Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Tafadhali jumuikeni nami kuanzia saa 2:00 hadi 2:30 usiku huu wa leo kwa ajili ya kumuombea Rais Magufuli.
Maandiko yanasema wanapokusanyika wawili au zaidi Mungu atayapokea maombi hayo. Umbali siyo tatizo, kwenye mambo ya kiroho hakuna umbali.
Tumuombee afya njema, hekima, huruma, maarifa, roho ya kiasi na kuepuka hasira.
Najua wengi tuna maoni HASI kuhusu Rais Magufuli na serikali yake ila inabidi tukumbuke wote tuko kwenye boti moja. Ikizama tunazama wote na najua wengi wetu hata kuogelea hatujui.
Kuna njia halali za kumshinikiza Rais na serikali yake. Kwa mfano bado naamini maandamano ni njia sahihi na ambayo ingeweza kutumika ila kila Afande Mroto akitoa vitisho watu wanapoteana. Hilo siyo la kumlaumu Rais Magufuli ni woga wetu sisi wenyewe.
Kutumia njia za hila, blackmail na zingine za kiuhalifu ili Rais atimize matakwa ya kundi fulani siyo njia sahihi. Rais ana madaraka makubwa sana, anaweza kuamua kulianzisha hapa na hakuna atakayeweza kumzuia. Tuwe makini sana.
Nimekumbuka Mfalme Sauli alikuwa anamsakama Daudi kwa muda mrefu ili amuue ila Daudi pamoja na kwamba tayari alikuwa ameshapakwa mafuta na Nabii Samuel ya kuwa mfalme lakini hata alipopata nafasi mara kadhaa ya kummaliza Sauli kwa mikono yake mwenyewe hakufanya hivyo. Alimuachia hilo jukumu Mwenyezi Mungu mwenyewe.
Kumbuka ni kuanzia saa 2:00 hadi 2:30 usiku huu wa leo. Tafadhali usizembee na mtaarifu mwenzio.