Leo naomba nimtetee mheshimiwa raisi wangu ndugu J M Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo naomba nimtetee mheshimiwa raisi wangu ndugu J M Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dijovisonjn, Apr 10, 2012.

 1. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa naomba niseme kama wewe unadhani utachangia hizi hoja zangu kwa matusi ni bora ukasoma tu na kupotezea, natamani kuona wale wote watakao changia hapa wachangie kwa lengo la kujenga na sio kujionesha bora zaidi ya wengine. Nikiwa kama mtanzania wa kawaida nisiyeamini katika chama chochote kile cha siasa katika hii dunia lakin mfuatiliaji mzuri wa masuala ya siasa za dunia (nadhan ni kwa vile nasoma POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION (BA PSPA)) nimeguswa kidogo leo walau kumtetea raisi Kikwete japo mi sio msaidizi wake wala sio mfuasi wake ila kama mtanzania nliye chini ya utawala wake naamini nina haki 100% kumtetea raisi wangu kwa nguvu zangu zote.
  Katika mitandao mbalimbali na hata hapa JF raisi Kikwete amekuwa akipewa lawama kibao mfano juu ya ufisadi, umaskini wa mtanzania, kushuka kwa uchumi, kuwa mzito wa kutoa maamuzi n.k naamini hizi lawama zote JK anazifahamu ila aidha kwa kuzipuuzia, au kwa kuwaacha watu waongee tu watakavyo coz kuna uhuru wa kuongea am eamua kukaa kimya. Binafsi naomba nitoe ufafanuzi kidogo wa baadhi ya lawama kwa mh. raisi.

  1) Tanzania tupo nyuma kimaendeleo tukijilinganisha na jirani zetu. Hii ni kweli sisi tupo nyuma kimaendeleo ukitulinganisha na nchi kama Kenya na Rwanda, lakin hii sio kwa sababu ya JK, kihistoria Kenya ilikuwa kolononi la kilowezi yaani ni kwamba wazungu walikaa/kuishi Kenya na kujenga miundombinu na huduma za kijamii mfano hospitali, shule n.k, pia walianzisha mashamba makubwa pia kwa kuwa Muingereza ndiye aliyekuwa mtawala wa nchi nyingi za Afrika mashariki, aliifanya Kenya kama makao makuu yake, kwa sababu hii Muingereza aliweza kuijenga Kenya zaidi kuliko koloni lolote lile ndani ya Afrika Mashariki ndo maana leo Kenya ipo juu zaidi ya nchi zote za Afrika Mashariki.
  Kwa upande wa Rwanda, naamini wote mnatambua kuwa Rwanda kijografia ni nchi ndogo sana kwa kuilinganisha na Tanzania kitu ambacho kinawasaidia wanyarwanda kusimamia shughuli za kimaendeleo na mali asili zao kikamilifu zaidi.

  2) Kuwateua rafiki zake kuwa wasaidizi wake wakuu katika uongozi wake. wengi wanaamini kuwa kosa kubwa alilofanya JK ni kuwateua rafiki zake kuwa wasaidizi wake kitu ambacho kinamsababisha kushindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu pindi wanapofanya makosa, Binafsi naamini kuwa JK hakufanya kosa kuwateua rafiki zake kwa sababu kiongozi yeyote yule huteua wasaidizi ambao kwa 100% anaamini kuwa watamsaidia katika uongozi wake, hakuna raisi anayeteua watu asioamini kama watamsaidia kutimiza lengo lake, naamin hata siku mimi nikiwa raisi siwezi kukuteua wewe nisiyekufaamu wala kuamini kama kweli utanisaidia katika uongozi wangu. Kuhusu kutokuwachukulia hatua hawa wasaidizi wake naielezea hapa kwa chini.

  3) Kuchelewa kufanya maamuzi au kushindwa kabisa kufanya maamuzi. Inasemekana kuwa na huu ni udhaifu wa JK, kwanza naomba niseme kuwa mtu kuwa raisi ni tofauti na mtu kuwa baba au mwenyekiti wa taasisi fulani, sifa kubwa ya mfanya maamuzi ni kupima faida na hasara za maauzi atakayofanya katika jamii husika na kama maauzi hayo yana faida kubwa kwa jamii yambidi ayafanye na kama hayana faida kubwa kwa jamii sio lazima/haitakiwi kuyafanya hayo maamuzi. Hapa naomba niwakumbushe tu kuwa JK ni raisi na mwenyekiti wa CCM ivyo basi katika maamuzi yake ni lazima yawe na faida kote kote kwa CCM na kwa serikali, maamuzi yeyote kwa serikali yasiyo na faida kwa chama hayatakiwi, hii sio kwa CCM tu bali hata wewe chama chako kikiingia madarakani kitafanya hivi, na kwa sababu hii ndio maana anashindwa kuwachukulia hatuna wasaidizi wake wa karibu haswa haswa mawaziri kwa lengo la kukilinda chama kisisambaratike.

