Leo nahisi mke wangu anachepuka huko alipoenda

kabunda88

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
3,095
2,680
Wakuu ipo hivi nilisafiri toka Jutano mkoa fulani plan ya kurudi ilikuwa Jumamosi kesho jioni lakin nikaamua tu nirudi leo kwa sababu kazi nilionda kufanya imeisha toka jana jioni.

Sasa nikampigia mchepuko wangu leo narudi aje anipokee leo narudi zangu Dar , na nikamwambia nitafika saa kumi na moja so awe hapo.

Huku wife anajua kesho Jumamosi ndio nakuja tena jioni sana ndio ratiba nilivyompa ila plan yangu ni nikalale sehemu na mchepuko wangu na kushinda nae mpaka jioni.

Nimefika stand sijamkuta napiga simu hapokei nikasema poa acha tu niende zangu home kwanza nimechoka sana nitamchek next time huu ni mchepuko haunaga shida niko nae kitambo na anamjua wife vizuri sana ,pia anasubiri nimwoe mke wa pili nimemwambia awe na subira.

Hata hivo nimefika home ndio mchepuko anajibu Sorry nilipitiwa nilikuwa nimelala so nakusubiri tunafanyaje nikamjibu Poa subiri nitakwambia,

Tatizo nimerudi home wife hayupo na sasa inaenda saa tatu usiku nimefika toka saa moja usiku na nimempigia simu just kumwambia vipi huko unaendeleaje kasema yupo home anaangalia tamthilia zake yaani hapa nilipo uongo sijui kaanza lini huyu wife

Tena kwa sauti kavu kabisa anasema nipo nyumbani anaangalia tu tamthilia na anaanza kunihoji unarudi saa ngapi kesho mi nikamjibu tu kesho usiku saa mbili hivi kasema sawa nimletee zawadi.

Nafikiri tabia hii imeanza muda kidogo japo huwezi kujua kirahisi ila mtu unayekaa nae mabadiliko kidogo tu utajua kuna shida maana alikuwa hayupo huru sana na simu yake na hata akiiweka anaigeuza sehemu ya mbele inakuwa chini na password kabadilisha na simwoni tena kufatilia nyendo zangu kama zamani.

itakuwa kuna msela ameshakula mzigo tayari naleo mida hii itakuwa anakula.

Nimefika tu kuingia ndani bafuni mtu ameoga,mswaki amepiga,na ni kama tumepishana tu mi nafika saa moja kamil yeye itakuwa ametoka saa kumi na mbili jioni.

Hapa nawaza sijui nimpigie tu mchepuko wangu nikalala huko au nimpigie wife arud home .

Inauma lakini hebu wakuu nipeni msaada tumezaa nae watoto wawili wote madume sema walienda kwa bibi yao mwezi sasa ndio maana amekuwa huru kutoka.

Pia huwa inaeza kuwa hata mimi nimechangia maana huwa nachepuka mara kwa mara lkn hajawahi kunikamata ila hiyo haihalalishi yeye pia achepuke.

Nawasilisha.

Mrejesho wa kisa hiki soma hapa:Mrejesho: Kilichotokea baada ya wife kurudi saa sita usiku
 
Habari ya kwako shehe.

Kwa kweli nimesoma yanayokusibu sio siri inauma kama mwanaume. Na sidhani kama yeye anajua ama ndio kuumizana moyo.

Tatizo kubwa ambalo nimeliona na wewe inabidi udili nalo mapema kabla hujachelewa kwa nini mkeo amekuambia umletee zawadi na wala hajataja anataka zawadi gani?

Sasa ukisema unamletea nguo wakati yeye anataka biskuti ama keki hauoni itazidi kuleta mchanganyiko?

Mwanamke wako alitakiwa akuambie ukirudi mletee zawadi ya simu ama pochi ama viatu sio kukuweka wewe hewani kama nyaya za umeme yakhe.

Ukiweza solve hilo tatizo la zawadi mtaishi maisha mema na mazuri mstarehe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom