Dijovisonjn
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 466
- 125
- Thread starter
- #61
Naomba nielezee kwa vipengele ulivyochambua
- Ni kweli Kenya imejengwa sana na wakoloni na rwanda ni nchi ndogo lakini kwa miaka hamsini ya utawala wa ccm yalitakiwa yawepo mabadiliko,kwanza uchache wa watu katika nchi sio sababu ya kuwa tajiri kumbuka china ina watu karibu bilioni moja na inaendelea kwa kwasi,burundi nayo ni nchi ndogo lakini bado maskini wa kutupa,TATIZO LA KIKWETE HANA VISION HAJUI HAFANYE NINI NDIO MAANA ANAKUWA MZIGO KWETU WA TZ,hao kwenye na rwanda hawana rasilimali tulizonazo sisi ,achana na madini yanayohitaji technolojia kuchibwa hata watu pia ni rasilimali serikali imeshindwa kutumia kuongeza pato la nnchi,kikwete hajui anachofanya NDIO MAANA ALIULIZWA KWA NINI NCHI YAKO MASIKINI AKAJIBU SIJUI,
- KUHUSU KUTEUA RAFIKI ZAKE,ameteua rafiki zake sio kwa kuwa ana waamini na anajua watatimiza malengo HAPANA KAFANYA HIVYO KULIPA FADHILA YA WALIYOMFANYIA KUMSAIDIA KUINGIA IKULU,KWA HIYO WAMEPEWA VYEO KAMA MSHAHARA WAJILIPE KILE WALICHOPOTEZA KWA SABABU YAKE NDIO MAANA PESA NYINGI YA SERIKALI IMEPOTEA mambo ya richmond na epa.
- pia kikwete hawezi kuwachukulia hatua kwa sababu naye ni mmoja wapo ya mambo machafu yanayofanyika namnukuu lowasa akisema katika kikao cha nec ya ccm "WATU WANANISHAMBULIA KWA KUNIITA FISADI LAKINI UNAKUMBUKA WAKATI HII KAMPUNI YA RICHMOND INAINGIA NILITAKA KUIKATAA ULIVYOWASILIANA NA WEWE UKASEMA UMEPATA TAARIFA KWA MAKATIBU WAKUU KUWA HAINA TATIZO IENDELEE NA KAZI" kwa hali kama hiyo kikwete akichelewa kufanya maamuzi utasema anapima faida na hasara?
- Rais kusafiri ,watu sio kwamba wanataka rais asisafiri tatizo ni safari za mara kwa mara na rais huwa anasafiri na msafara kiasi kwamba yanatumika mabilioni ya fedha,kuna mengine ambayo unakuta hata angeenda waziri ingetosha ambaye garama zake za usafiri ni chache kulingana na rais,ni kweli technolojia yetu ndogo lakini kuna mawaziri wengi wanaweza kuliwakilisha taifa,HATUTEGEMEI RAIS AENDE MAREKANI ALAFU AKAPIGE PICHA NA 50CENT au kwenda kuomba kikampuni fulani cha IT kije kiwekeze TZ wakati ni vitu vizuri lakini hata balozi angevifanya achana na wakurugenzi,makatibu wakuu au mawaziri
sijaongelea idadi ya watu (population) bali nliongelea eneo la kijografia (territory) ya nchi husika.
Yote Kikwete anayofanya yupo sahihi (sio makosa) katiba ina mruhusu, je unadhan kuna ulazima kwenye katiba mpya tuweke ni safar zipi raisi anatakiwa kusafir kwa mwaka na nyingine awaachie mawaziri?
Na je unadhan kuwa raisi anaweza kuteua wasaidizi wake bila kuwalipa wadhila wale jamaa zake wa karibu? Kama unaamin ni kivipi? Na vp anaweza kukacha kulipa fadhila?
Na unadhan tatizo ni JK au ni mfumo wetu wa kiuongozi?