  4) Kusafiri nchi za nje na kuomba misaada. Naamini hata kama Obama ndo angekuwa raisi wetu naye angekuwa anasafiri kama JK anavyosafiri, watanzania wenzangu, japokuwa tuna rasilimali nyingi sana hapa kwetu tatizo ni kwamba hatuwezi kuzitumia hizo rasilimali sisi wenyewe, mbali na kuzitumia hata namna ya kuzivuna hatujui kwa sababu teknolojia yetu ni ya chini saaaana, hivyo ili walau tufaidi kidogo hizi rasilimali zetu tutahitaji kuwaomba wenye ujuzi na teknolojia yao waje watunyonye kidogo, hali hii haisababishwi na JK bali ni kwa sababu ya mfumo tulioachiwa na wakoloni (ukoloni mamboleo)

  kwa udogo na uchache ndo hayo tu kwa leo.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  unacho jaribu kukifanya ni kusema mavi yana nukia haya nuki....
   
 3. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  kwa hicho kipengele cha nne tu Bila ya kuwa na technology hatuwezi kuendelea kwa maana tutashindwa ku-export bidhaa zetu wenyewe.
  Hivyo angeenda nje kuomba Technology na sio msaada. Nyerere alichokifanya mpaka tukawa na viwanda vingi vikiwemo General tyre na Nyumbu ni kwamba alikuwa anasafiri kwenda kuomba technology na sio misaada ndio maana kama warithi wake wangeendeleza ile sera ya ujamaa na KUJITEGEMEA tungekuwa na viwanda vingi Hai na tunge export bidhaa nyingi sana.
  Lakini kwenda kuomba misaada ndio yaleyale mtu anakuchimbia kisima cha maji nyumbani kwako halafu anakuuzia maji miaka yote kisa wewe hujui kuchimba na huna vifaa kwanini asikufundishe wewe kuchimba?
  Angalia gesi inachimbwa kwetu na tunauziwa sisi je, tungekuwa na hiyo Technology sisi wenyewe Tanesco ingekuwa hapo ilipo? Tusingeuza umeme wa ziada nje? Hiyo ni mifano tu ya kutafuta technology na SIYO MISAADA.
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Siamini kama kuna mtu mwenye akili timamu akatumia muda wake mwingi kwenye keyboard kuandika huu ushuzi, au upo field ya typist course?
   
 5. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Magamba at work!CRAAAAAAAAAAAAAAPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPP!!!!!!!!!!!!
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwanini uombe wewe toka kifua mbele na unachokiamini. Hii kuomba nikama unahitaji huruma fulani
  too low!
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Asante kwa mawazo yako!
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na wewe unajiita Great Thinker!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Pedestrian thinking. Hakika wewe IQ yako ni below 20. So unastahili kumwita kenge ni mamba.
   
 10. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hio shule unayosoma kama ndio mawazo ya hivi unayo haitakusaidia ..jaribu kitu kingine
   
 11. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  weka hitimisho sasa.
   
 12. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama ni kweli mimi nafanya hicho unachodhani nakifanya, hebu tujaribu kufanya kitu kimoja hivi, jiweke kwenye nafasi ya JK then tell us what your going to do to save our country?
   
 13. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna lolote hapa.
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  childish!
   
 15. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama ni kweli mimi nafanya hicho unachodhani nakifanya, hebu tujaribu kufanya kitu kimoja hivi, jiweke kwenye nafasi ya JK then tell us what your going to do to save our country?
   
