Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Tanzania imethibitisha kisa kimoja cha virusi vya corona. Mgonjwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda Air.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy Mwalimu, Mwanamke huyo alitoka Ubelgiji na alikuwa anaishi kwenye nyumba ambapo kuna mwanaume alipata virusi vya corona, baadae aliamua kurudi nchini na alipopimwa uwanja wa KIA alionekana mzima hana maambukizi kisha akaamua kujitenga na kujiweka karantini yeye mwenyewe na kukaa hotelini.

Baadae mwanamke huyo alianza kujisikia vibaya na kuamua kwenda hospitali ambapo alipopimwa akathibitika kuwa na virusi vya Corona.



F407E9A2-7B8C-4D66-BFFA-0D87533532EE.jpeg

TAARIFA KWA UMMA

KUWEPO KWA MGONJWA WA CORONA NCHINI TANZANIA


Ndugu Wananchi, Mnamo tarehe 15 Machi 2020, tulipokea msafiri mtanzania mwanamke mwenye umri miaka 46, ambaye aliwasili na ndege ya Rwandair, akitokea nchini Ubelgiji. Msafiri huyu aliondoka tarehe 3 Machi 2020, ambapo kati ya tarehe 5-13 Machi alitembelea nchi za Sweden na Denmark na kurudi tena Ubelgiji na kurejea nchini tarehe 15 Machi saa 10 jioni. Msafiri huyu alipita uwanja wa KIA akafanyiwa ukaguzi na kuonekana kutokuwa na homa.

Baadae alianza kujisikia vibaya akiwa hotelini na kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mt. Meru ambapo sampuli ilichukuliwa na kupelekwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii iliyopo Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi. Vipimo vya maabara vimethibitisha kuwa mtu huyu ana maambukizi ya ugonjwa wa Corona (COVID-19). Mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu. Ninapenda kutumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae nchini. Aidha Serikali inashirikiana na Shirika Ia Afya Duniani (WHO) na wadau katika kuendelea kutekeleza mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu.

Aidha, ninapenda kuendelea kuwataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama tunavyowapatia taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbali mbali. Aidha, kwa kuzingatia Kanuni ya 46 ya Sheria ya Afya ya Jamii, 2012 (Reg. 46 of the Public Health Regulation (Sanitisation and Hygiene Practices), 2012); ninaelekeza mambo yafuatayo:-

I. Watanzania wasiokuwa na safari za lazima, wanashauriwa kwa sasa kusitisha safari zao kwenye nchi zenye maambukizi

2. Nazitaka Taasisi zote zikiwemo Shule, Hoteli, Maduka ya Biashara, Nyumba za Kulala Wageni (Lodges/Guest Houses), Makanisa, Misikiti, Ofisi za Umma na za Binafsi, Vituo vya kutolea Huduma za Afya, taasisi za fedha, vyombo vya Usafiri, pamoja na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, viwanja vya mpira, na vituo vya abiria kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji tiririka na sabuni au maji yenye Klorini kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa mikono. Aidha kwa kadri itakavyowezekana, maeneo hayo yawekewe vifaa maalum vya kuwekea vitakasa mikono (Sanitizer Dispensers)

3. Kuweka maji yenye dawa ya Klorini au vitakasa mikono (hand sanitizers) katika mageti ya kuingilia hifadhini au mahotelini kwa ajili ya kusafisha mikono ya watalii na waongoza watalii wote.

4. Kuweka maji yenye dawa ya Klorini katika Vituo vya Mabasi ya abiria na Mwendokasi kwa ajili ya kusafisha mikono ya wasafiri.

5. Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana, kugusa pua, mdomo pamoja na macho kadri itakavyowezekana.

6. Hospitali zetu zihakikishe kuwa ndugu/jamaa wanaokwenda kuona wagonjwa waliolazwa idadi yao isizidi wawili kwa kila mmgonjwa

7. Kutoa taarifa kwenye Ofisi za Afya au Vituo vya Kutolea Huduma za Afya endapo watamwona mtu mwenye dalili za ugonjwa wa COVID- 19

Imetolewa na: Ummy Mwalimu,Mb.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Dar es Salaam.

16/3/2020

1584362523020.png
1584362535692.png





PIA SOMA
Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi |Usambaaji, Dalili na Kinga
 
Hatari.

Wakati wengine wanazuia watu kuingia nchini kwao nchi kubwa kama Marekani sisi tukajidai eti tuna vipimo uwanja wa ndege, marekeni wao hawana vipimo uwanja wa ndege? Marekani alizuia watu kutoka ulaya kuingia kwake sisi tukajifanya tuko vizuri kuliko Marekani.

Ccm hawana malengo mazuri na afya za watanzania. Sasa subiri tuipate fresh.

Wenzetu kila anaeingia toka nje ya nchi huwekwa karantini siku 14 hadi hali iwe sawa, sisi watu wanaibuka wakipimwa airport hakuna dalili wanaondoka kwenda makwao. Ni cases ngapi zimetokea kama za jana? Maana bado watu wako kwenye window period. Ulaya ni risk area watu wanatoka huko tunawaacha tu bila kuwaweka kwenye karantini.

Tulichokua tunakitafta tumekipata
 
Back
Top Bottom