Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,181
- 5,321
Mimi kama Mtanzania ninalahumu media za bongo kwa kuwa na double standards hasa linapokuja suala la kuhabarisha umma juu ya matukio ya muhimu.
Mfano mzuri ni juzi limetokea tetemeko lenye ukubwa wa licha skeli 4.7 mkoani mara hili halikuwa suala la kupotezewa kabisa kisa limetokea upande fulani wa nchi hivyo alikupaswa kupata attention ya vyombo vya habari.
Hapa nawaza tu je, kama lingetokea Dar es salaam au Dodoma pia msingetangaza? Au kulipa headlines kwenye magazeti,televisheni na redio zenu? Au ni kwasababu waliokumbwa na janga ni akina Mara, Simiyu, Katavi nakadhalika kwahiyo haina inshu.
Masuala kama haya yahusuyo natural calamities mfano wa volcanic activity hayapaswi kufumbiwa macho na pia ni haki ya raia kujua kinachoendelea katika mazingira yao hasa pale jambo lenyewe linapoweza kuhatarisha maisha au kuleta taharuki katika jamii.
Mwisho media za Tanzania zibadilike habari si udaku tu na siasa hata majanga pia ni habari yawe yameleta madhara au la, kikubwa habari ikitolewa inaweza vutia hata attention ya wataalamu kuanza kuchunguza kuwa chanzo ni nini hasa maana si mara ya kwanza kwa kanda ya ziwa kukumbwa na tatizo hili siku za hivi karibuni.