajili ya kampuni ya Kahama Mining.


  Mzee Henry Kisambale (67), aliyeishi Kakola kwa zaidi ya miaka 57, anasema hakuona watu wakifukiwa katika maduara yake, lakini walipata ushahidi wa kimazingira walipojitolea kufukua mashimo ili kuthibitisha.
  Kisambale anasema alikuwa na maduara 20 yaliyokuwa na watu 351 na kwamba hakuna hata mmoja aliyefukiwa katika maduara yake "isipokuwa kwa wengine."
  "Bali kuna ushahidi wa mazingira. Siku serikali iliposema kijiji kifukue ili kuthibitisha; walipofikia hatua fulani, walianza kutoka funza, mainzi yakajaa na kukawa na harufu kali. Hapo polisi wakasitisha ufukuaji na kuwafukuza watu wote," anasimulia Kisambale.
  Elias Lujiga (65), ni miongoni mwa wakulima 58 waliofungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Tabora wakitaka walipwe fidia baada ya mgodi wa Bulyanhulu kuchukua mashamba yao.
  Anasema anaamini watu walifukiwa wakiwa hai na anapenda ufanyike uchunguzi huru.


  Mwaka 2002, Mark Bomani, aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, alipendekeza pia ufanyike uchunguzi huru.
  Watu mashuhuri duniani, wanaharakati, wanasheria na mashirika yasiyo ya kiserikali, wanaunga mkono uchunguzi huru lakini serikali imekaa kimya.
  Wanasheria wa Chama cha Wanasheria wa Mazingira (LEAT), Tundu Lisu na Rugemeleza Nshalla ambao walijitosa kutetea haki za wachimbaji wadogo, wamewahi kufunguliwa kesi na kushitakiwa kwa "uchochezi."
  Hivi sasa mgodi ulioua unamilikuwa na African Barrick Gold (ABG) ambayo inaendeleza upanuzi wa eneo la mgodi na kufanya wakazi wa Kakola waishi kwa woga wa kutimuliwa kutoka walipo wakati wowote ule.


  ILIANDIKWA NA MWANA HALISI
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  R.I.P kuna siku haki itatendeka sisi huku duniani bado tunateshwa na haya
  madini ni mwaka huu tumeshuhudia NYAMONGO lakini cha kushangaza hakuna haki
  iliyotendeka mbaya zadi ni kitendo cha polisi kuchezea miili ya marehemu
  Bado tuna serikali dhalimu hakuna wanachojari ila matumbo yao na familia zao

  Njia ni mmoja na sisi tutafuta sio muda mrefu tunaomba MUNGU atuepushe na mateso mliyopata
   
 3. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nchi iliyolaaniwa kwa vitendo vya viongolzi wake imewafanya watu wake kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe. Sijui kama watu hawa wanawaza kuwa kuna kumwona Mungu!!
   
 4. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi kweli wabunge wetu wameshindwa kuishinikiza serikali kufanya uchunguzi huru kuhusu hili? Au kwa sababu JK ana hisa kwenye hili Barrick?
   
 5. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  siku hizi naamini BUNGE ni dhaifu kuliko JF kwa upande wa kusema UKWELI wabunge wengi
  michango yao bungeni ni kama wako blackmail au wamenunuliwa inatia UCHUNGU sana
  Tuna wabunge makini kutoka CHADEMA lakini hawana nguvu hatukuwapa nguvu(wabunge) za kutosha
  sasa tutajuta kwa miaka mitano

  ILA ILI LA MADINI HAKI ITENDEKE ILI NDUGU WAISHI KWA AMANI
   
 6. W

  Willegamba Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali iliyopo madarakani ndio ilitenda huu unyama uliovuka mipaka na unaokiuka hata amri za Mungu. Sio rahisi ijichimbie kaburi yenyewe, kwa kudra zake Mungu tukifanikiwa kuibadilisha serikali hii onevu na kiziwi ya manavu yote yatafanyiwa kazi na wahusika watawajibishwa vinginevyo tutasaga meno duniani na jehanam.
   
