MANYASANI
Member
- Jun 15, 2013
- 46
- 13
Nina maswali kadhaa
1) Ningependa nipewe majibu na waziri husika hivi kama serikali ina mpango gani wa kuchunguza haya makampuni ya recruitmen ili ijiridhishe kama watanzania wanatendewa haki ama ione kuna umuhimu wakuendelea kuyaruhusu kuendelea na biashara hii?
Serikali ijiulize hivi binadamu ni sawa na nyumba kuwa ni lazima awepo dalali wa kumtafutia kazi.
Je, suala la uwazi likoje? Mfano kuna kampuni yaani ikikupatia ajira wanachukua nusu ya mshahara wako kila mwezi.
Kama haya mambo yapo ulaya yanafanyika kama ilivyo hapa Tanzania,kwamba tunageuzana punda mtu kakaa kwenye kiyoyozi anachukua nusu ya mshahara wangu.
2) Serikali kupitia waziri husika hivi kweli uendeshwaji wa interview katika ajira za serikali upo uhuru na wa haki!?Ebu tujiulize iweje wengine wanamaliza tu mtihani wa chuo wiki inayofuata tayari kashasaini mkataba na taasisi ya umma.
Pia iseme kabisa kweli kuna fairness katika masuala ya interview ikiwa kabisa kuna baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanatoa majibu ya interview kwa ndugu zao haswa written. Mfano mzuri ni interview moja iliyowahi kufanyika IFM.
Mheshimiwa waziri husika hivi kweli hawa ambao wanaandaa written interview za serikalini huwa wanataka uelewa ama kukomoana maana yanaulizwa maswali ya ajabu hata hayafanani na career.
3) Je, Serikali ina mpango kwa waendesha interview wa serikali ambao katika kuendesha interview ya oral huuliza maswali ya kukomoa na pia hata hayahusiani kabisa na career au hayapo katika ethics za kufanya interview,ukiuliza unaambiwa wanapima confidence kumbe lengo ni fitina za kukuzubaisha wapate uwezo wakukuangusha.
4) Mheshimiwa rais, najua sina hadhi wala hata weledi wa kukuuliza ila nisamehe kwa utovu wa nidhamu huu. Je, ni kweli rais wangu vijana hawataki kazi?
Ni kweli mfumo wa elimu ya IFM, TIA, TPSC, DSM, UDOM,SAUTI, ST JOSEPH, DUCE na kadhalika unamuandaa kijana kujiari?
Mheshimiwa rais wangu, unajua vijana wengi ambavyo wanatamani na wenyewe wapate shughuli tu yakufanya hawapati huko kwa watoa ajira wanaambulia kudhalilishwa?
Mheshimiwa Rais, je unajua kuwa hata ziwa Victoria ambalo vijana wasio na ajira wanalitegemea kuna matajiri wamejimilikisha sehemu zenye samaki wengii? Na ukikutwa mnyonge huenda shaba ikakuhusu!
Mheshimiwa Rais, unajua kuwa vijana wako tayari kufanya kilimo cha kisasa japo hawana mtaji ila hata ardhi hawana kabisa? Amini Rais wangu kuwa nchi hii inakuangalia vijana ukiwatengenezea mazingira wajiajiri.
5) Serikali kupitia waziri husika, je mna taarifa kuwa huko maofisini unaweza kuta eti mgeni mwenye diploma analipwa mamilioni na mtanzania mwenye masters anazidiwa mshahara mara kibao. Je, ni kweli eti watanzania sio sawa kupokea mishahara mikubwa huko migodini kama wazungu?
Je, serikali inajua kuwa mtanzania mmoja anategemewa karibia na ukoo mzima?
Je, haioni kuwa kama ni kweli kuna zuio huko migodini vijana wenzetu walipwe stahiki kuendana na kampuni inavyopata faida na kama ambavyo wageni wanalipwa?
6) Mabosi na wamiliki wa makampuni napenda niwaulize swali, hivi kweli kuna umuhimu gani wakampuni zenu kuajiri wafanyakazi kupitia third ambae naona kama anawageuza watumwa mfano mzuri ni mitandao ya simu haswa upande wa call center!!
