LEO ni Miaka 15 ya Dhahabu ya damu’ ya Bulyanhulu (7 Agosti 1996 majira ya saa 10.00 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LEO ni Miaka 15 ya Dhahabu ya damu’ ya Bulyanhulu (7 Agosti 1996 majira ya saa 10.00

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lifeofmshaba, Aug 7, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [h=3]je haki imeshatengeka? na sheria za madini je?[/h]

  Dhahabu ya damu’ ya Bulyanhulu
  1.haki itendeke kwa damu iliyomwagika
  2. makampuni ya madini sasa iwe mwisho wa kupotea roho za watanzania bali wapate utajili


  MIAKA 15 imepita, lakini sauti za wachimbaji wadogo wa dhahabu waliouawa kwa kufukiwa katika mgodi wa Bulyanhulu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, bado zinasikika katika kijiji cha Kakola, wilayani Kahama.
  Njile, Toloka, Jonathan, Ernest na Mororasa ni baadhi ya majina yanayotamkwa na wengi na kutajwa kuwa walifukiwa na magreda ya Kampuni ya Kahama Mining Corporation Ltd (KMCL) – wachimbaji dhahabu Bulyanhulu.


  Leo hii, wakazi wa Kakola, mkoani Shinyanya, wanaendelea kudai ufanyike uchunguzi huru juu ya tukio hilo ambalo linatajwa kuangamiza maisha ya watu wapatao 52.
  Miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo lililofanywa na mwekezaji katika mgodi wa dhahabu, ni Sweetbert Paul (48), kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  “Sikusimuliwa. Nilishuhudia kwa macho yangu, unyama ukifanywa na polisi,” anaeleza Paul.
  Anaendelea, “Kuna vijana watatu waliokuwa kwenye duara moja wakifungua mashine yao ili kutekeleza agizo la kuhama eneo lile. Kwa bahati mbaya walikaa muda mrefu chini, hawakusikia fukuzafukuza juu; wakafukiwa na greda la kampuni.”
  Paul anasema alipojaribu kuwaambia polisi kuwa katika shimo walilofukia mlikuwa na watu, “…walinitishia kwa bunduki nikakimbia. Katika shimo hilo walikuwemo Njile, Toloka na Mororasa.”


  Huyu ni shahidi muhimu pindi ikiamuliwa kuwa ufanyike uchunguzi huru kuhusu mauaji yaliyofanywa na kampuni ya kigeni na kulindwa na serikali.
  Paul anasema anakumbuka pia kuona polisi wakiwavua nguo vijana 13, kuwaacha uchi na kuwaambia washikane mikono viunoni huku kila
  mmoja akiweka uume wake katika makalio ya mwingine.
  Anakumbuka kuona polisi wakichapa viboko kijana wa 13 (mwisho); na kadri aliyepigwa ndivyo alivyojisukuma mbele na kusukuma uume wake kwa aliyemtangulia, vivyo hivyo kila mmoja kwenye msululu hadi mtu wa pili.
  “Sijawahi kuona unyama kama ule maishani. Baadhi ya watu walikaidi; na mmoja wao, Mustafa Taslim alivunjwa kiuno kwa kipigo,” alisisitiza.
  Hakika uchunguzi hautarejesha waliokufa, lakini utainua ukweli ambao wananchi wamesimamia tangu tarehe 7 Agosti 1996 na kuweka msingi wa uwazi kwa serikali zijazo.


  Uchunguzi utaweka wazi, ushiriki wa kampuni mama ya Sutton Resources ya Vancouver, Canada ambayo kupitia KMCL ilipewa leseni kumiliki mgodi huo, katika mauaji ya Watanzania.
  Kwa mujibu wa jarida la The Varsity and the Atkinson, Toleo la 15 Aprili 2002, Ofisa mtendaji mkuu wa Sutton Resources, James Sinclair alikuwa “rafiki wa rais wa Tanzania na mawaziri kadhaa waandamizi.”


  Inaweza kuthibitishwa wakati wa uchunguzi, ni nani kati ya marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, alikuwa “rafiki” wa mwekezaji muuaji.


