Leo mbunge mmoja wa chadema sawa na wabunge 30 wa ccm, kesho mbunge mmoja wa ccm sawa na wabunge 60 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo mbunge mmoja wa chadema sawa na wabunge 30 wa ccm, kesho mbunge mmoja wa ccm sawa na wabunge 60

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dijovisonjn, Mar 13, 2012.

 1. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa alivyosema mh. Mbowe kuwa mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 30 wa CCM.

  Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini wabunge wa ccm (walio wengi sio wote)
  ni very weak? hawajui kujielezea, hawajui kujenga hoja? kama hukupata majibu mimi nitakusaidia kukujibu leo, ni kwa sababu chama chao ndio kinashika dola, ni kwa sababu wengi wao walitumia pesa kuupata ubunge na ni kwa sababu wamelizika na mambo yanayofanywa na serikali yao ya CCM!
  Na je ulishawahi kujiuliza kuwa ni kwa nini wabunge wa CHADEMA ni wazuri kujielezea, kujenga hoja na kuonekana kwenda sawa sawa na wale wa CCM japokuwa wao ni 48 tu? Na hapa nikusaidie kukupa jibu ni kwa sababu wengi wao ni vijana (wanatafuta umaarufu wa kisiasa), wengi ni wasomi,hawakuingia bungeni kwa pesa na sasa wanajitahidi kumaintain position yao katika jamii na sababu kuu ni kwa sababu chama chao hakijashika dola!
  Hivi ulishawahi kujiuliza siku CHADEMA ikishika dola hali itakuwaje bungeni?
  mi naona hivi:-
  Wabunge 60 wa CHADEMA watakuwa sawa na mbunge 1 wa CCM.

  kivipi?

  kwanza, wabunge wa CHADEMA watapunguza ukali wao bungeni na kuwa bize kuitetea serikali.

  Pili, mawaziri wengi wa CHADEMA watakuwa hawana na uzoefu wa kiutawala wakati wapinzani wao watakuwa na uzoefu mwingi na wakutosha (kumbuka uwaziri kivuli unatofauti kubwa sana na uwaziri kamili)

  Tatu, CHADEMA wakiingia madarakani watataka kuongoza tofauti na CCM wanavyoongoza kitu ambacho kukiongea ni rahisi lakini kukitekeleza ukiwa madarakani ni vigumu mno. kwa mfano kama Dr Slaa angeshinda katika uchaguzi wa 2010 angewezaje kutengeneza serikali yake bila kuwachagua wale anaowafahamu na kuamini ndo atakaoweza kufanya nao kazi? naamini hata kama mimi ningekuwa na uwezo gani asingenichagua kwa sababu hanijui na wala sijawahi kufanya naye kazi (kitu ambacho JK amefanya na hata kiongozi yeyote atalazimika kufanya kama JK)

  Nne, CHADEMA watataka kutuonesha watanzania kuwa hatujakosea kuwachagua kutuongoza nahisi watakuwa wanafanya maamuzi mengi ya kuturidhisha wananchi kwa 100% kitu ambacho ni hatari kwa uongozi.

  Tano, kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika, CHADEMA na wao hawataongoza bila kuwa na msukumo kutoka nchi za magharibi, kitu ambacho ni hatari kwa viongozi woooote wa Afrika.

  HITIMISHO.
  UZOEFU WA KISERIKALI WALIONAO VIONGOZI WENGI WA CCM NA UKOSEFU WA UZOEFU WA UONGOZI WA KISERIKALI WALIONAO VIONGOZI WENGI WA CHADEMA UTAWAFANYA WABUNGE 60 WA CHADEMA KUWA SAWA NA MBUNGE MMOJA WA CCM SIKU CHADEMA WAKISHIKA DOLA!


   
 2. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Very poor!
  Aliyekuambia wabinge wanaongoza aerial ni nani? Zitakuwa bange tu hizo.
  Hivi unafikiri serikali ni Kama Yanga SC? Kwamba wakati wa uchaguzi basi viongozi wote wanabadilishwa? Kwamba wizara zitahitaji wafanyakazi wapya?

  Mwanaasha at it again!
   
 3. D

  DOMA JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Pumba zako peleka facebook
   
 4. Oscar Kimaro

  Oscar Kimaro Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unatuchosha tuu bure!!:crazy:
   
 5. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Natambua hujui kuwa katiba ya sasa ya Tanzania hairuhusu kuteuliwa kwa waziri asiye mbunge, natambua haujui kuwa katika mfumo wa siasa zetu ni jukumu na wajibu wa mbunge kuwawakilisha wale waliomchagua pamoja na kukiwakilisha chama chake natambua hutambui kuwa ni wajibu wa mbunge kukitetea chama chake serikalini na mwisho natambua kuwa huwa hata hufuatilii bunge hata hili la sasa na kuona wabunge woote wakichangia na kupiga kura kwa matakwa ya vyama vyao.
  ndugu yangu hacha kuwaza ma kufanya maamuzi kwa kuegemea vyama vya siasa hebu jifunze kwenda na uhalisia
   
 6. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamii forums ni social network facebook ni social network zote tunazitumia kuelimishana
   
 7. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nawachosha kwa sababu wengi hampendi kuwaza au kufikiri wenyewe kwa kujitegemea badala yake mnapenda watu wengine wawaze na kufikiri kwa niaba yenu
   
 8. mchadema

  mchadema JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  ni social network ila inamlengo tofauti. Hapa hatujadili vi2 vyakufikirika kama ulcholeta, tunajadili wada zenye tija, hi pumba ulitakiwa uweke kule facebook kwenye watu wengi wa dizaini yako, umekosea mlango mkuu. Hz akili kama za samaki lazima zitoe hypothetical ideas za aina hii.
   
