Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,912
- 30,253
LEO NDIYO SIKU ALIYOULIWA MALCOLM X
MALCOLM X alikuwa hero wangu toka udogoni na nimekisoma kitabu cha maisha yake alichoandika Alex Hailey nikiwa na miaka labda 15/16.
Nilipofika New York nimekuta ndiyo wiki kitabu chake alichoandika Manning Marable, ''Malcolm X Life of Reinvention,'' ndiyo kimetoka na kwa bahati mbaya mwandishi alikufa wakati anakaribia kufanya uzinduzi wa kitabu hiki.
Nilikinunua kitabu hiki katika duka maarufu la vitabu Marekani, Barnes and Nobles sehemu za Manhattan.
Halikadhalika nikamuomba mwenyeji wangu anipeleke Harlem 125 Street mitaa aliyokuwa akivinjari Malcolm X wakati wake katika miaka ya 1950/60.
Nililiona lile jumba Audobon Ballroom ambamo Malcolm X alipigwa risasi.