  Kuna madai kuwa polisi waliharibu ushahidi wa picha Kakola, huku serikali ikitoa tamko bungeni kukanusha taarifa za magreda ya Kahama Mining kufukia maduara huku wachimbaji wakiwa ndani.
  Taarifa ilisomwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Shija. Hivi sasa ni Katibu mkuu wa chama cha mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola
  Polisi waliwaziba midomo wananchi; serikali ikatoa taarifa ya “kujisafisha;” lakini kila wakazi wa Kakola wanapokumbuka tukio hilo, hujawa hasira na chuki dhidi ya mgodi na serikali yao.


  Melania Maesi (67) na mumewe John Mutemankamba, wanaendelea na msiba wa kudumu kufuatia watoto wao wawili – Ernest na Jonathan kuuawa kwa kufukiwa na magreda ya mwekezaji chini ya usimamizi wa polisi.
  Familia hiyo imelia, imelalamika, imeomba msaada wa kisheria bila mafanikio. Hata hivyo haijakata tamaa na inaomba ufanyike uchunguzi nje ya vitisho vya polisi.
  “Siku hiyo, 7 Agosti 1996 majira ya saa 10.00 hivi alasiri, alikuja rafiki yetu Mafuru Butondo. Alitupatia taarifa kwamba watoto wangu Jonathan na Ernest wamekufa,” anaeleza Melania. Alisema wamefukiwa wakiwa hai na mabuldoza ya kampuni ya Kahama,” anasimulia Melania.


  Melania na mumewe walikuwa wanamiliki maduara mawili ambayo yaliwawezesha kupata fedha na kujenga nyumba wilayani Muleba mkoani Kagera. Dhahama ya Bulyanhulu imewaacha patupu na nyumba waishio Kakola imekandikwa kwa udongo.
  Wiki moja mapema, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na polisi walikuwa wamekwenda Kakola na kuwaambia wananchi waondoke katika eneo la machimbo “zibaki zinasikika sauti za ndege tu” kwa ajili ya kampuni ya Kahama Mining.


  Mzee Henry Kisambale (67), aliyeishi Kakola kwa zaidi ya miaka 57, anasema hakuona watu wakifukiwa katika maduara yake, lakini walipata ushahidi wa kimazingira walipojitolea kufukua mashimo ili kuthibitisha.
  Kisambale anasema alikuwa na maduara 20 yaliyokuwa na watu 351 na kwamba hakuna hata mmoja aliyefukiwa katika maduara yake “isipokuwa kwa wengine.”
  “Bali kuna ushahidi wa mazingira. Siku serikali iliposema kijiji kifukue ili kuthibitisha; walipofikia hatua fulani, walianza kutoka funza, mainzi yakajaa na kukawa na harufu kali. Hapo polisi wakasitisha ufukuaji na kuwafukuza watu wote,” anasimulia Kisambale.
  Elias Lujiga (65), ni miongoni mwa wakulima 58 waliofungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Tabora wakitaka walipwe fidia baada ya mgodi wa Bulyanhulu kuchukua mashamba yao.
  Anasema anaamini watu walifukiwa wakiwa hai na anapenda ufanyike uchunguzi huru.


  Mwaka 2002, Mark Bomani, aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, alipendekeza pia ufanyike uchunguzi huru.
  Watu mashuhuri duniani, wanaharakati, wanasheria na mashirika yasiyo ya kiserikali, wanaunga mkono uchunguzi huru lakini serikali imekaa kimya.
  Wanasheria wa Chama cha Wanasheria wa Mazingira (LEAT), Tundu Lisu na Rugemeleza Nshalla ambao walijitosa kutetea haki za wachimbaji wadogo, wamewahi kufunguliwa kesi na kushitakiwa kwa “uchochezi.”
  Hivi sasa mgodi ulioua unamilikuwa na African Barrick Gold (ABG) ambayo inaendeleza upanuzi wa eneo la mgodi na kufanya wakazi wa Kakola waishi kwa woga wa kutimuliwa kutoka walipo wakati wowote ule.


  ILIANDIKWA NA MWANA HALISI
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu umetukumbusha mbali, R.I.P wote waliofukiwa... MUNGU IBARIKI TZ
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bado kama haitoshi wanatimuliwa na kukamatishwa Mbwa hata kwa kuokota yale mabaki ya mawe ambayo wawekezaji washayatelekeza baada ya kupora rasilimali zetu katika mtindo ule ule wa kichwa cha mwendawazimu
   
 4. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  "Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele" foolish ccm n his supporters.
   
Loading...