Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 16,958
- 7,512
Naamini tukiandika humu kumbe huwa unapita sana na kusoma sana. Wiki moja imepita niliandika hapa Jf nikikusihi jambo jema la wewe kuanza kufikiria namna ya kuwatambua, kuwaenzi na kuwaweka karibu wale waliokutangulia katika uongozi. Nilisema nchi yetu tunahitaji kuwaenzi wazee hata kama kuna mahala walikosea na kweli walitukosea, ni vizuri kutokujenga ukuta ijapo naamini wengine hawakuwa labda karibu sana na wewe lakini Tz ni moja, Tanzania kwanza. Na katika kulielezea vizuri hili, nilitolea mfano kupitia nchi ya marekani kama case study yangu.
Leo nakupongeza kwa kulitimiza hili, hakika nafsi yangu imefarijika sana kwa hii hii hafla ya leo hapo Ikulu. Ukiwa pamoja na mgeni wako rais Lungu, umefanya jambo la maana sana kitaifa na kihistoria pia.
Namwona JK, Mwinyi, Karume, CJ, CDF, Msekwa, PM, N.spika, Warioba, Mawaziri na wengine wengi ...nakupongeza sana kuwatambua na naamini ulichokikusudia leo kitakuwa kimetimia kwa 100%
Hongera sana!