 16. M

  Masabaja Senior Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dogo kama unasoma degree halafu unasema Rwanda imeendelea kwa sababu ni nchi ndogo je mbona marekani imeendelea na ni nchi kubwa. Kwa hiyo kumpata mtendaji lazima uwe unamfahamu au unatafuta mtanzania mwenye sifa zinazotakiwa na kufanyia verting kujua records zake kisha unampa nafasi ya kutumikia umma sasa kama ni rafiki na hana sifa inakuaje nina wasiwasi na elimu unayosoma kama ndiyo elimu ya chuo kikuu unayosoma nchi yetu inaenda wapi?
  Unaweza ukawa unataka kuwasilisha hoja lakini kwa utetezi wako nenda kajipange
   
 17. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Amesema anasoma degree ya siasa, sasa hapa naona anataka tumsaidie kutoa mawazo atakayoyatumia kwenye utafiti wa shahada yake ambayo nadhani title yake inaweza kuwa THE SHORT_COMINGS OF KIWETE'S RULE 2005-2015!!!!
   
 18. Nani Kasema

  Nani Kasema Senior Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pumba tupu

  eti hawa ndio wasomi wa political science?

  pyuuuuuuu
   
 19. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  If I were in his shoes I would do the exact opposite of what he is doing. People would be appointed to leadership positions not on the basis of religion or friendship but on the basis of their professionalism and ability to deliver. I would spend more time in the country making timely decisions on pressing issues instead of globetrotting. I would promptly fire any civil servant a' la Jairo who had been proven to put his hands in the nation's till.
   
 20. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Naomba nielezee kwa vipengele ulivyochambua
  • Ni kweli Kenya imejengwa sana na wakoloni na rwanda ni nchi ndogo lakini kwa miaka hamsini ya utawala wa ccm yalitakiwa yawepo mabadiliko,kwanza uchache wa watu katika nchi sio sababu ya kuwa tajiri kumbuka china ina watu karibu bilioni moja na inaendelea kwa kwasi,burundi nayo ni nchi ndogo lakini bado maskini wa kutupa,TATIZO LA KIKWETE HANA VISION HAJUI HAFANYE NINI NDIO MAANA ANAKUWA MZIGO KWETU WA TZ,hao kwenye na rwanda hawana rasilimali tulizonazo sisi ,achana na madini yanayohitaji technolojia kuchibwa hata watu pia ni rasilimali serikali imeshindwa kutumia kuongeza pato la nnchi,kikwete hajui anachofanya NDIO MAANA ALIULIZWA KWA NINI NCHI YAKO MASIKINI AKAJIBU SIJUI,
  • KUHUSU KUTEUA RAFIKI ZAKE,ameteua rafiki zake sio kwa kuwa ana waamini na anajua watatimiza malengo HAPANA KAFANYA HIVYO KULIPA FADHILA YA WALIYOMFANYIA KUMSAIDIA KUINGIA IKULU,KWA HIYO WAMEPEWA VYEO KAMA MSHAHARA WAJILIPE KILE WALICHOPOTEZA KWA SABABU YAKE NDIO MAANA PESA NYINGI YA SERIKALI IMEPOTEA mambo ya richmond na epa.
  • pia kikwete hawezi kuwachukulia hatua kwa sababu naye ni mmoja wapo ya mambo machafu yanayofanyika namnukuu lowasa akisema katika kikao cha nec ya ccm "WATU WANANISHAMBULIA KWA KUNIITA FISADI LAKINI UNAKUMBUKA WAKATI HII KAMPUNI YA RICHMOND INAINGIA NILITAKA KUIKATAA ULIVYOWASILIANA NA WEWE UKASEMA UMEPATA TAARIFA KWA MAKATIBU WAKUU KUWA HAINA TATIZO IENDELEE NA KAZI" kwa hali kama hiyo kikwete akichelewa kufanya maamuzi utasema anapima faida na hasara?
  • Rais kusafiri ,watu sio kwamba wanataka rais asisafiri tatizo ni safari za mara kwa mara na rais huwa anasafiri na msafara kiasi kwamba yanatumika mabilioni ya fedha,kuna mengine ambayo unakuta hata angeenda waziri ingetosha ambaye garama zake za usafiri ni chache kulingana na rais,ni kweli technolojia yetu ndogo lakini kuna mawaziri wengi wanaweza kuliwakilisha taifa,HATUTEGEMEI RAIS AENDE MAREKANI ALAFU AKAPIGE PICHA NA 50CENT au kwenda kuomba kikampuni fulani cha IT kije kiwekeze TZ wakati ni vitu vizuri lakini hata balozi angevifanya achana na wakurugenzi,makatibu wakuu au mawaziri
   
Loading...