Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

Wanasema leo ni kumbukumbu ya Kifo cha Nyerere lakini viongozi wote wakubwa wameenda kutembelea na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Magufuli. Kwahiyo siku ya kumbulumbu ya kifo cha Magufuli watakwenda Butiama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Nyerere? Au walitaka kutuonesha kuwa wamelijengea nyumba kaburi la Magufuli? Sijaelewa!
View attachment 1973955View attachment 1973956View attachment 1973957
Ni kutokuelewa tu. Serikali imekuwa na utaratibu wa kufanya tarehe 14 Oktoba ya kila mwaka kuwa kilele cha wiki ya vijana, kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa. Vilele hivi hufanyika katika mikoa mbalimbali kwa kupokezena haijaanza mwaka huu.
 
Ni kumbukumbu ya kifo cha Hayati Mwl Nyerere na kilele cha mbio za mwenge shughuli iliyofanyika chato. Isinge kuwa busara Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi afike chato kwa shughuli hiyo ya kitaifa ya kilele cha mbio za mwenge na asiende kwenye kaburi la Hayati JPM na kumuenzi. Hapa serikali ya JMT chini ya Mh Rais SSH imeua ndege wawili kwa jiwe moja.

Bavicha nao wameazimisha kumbukumbu ya Hayati Nyerere kwa namna yao. Ndio demokrasia hiyo ingawa cdm wakati mwengine kwa nongwa tu hutaka kuonesha kila jambo la serikali ni baya.

# JMT kazi iendelee.
 
Wanasema leo ni kumbukumbu ya Kifo cha Nyerere lakini viongozi wote wakubwa wameenda kutembelea na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Magufuli. Kwahiyo siku ya kumbulumbu ya kifo cha Magufuli watakwenda Butiama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Nyerere? Au walitaka kutuonesha kuwa wamelijengea nyumba kaburi la Magufuli? Sijaelewa!
View attachment 1973955View attachment 1973956View attachment 1973957
kwani kujenga nyumba ndio nini.


Kaburi lapeke yako linakosa dua zakilamara.
Ukizikwa kwenye makaburi mengine pamoja na watu unapata dua kila watu wanapokuja kuombea watu wawo.
Karume katengwa Magufuli katengwa Sijui nyerere na mkapa kama pia wame tengwa.

Alikozikwa Jumbe watu wengine wanazikwa
Alipo zikwa Adulwakil, Watu wengine wana zikwa
Alipo zikwa Maalim Seif ni karibu na msikiti na watu wengine wana zikwa
 
Huna ushahidi wowote ule bali kuropoka Jamii Forum, shukuru kuna watu wameliwezesha hilo la wewe kupayuka.
Ushahidi? Basi Mungu ana ushahidi! Kamfuate huko kaburini umbusu, na Inshallah leo utamfuata muuaji mwenzako mnywe mikojo yenu wauaji
 
Ni moja ya maajabu ya viumbe waitwao binadamu hasa wale wanaoishi kiujanjaujanja yaani WANASIASA. Ni ajabu lakini ni kweli. Inachekesha haswa ukizingatia inapangwa na inafanywa na watu walioona mlango wa shule. Binafsi nimeshindwa kuelewa uhusiano. Pengine tu ni kuwafanya kina flani bado waamini kwamba "hakuna kama marehemu baba" huku wanae wakipukutishwa kila uchao. SIASA na wanasiasa ni hatari mnoooo.
 
Ukosefu wa mbinu za kisiasa na utovu wa nidhamu. Hivi kweli DrJKNyerere anastahihi kufananushwa na Magufuli kwa kiwango tunachotaka kuaminishwa? Kweli? Sio hata kwa 30%
... Jpm aundiwe siku yake ya mapumziko; siku ya Mw. unamuenzi mwingine huku mwenye siku yake akiachwa tafsri yake nini? Mashada yalitakiwa yakawekwe Butiama kama yanavyowekwa Kisiwandui na sio Chato! Baba wa Taifa amekosewa heshima sana leo
 
Ni upumbavu wa Hali ya Juu, yaani leo hii Magufuli ndio achukue nafasi ya Mwalimu?

Hivi mama hawezi kufikiri kwamba timu ya Mwendazake inamuendesha inavyotaka?

Yaani kapigwa na kuaminishwa propaganda kwamba wasukuma ndio wanaamua Rais? Miaka yote kabla ya Uhuru walikuwa wanaamua Rais?

Magu alipata 58% za kubumba dhidi ya Lowassa kwa nini wasukuma hawakumpa aailimia zote? Huu ni upuuzi na dhihaka kwa Marehemu mwalimu Nyerere.
Mnawaongelea wafu lakini, kumbukeni hilo sana tena sana, inavyoonyesha kunahaja kubwa sana ya kurudi kwenye ibada zetu za mizimu…
 
Mwenyewe sikuelwa kuona mashada yanawekwa Chato badala ya Butiama. Pengine Shaka atalitolea maelezo kama sio Msigwa.
 
Umeshangazwa na Nini!?,mwal.anasheshma zake zote kwa kila mtz na tumekuwa tukimuenz kila kukicha Hadi leo,jpm alikuwa mbadala wa mwal. hivyo ni sawa pia katka kumbukiz za mwal.kumkumbuka pia jpm.hii ni meseji kwa mwal. ya kuwa baada ya wewe mwal. alitokea kijana wako ambae alitembea kwenye maono yako ya miaka mingi,bahati mbaya hatunae ,Ila ametufikisha mahali fulani pa kuanzia na kuendeleza.
Hebu acha kulinganisha mtu wa maana kuwahi kutokea nchi hii, na viumbe wa ajabu ajabu hao!!MUNGU FUNDI
 
Ndugu zangu kwa nini tunapenda fikra hasi ktk kila jambo? Kumbukizi ya Mwalimu imefanyika Chato, ambako kuna kaburi la Dk. Magufuli.

Kosa nini hapo kwa Rais na viongozi wengine kupita ktk kaburi na kuweka shada la maua na kumuombea dua aliyekuwa kiongozi wetu?
Utetezi duni sana !
 
Anayelia sana msibani 90% huwa ni muhusika mkuu,....(.1) mtoto wa marehemu ntamsomesha mimi (2) chakula na mazishi ntasimamia mimi (3) hujitoa sana kuwa hadaa watu kumbe kikulacho by mr nice
 
Utetezi duni sana !
Wami Dakawa ni site ya mpendwa Sokoine, ikitokea kumbukizi ya Mwalimu, Wiki ya Vijana na kuzimwa Mwenge wa Uhuru ukifanyika Moro, je, viongozi wakienda pale kabla ya kuelekea ktk tukio la kumbukizi ya Mwalimu, ni kosa?
 
Wanasema leo ni kumbukumbu ya Kifo cha Nyerere lakini viongozi wote wakubwa wameenda kutembelea na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Magufuli. Kwahiyo siku ya kumbulumbu ya kifo cha Magufuli watakwenda Butiama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Nyerere? Au walitaka kutuonesha kuwa wamelijengea nyumba kaburi la Magufuli? Sijaelewa!
View attachment 1973955View attachment 1973956View attachment 1973957
Aliyepanga ratiba ya SSH Nyerere day alichemsha sana!
Hastahili kuwepo ikulu.
 
Back
Top Bottom