Leo nakupongeza Rais Magufuli kwa kuwapa heshima viongozi hawa

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Naamini tukiandika humu kumbe huwa unapita sana na kusoma sana. Wiki moja imepita niliandika hapa Jf nikikusihi jambo jema la wewe kuanza kufikiria namna ya kuwatambua, kuwaenzi na kuwaweka karibu wale waliokutangulia katika uongozi. Nilisema nchi yetu tunahitaji kuwaenzi wazee hata kama kuna mahala walikosea na kweli walitukosea, ni vizuri kutokujenga ukuta ijapo naamini wengine hawakuwa labda karibu sana na wewe lakini Tz ni moja, Tanzania kwanza. Na katika kulielezea vizuri hili, nilitolea mfano kupitia nchi ya marekani kama case study yangu.

Leo nakupongeza kwa kulitimiza hili, hakika nafsi yangu imefarijika sana kwa hii hii hafla ya leo hapo Ikulu. Ukiwa pamoja na mgeni wako rais Lungu, umefanya jambo la maana sana kitaifa na kihistoria pia.

Namwona JK, Mwinyi, Karume, CJ, CDF, Msekwa, PM, N.spika, Warioba, Mawaziri na wengine wengi ...nakupongeza sana kuwatambua na naamini ulichokikusudia leo kitakuwa kimetimia kwa 100%

Hongera sana!
 
Hakuna hata mmoja kutoka Upinzani Kaalikwa? Ni wazo limenijia nimehisi iyo niya kitaifa zaidi na sio kichama au??
 
Kwa Hii Habari Yako Huenda Ulikuwa Hujui Kitu Kuhusu Dhifa Kama Hizo,Mara Zote Hao Uliowataja/Wengine Hukuwataja Hualikwa Ikulu Na Mh. Rais Sema Unapoona Wengine Wanakosekana Ni Kwaajili Ya Majukumu Ya Nchi Hii.

Siku Nyingi Huwa Hivyo
 
Back
Top Bottom