Waheshimiwa nyie wakubwa nauliza, je hamuamini kuwa mfanyakazi ni sehemu ya kampuni zenu iweje mnaajiri wataalam wakitoa mapendekezo wa kitaalam hamfuati haswa mkiona ni running cost? Mfano mzuri ni moja ya kampuni ya gas hapa Tanzania.
7) Wakubwa mabosi wamiliki wa makampuni, je mnadhani ni busara kuwafanyisha interview watu wengi kisha unabakiza wachache unawakalisha muda mrefu kisha unawapiga chini? Ina maana muda walioutumia kuja kwenye interview daily nani anaubeba?
Mbona ni kama watafuta ajira hawaheshimiwi hata kidogo!! Hii ni kwa makampuni tena yenye majina lakini ukiingia kwenye website mnajitapa majali utu.
8) Mabosi wamiliki wa makampuni binafsi hivi utaratibu wakufanya interview kabisa au unatofautiana maana ni kama vile kuna baadhi ya makampuni ni pasua kichwa. Ebu fikiria mtu aliefanya interview mara tano kwenye same position anapuuzwa ila mtu aliefanya interview moja anachukuliwa. Yaani bias mchana!! Jaman sekta binafsi mchana kweupe nanyi imekuwa kujuana ukabila na mambo yasiyo ya Kitanzania.
9) Helo maprofessa,madokta,manguli wa sheria,wanauchumi,wahandisi, mbona mpo kimya kama hakuna tatizo la ajira sasa hayo maarifa mnayafanyia nini? Sijasikia hata kongamano la wasomi bingwa kujadili tatizo la ajira zaidi nawaona kwenye maoni ya kisiasa.
Jamani tuna vyuo vya elimu ya juu zaidi ya arobaini ,ina maana vigogo wa elimu mmekaaa kimya kama sinyie watanzania nani aseme sasa au kwa tayari wengi wenu mna mafanikio,haina haja ya wadogo zenu na jamaa zenu!!
Hivi ni kweli kabisa tatizo hili sio kubwa kuwaadress nationwide?
Msiawaachie wale wanatumia tatizo hili kujitajirisha na kutafuta umaarufu.
10) Jamaa zangu mlioko vyuoni na nyie wa mtaani ambao ni jobless hivi mna njia mbadala za kujikwamua na janga ambapo ni mwendo wa kujijua utatokaje?
Hivi ni kweli hili suala linawagusa kama ambavyo limenigusa mimi? Nimedhalilishwa,nimenyanyashwa kiakili,nimepotezewa muda. Je, kuna yeyote ana maumivu kama yangu?
Je, hii hali ya kudhalilishwa kisa ajira itamalizwa na nani kwa kizazi cha watoto wetu?
Nani anadhani yupo tayari kusimama na mimi tukaomba kwa sauti moja kuwa rais atoe waraka wa kufuta recruitment agent zote?
Serikali itoe muongozo jinsi ya kuendesha interview ili kupunguza unyanyasaji wakisaikolojia maana haiwezekani mtu ambae alisimamishwa kwenye pannel akalia harafu kesho ndie kaajiliwa!!. Nini maana ya interview au kupotezeana muda?
Nani yupo tayari kusema yatosha kuwa serikali sasa iondoe ukilitimba huu wa kwamba experience miaka mitano tena kwenye kazi ukifika kuna training,what for?
Je, nani yuko tayari kuomba kuonana na Rais amuelezee yanayotokea huko kwenye ajira?
Nani yupo tayari tuungane kwa kupaza sauti ambaye anajua ana logic kabisa ya kwenda kujieleza na mheshimiwa akaelewa?
11) Mwisho, serikali na waajili binfsi kama cv ya mtu hujaipenda usimwite kwenye interview maana watu wanauza mashamba,wanachukua mikopo,wengine hata wanalazimika kutembea kimwili ili wapate tu nauli ya kuja kwenye interview na kazi hakuna.
Serikali kupitia TCRA ikomeshe matapeli wa mitandaoni amabao wanatangaza ajira fake kisha wanawaibia watu mapesa mengiiiiii.
Mungu umependa niwe hapa naamini ni mapenzi yako hata kesho nikiwa pale.