 9. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  umefubaa kaka
   
 10. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  maskini mtanzania mwenzangu, kumbe pa1 na kujiita mchadema lakin hujawah kuwaza nini kitatokea kama chadema wakishika dola? eti "vi2 vyakufikirika" ndugu yangu mpaka leo unatumia maneno haya ya kizamani kujidefence? kama hujui msamiati"vi2 vyakufikirika" ni msamiati unaopatikana kwenye kamusi ya wapumbavu!
   
 11. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kati yangu mimi ninayewaza future na wewe unayewaza past ni nani aliyefubaa?
   
 12. m

  matamvua Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hujuii unalofikiria jaribu tena baadaye.
   
 13. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,506
  Likes Received: 2,054
  Trophy Points: 280
  JUSSA brain disease at work..
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Wabunge wengi wa CDM ni makanjanja wa siasa, watupu na weupe kama pamba
   
 15. B

  Benaire JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Uongozi huwa hauna uzoefu..uzoefu ni propaganda ambazo hutumiwa na viongozi wasio waadilifu kulinda maovu yao...uzoefu wa kuiba au kunyonya wananchi bila kujua,kwa hili la uzoefu ni kitu ambacho ni unpredictable katika uongozi hata wakoloni walidai waafrika hawana uzoefu katika masuala ya uongozi.
  Suala la kuongoza tofauti na utawala uliopita linatekelezeka na sio gumu hapa afrika.
  Fuatilia Rwanda na Zambia kwa sasa!
  By the way umechambua vizuri lakini bado nasisitiza utendaji wa CDM madarakani ni unpredictable sababu hatuna uhakika na personnel watakao kuwa wabunge kwa CCM labda new faces,the same thing to other parties...hapo utasema bunge linatabirika?
   
 16. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hivi ni kwa nini badala ya kutafakar na kufafanua kile kilichosemwa mnakimbilia kumshambulia mtu?
  Binafsi mimi Dijovison Josephat sio mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha siasa,
  siku zote naongea ukweli ili kukusaidia mtanzania mwenzangu kujua kile usichokijua.
   
 17. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sio kweli ulichosema, naweza kukiri kwa sasa wabunge wa chadema ndiyo wabunge bora katika bunge letu (kwa kuangalia sifa za mbunge bungeni) wasiwasi wangu ni kwamba sina uhakika kama watakuwa na ubora huo siku chadema ikishika dola!
   
 18. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  unafikiri hao wazoefu wa ccm watakuwepo?tutakuwa tumewafunga tayari kwa wizi wa mali za umma.hivyo watakaobaki wazoefu ni wa cdm peke yake.pia ccm nayo itakuwa imekufa hivyo hakuta kuwa na ccm tena.
   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Pamoja na hoja zako nataka nikukumbushe utetezi kwa serikali upo tu pale serikali yenyewe inapokuwa haiwajibiki kwa wananchi badala yake huwajibika kwa chama, kwahiyo huo ni utabiri wako kwamba cdm nacho kitaunda serikali ya kutumikia chama na si wananchi kama ilivyo sasa kwa magamba na serikali yao! Lakini kwa sera za cdm ni kuwa na serikali itakayo wajibika kwa wananchi na wakifanikiwa kufanya hivyo kuna hatari ya mbunge mmoja wa cdm kuwa wabunge 60 wa magamba.
   
 20. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,966
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  hayo ni mawazo yako na upeo wako wa kuchambua mambo ndipo ulipogota..ccm ilitoka mikononi mwa wananchi na kuwa chama cha watu wachache wenye pesa mingi..wakahodhi rasilimali zote za nchi..na wengi wa ccm wanagombea ubunge ili wawe na maisha safi na sio kutetea wananchi ndio maana wanamwaga pesa mingi..na ndio maana huwa wanakaa mbali na wananchi wakifanya biashara zao..watu wenye nia ya dhati wapo cdm..wao wamepima na kuona nchi inaingia shimoni..mtu kama mbowe,dr silaa, tundu, zitto,mnyika,mdee na wengine ccm inawahitaji na walikuwa na uwezo wa kwenda na leo wangekuwa wakubwa tu..dr silaa aliombwa apelekwe UN akakataa..kila watu na zama zao..ccm ndio wamefikia hapo kiuongozi..ndio maana hata ANC,republican,UMD na vyama vingine vya siasa vina taratibu tofauti za uongozi..umesukumwa tu na itikadi lakini umewaaibisha waliokusuma kuandika hayo..
   
Loading...