Leo ndio nimeambiwa ''nakupenda mme wangu" nilipotinga nyumbani na Bodaboda

Mr mgeni

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
1,222
803
Habari zenu wana JF,

Najisikia faraja ila kwa upande mwingine ni simanzi, baada ya mikimiki na kujibana kibajeti nimefanikiwa kununua Bodaboda mpya leo hii. Nilipofika nayo tu nyumbani nikamwambia mke wangu, chombo chetu hiki sasa sipigi dei waka na pikipiki za watu aiseeee! Alifurahi sana na kunikumbutaia nikasikia "Nakupenda sana mme wangu" sikuwahi kusikia akiniambia hilo neno hata siku moja nikawa na walakini!Mmmhh miaka 3 yote ya ndoa leo ndo ananiambia ananipenda, kweli mapenzi pesa.

Nanyie msiwe wachoyo bana nipeni pongezi za dhati.

Siku njema nawapenda wote wana JF.
 
Naona uliniwahi kumchukua huyo mke....mwanamke anyechochea kazi za kimaendeleo kama hizo ni dili...lakini ukiona ambaye anapata pesa bado anakwambia anakupenda baada ya kumpa pesa ya saloon, huyo ni UKOMA....Hongera mkuu kwa kupata bike mpya.
 
Habari zenu wana Jf,
Najiskia faraja ila kwa upande mwingine ni simanzi,baada ya mikimiki na kujibana kibajeti nimefanikiwa kununua Bodaboda mpya leo hii.nilipofika nayo tu nyumbani nikamwambia mke wangu,chombo chetu hiki sasa sipigi dei waka na piki2 za watu aiseeee!!!!!alifurahi sana na kunikumbutaia nikasikia "Nakupenda sana Mme wangu"sikuwahi kusikia akiniambia hilo neno hata siku moja nikawa na walakini,,,!!!mmmhh miaka 3 yote ya ndoa leo ndo ananiambia ananipenda??Kweli mapenzi pesa.Nanyie msiwe wachoyo bana nipeni pongezi za dhati.
Siku njema Nawapenda wote wana JF.
Hongera sana mkuu, inaonekana alikuwa anakuhesabia siku tu, zilibaki chache angekula kona
 
Back
Top Bottom