 7. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Machungu yamenijaa moyoni. hivi serikali gani duniani inaweza kufanya hivi, naomba kwa pamoja tuanze kuwaelimisha watz wenzetu ili 2015 tuiondoe hii serikali ya zzm inayo ua watu kama wanyama, na One day GOD WILL SAY YES, KWA Pamoja tutawaondoa hawa wauwaji halafu wahusika wote wachukuliwe hatua.
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Ipo siku ccm tutaisahau na damu ya wazalendo itapotea akilini mwa wazalendo hao!
   
 9. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Truth will NEVER be buried forever and you can always win the nature, but nature will never be defeated
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tafadhali nibandikie ule wimbo wa Remi Ongala juu ya Bulyanhulu hapa; tajiri na mali yake, masikini na baiskeli.

  Namkumbuka sana Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema na jitihada zake zote kutufahamisha kilichotokea kabla, wakati na baada ya shimo la dhahabu KUFUKIWA na Walazwahoi mle ndani!!!!!!!!!!!!

  Tufarijiane japo na hako ka wimbo plz kwa siku hii ya majonzi kwa wavuja jasho nchini.
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hongera sana kwa kutuletea historia. Hili ni jambo muhimu sana kulikumbuka. Ningependa watengeneze documentary, au hata kitabu kitakachowanukuu wahusika, including opinion za politicians waliokuwa madarakani wakati huo. Ukweli utabaki pale pale daima! Mungu awapumzishe mahali pema peponi.
   
 12. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna mtu alijua Pinochet au Noriega atashitakiwa kwa mauaji ya nchini mwao. Mubarak na Ben Ali walikuwa ni watu powerful sana na wana inteligency ya ajabu katika kukandamiza wananchi leo hii hawapo tena. Wazungu hawa waliomiliki Bulyanhulu sasa yaani Barrick wananyanyasa sana waafrika, ubaguzi ndio maana kila kukicha wanatangaza kazi magazetini. Mzungu analipwa $ 10000- 25,000 kwa mwezi mswahili analipwa laki 5 mpaka milioni 1 na nusu hii ni haki kweli. Lazima iwepo independent enquiry commission kuhusu vifo vya watu hawa.
   
 13. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mh! Nakumbuka wkt nimeanza kazi pale TL alitupelekesha, lakini Kahama Mining pia wana vizee kadhaa vilivyorekodiwa kusema hayo si kweli...
   
 14. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />

  Turnover kubwa mgodini ni inevitable! Maisha ya kule huwezi kaa zaidi ya miaka 3...

  Pia wkt mgodi unaanza expats walikuwa wengi ili wawatrain watanzania mining, ila mishahara pia kwa wabongo wenye nafasi zao si haba..inategemea na usenior wako..
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Utakuta huyu jamaa bado ni kada wa hicho chama....
   
 16. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  We unakula nchi tuu....
   
 17. K

  Karry JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  R.I.P na pole kwa wafiwa wote mungu awape nguvu
   
 18. K

  Karry JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  je watanzania tunapata faida gani kwa uwekezaji huu zaidi ya kuzidisha umaskini
   
 19. nzumbe

  nzumbe Member

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna faida bali ni tumezidishiwa umasikini!!.. Hii serikali ya CCM haisaidii lolote bali ni matatizo tuuuuu....
   
 20. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waafrika tuna angazwa kwa rasilimali zetu wenyewe. Viongozi wetu wa sasa wamekuwa ni wauza nchi zaidi ya Chief Mangungo, wanapewa vitu vidogovidogo kama vyandarua, mikopo ya vijisenti, kujengewa vyoo nk. Hii ni aibu kubwa kwa bara zima na maendeleo ya ukweli tutayasikia kwa wazungu tu labda tujipange upya kulikomboa bara letu toka kwa vibaraka hawa.
   
Loading...