Leo ni kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Hananasif, aliyeuwawa kinyama 11/02/218 kwa sababu za kisiasa (Daniel John)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
KUMBUKUMBU YA MWAKA 1 YA KIFO CHA KATIBU CHADEMA KATA YA HANANASIF DANIEL JOHN (KAMWENE)


Leo 11/02/2019 ni kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Hananasif, aliyeuwawa kinyama 11/02/218 kwa sababu za kisiasa.


Ikumbukwe Katibu Daniel (Kamwene) alitekwa na kuawawa kweny uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni wiki moja kabla ya kupigwa kura, uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kujihudhuru kwa kununuliwa na Ccm.


Kwa mujibu wa rafiki yake Bw. Reginard waliotekwa pamoja ila yeye kunusirika baada ya kuokolewa na wasamalia wema akiwa hajitambui.
Ni kwamba usiku wa saa 2 siku hiyo watu wasiojulikana walienda nyumbani kwa marehemu lakin hawakumkuta, baada ya kumkosa walimfatilie na kumkuta akiwa anacheza Pool(pulu) sehemu Fulani Kilimanjaro Bar mkwajuni.


Watu hao wasiojulikana wakaona ni vigumu kumtoa hapo kwenye Pool alipokuwa na huyo rafiki yake Reginard hivyo wakaenda Bar ya jirani iliyokuwa inaitwa Tweeter, kwa kutumia mtu anayemjua Marehemu Daniel akampigia simu kumwabia aje hapo Tweeter kuna kitu anataka kumpa, lengo lao atoke hapo ili iwe rahisi kufanikisha adhima yao na ikumbukwe pia marehemu alikuwa anajishughulisha na upigaji picha kwa hiyo haikumshitua sana, alipopigiwa simu alimwambia rafiki yake huyo kuwa waongozane, ndipo walipoanza safari ya kwenda huko alikopigiwa simu Tweeter.


Wakiwa njiani kuelekea walipopigiwa simu ndipo nyuma yao wakatokea watu wasiojulikana wakiwa kweny gari ya Landlover nyeupe wakamkamata Daniel wakamtupia ndani ya gari, wakati Reginard anashangaa hajui kinachoendelea, na yeye akatupiwa ndani ya gari na moja kwa moja wakapelekwa fukwe za Coco beach.


Huko Coco beach ndipo walipewa mateso ya hali ya juu huku wakiambiwa kuwa wao ndo wataalam wa kutafuta wapiga kura za mgombea wa Chadema, pia wakaambiwa watoe shahada za kupigia kura na kadi za uanachama za Chadema. Bw. Reginard aliwaambia kuwa sio mwanachama wa chama chochote ila anayo shahada ya kupigia kura lakin kaiacha nyumbani.


Ndipo Katibu Daniel alipigwa na kitu kizito kichwani, na akanyongwa kwa kupitiwa waya mdomoni baadaye wauaji wakaona haitoshi wakamtupa baharini.
Bw. Reginard yy alipigwa akazimia wakajua wamemuua wakaenda kumtupa maeneo ya masaki alipopata wasamalia wema wakamuokota na kumpeleka nyumbani kwao then hospitali.


Baada ya siku mbili kumtafuta bila mafanikio tulienda polisi Osterbay ndipo tulipoambiwa twende muhimbili ambapo tuliukuta mwili wa Marehemu Daniel John (Kamwene) ukiwa umepigwa vibaya mno na majereha kila sehemu na ilitupa ugumu sana kumtambua kuwa ndio Daniel John mpka alipokuja mke wake akathibitisha kuwa ndio mwnyewe.
Marehemu Daniel John alizikwa kijijini kwao Mafinga mkoa wa Iringa siku ya jumatano 20/02/2018.

Mimi Mwenyekiti kwa niaba ya viongozi, wapenzi, wadau na wanachama wa Chadema tutakumbuka daima kwa ushupavu, ujasiri na umakini wa kupigania haki, Demokrasia na kueneza Chama ndani ya kata ya Hananasif na nje ya kata, ulikuwa mtu muhimu sana ambapo pengo lako haliyazibwa na halitazibwa mtu yoyote.



Tunaamini kifo chako kilitokana na misimamo yako na hukutaka kuwapigia magoti hao waliotaka ufanye hivyo, umekufa kama wapigania haki wengine waliokufa vifo vya aina hiyo mfano Martin Luther king Jr, Patrice Lumumba, Alphonce Mawazo, Msafiri Mbwambo na wengine wengi waliokufa kwa kupigania haki na kusimamia kile walichokuwa wana kiamini.


Wapigania haki na demokrasia nchini wanakumbuka wiki mbili kabla ya kupigwa kura uchaguzi mdogo wa Kinondoni, Taifa liliingia kwenye majonzi ya kumpoteza Marehemu Tambwe Hiza, Daniel John na mwanafuzi wa chuo cha usafirishaji cha NIT Dada yetu kipenzi Akwelina Akwilina aliyrpigwa risasi na askali pale Mkwajuni Kinondoni na kesi yake kubambikiwa viongozi wa kitaifa wa Chadema ambapo mpaka nnavyoandika hapa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mh. Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Ester matiko wanasota jela kwa sababu ya kesi hiyo ya kubambikiwa



Sisi wanaHananasif tuliobaki tunaamin damu yako haikumwagika bure kupitia damu yako hiyo ndo italeta ukombozi wa pili wa taifa hili.
Tutakuenzi kwa kuendeleza kile ulichokuwa unakifanya na kukipigania enzi za uhai wako.


Mungu alitoa na Bwana ametwaa jina lako lihimidiwe

Innah illah wahinnah illah rajoun
 
Back
Top Bottom