Dijovisonjn
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 466
- 125
- Thread starter
- #21
Unafahamu kuwa mwanzoni British ndiye aliyekuwa ana teknolojia ya juu kuliko nchi zote za ulaya? unafahamu kuwa aliwahi kufanya maoesho ya teknolojia yake na kualika nchi nyingine kwenda kushuudia? anatambua kuwa tokea wageni wale walimuibia mbritish teknolojia yake? na je unatambua kuwa huo ndo ukawa mwanzo wa kufichwa kwa siri za teknlojia? na je unatambua kuwa ni vigumu sana na kwa kuifundisha nchi nyingne teknolojia yake labda kwa makubaliano maalumu? na je unatambua kuwa nchi za magharibi haziwezi kupromote maendeleo yako kwa kukupatia teknolojia yao kwa sababu wanaamini na wewe utaendelea na watakosa nafasi ya kukunyonya? Na je unatambua kuwa mwl Nyerere alikuwa anapewa teknolojia na nchi za kijamaa wakati ule wa vita baridi ya ubapari na ujamaa? Na je unatambua kuwa cku hizi ujamaa haupo tena? NADHANI UMENIELEWA, SASA TUFANYAJE KUIKOMBOA TZ YETU?kwa hicho kipengele cha nne tu Bila ya kuwa na technology hatuwezi kuendelea kwa maana tutashindwa ku-export bidhaa zetu wenyewe. Hivyo angeenda nje kuomba Technology na sio msaada. Nyerere alichokifanya mpaka tukawa na viwanda vingi vikiwemo General tyre na Nyumbu ni kwamba alikuwa anasafiri kwenda kuomba technology na sio misaada ndio maana kama warithi wake wangeendeleza ile sera ya ujamaa na KUJITEGEMEA tungekuwa na viwanda vingi Hai na tunge export bidhaa nyingi sana. Lakini kwenda kuomba misaada ndio yaleyale mtu anakuchimbia kisima cha maji nyumbani kwako halafu anakuuzia maji miaka yote kisa wewe hujui kuchimba na huna vifaa kwanini asikufundishe wewe kuchimba? Angalia gesi inachimbwa kwetu na tunauziwa sisi je, tungekuwa na hiyo Technology sisi wenyewe Tanesco ingekuwa hapo ilipo? Tusingeuza umeme wa ziada nje? Hiyo ni mifano tu ya kutafuta technology na SIYO MISAADA.