Leo ndiyo leo: Messi, Ronaldo vitani kupambania mataifa yao

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,515
Ni siku muhimu katika maisha yao ya kisoka. Siku ya kuzipambania timu zao za taifa ziweze kufuzu Kombe la Dunia la mwakani huko Urusi. Ni siku za wao kuudhihirishia ulimwengu wa soka kuwa wanaweza kuwa tegemeo katika klabu zao na timu zao za taifa.

Nchini Ecuador, Lionel Messi atawaongoza Argentina katika pambano la 'must win' kati yao na wenyeji Ecuador. Messi ataiongoza Argentina kusaka ushindi wa kufa au kupona ili waweze kufuzu fainali za kombe la dunia. Ushindi dhidi ya Ecuador utawafikisha Argentina kwenye alama 28 na kuweza kuwapiku wengine.

Huko Amerika ya Kusini, washindi wanne wa mwanzo hufuzu moja kwa moja. Wa tano hucheza na mshindi wa Oceania ambaye ni New Zealand ili mmojawapo afuzu. Kwasasa, Argentina inakamata nafasi ya sita. Tayari vinara Brazil wameshafuzu na leo watashuka uwanjani kupambana na Chile inayosaka kufuzu. Macho na masikio ya kocha Jorge Sampaoli na Waargentina wote ni kwa Messi.

Nchini Ureno, Christiano Ronaldo ataiongoza Ureno, mabingwa wa Ulaya, katika mechi ya kufa au kupona dhidi ya Uswisi. Hadi sasa, Uswisi inaongoza kundi la Ureno ikiwa na alama 27 na Ureno iko nafasi ya pili ikiwa na alama 24. Kwakuwa ina faida ya magoli ya kufunga, Ureno inahitaji ushindi wowote ili ifuzu. Uswisi inahitaji ushindi au sare ili ifuzu.

Hapa Ronaldo, pale Messi. Wote ni Manahodha na wachezaji bora wa soka kwasasa duniani. Wote wapo hatarini kufuzu kombe la dunia. Wote wanacheza mechi za leo wakiwa wanategemewa kuonyesha umahiri na ubora wao. Ureno watateremka dimbani saa 3:45 usiku huku Argentina wakicheza saa 8:30 usiku.
 
Mkuu Petro hali kama hii kisheria tunaweza kuiitaje? Kwako wakili msomi
 
Hahaaaaa kuna wababe German machine ,Brazil, Nigeria, na Misri raha ilioje,kama Waholanzi nao mguu nje mguu ndani hao wengine ndo watuume
 
Zitolewe tu...wachezaji wanaotembelea nyota za watu...watolewe na hakuna maajabu yoyote yatakayofanywa na hao .....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom