zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,039
- 28,688
Habari za jioni wana JF,
Natumaini wote wazima humu, na moja kwa moja niende kwenye mada.
UTANGULIZI
Leo major alikuwa mwanajeshi wa Canada ambaye aliyepigana vita mbili kubwa na kuibuka shujaa wa aina yake yaani Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1940s) na Vita vya Korea (1950s). Leo alizaliwa mnamo january,1921 huko Bedford Massachusets, USA na baadae wakahamia nchini Canada ambako ndio ulikuwa uraia wa wazazi wake. Inaelezwa kuwa Leo tokea utotoni hakuwa na uhusiano mzuri na baba yake hivyo ikapelekea aishi mbali naye (kwa shangazi yake) na kwakuwa alijua baba yake alimdharau sababu hakuwa na "jipya" hivyo hakuwa na mchango wowote kwenye familia ikampelekea leo kuamua kujiunga na jeshi la Canada mwaka 1940 ili aweze kuthibitisha kwa baba yake kuwa yeye ni "hazina" kwenye taifa na familia na sio "mzigo" kama walivyofikiri.
VITA KUU YA DUNIA YA PILI
Akiwa jeshini Leo alipangwa kushiriki vita kuu ya pili ya dunia na alikuwa mmoja ya wanajeshi ambao walihusika kwenye operation D-Day kule Normandy ambapo majeshi ya Marekani,Canada na washirika yalivamia ulaya ili kuikomboa kutoka mikono ya Ujerumani chini ya Hitler. Inaelezwa kwamba akiwa Normandy aliweza kuteka kifaru cha Wajerumani akiwa peke yake huku akipambana na maadui takribani 10 kwenye kifaru, kitendo hiki kiliwawezesha kunasa mawasiliano muhimu na taarifa za kiintelijensia zingine ambazo ziliwasaidia kufichua maficho ya wajerumani na kurahisisha uvamizi wao huko Ufaransa. Siku chache baadae Leo major alikumbana na kikosi cha wanajeshi wa Kijerumani na Major alifanikiwa kupambana nao kishujaa akiwa peke yake hadi kufanikiwa kuwaua wanne lakini kwa bahati mbaya mwanajeshi mmoja wa kijerumani alimrushia bomu ambalo lilimlipukia Major na kumjeruhi sana ikiwemo kumtoa jicho la kushoto.
Baada ya kuwa ameng'olewa jicho alitakiwa kuondolewa kwenye uwanja wa vita na kurudishwa nyumbani lakini katika kitendo cha kishujaa na kizalendo bwana Major aligoma kurudi nyuma na inaelezwa kwamba baada ya mabishano ya muda mrefu alidai haitaji macho mawili ili aweze kutumia bunduki kumlenga adui kwenye sniper gun yake maana ikumbukwe jamaa alikuwa ni mdunguaji (sniper) hivyo aliona jicho moja linatosha kulenga shabaha na mwishowe akakubaliwa kuendelea kuwepo uwanja wa vita huko Ufaransa.
USHUJAA UHOLANZI
Jeshi la washirika (Allied ) lilipofika nchini uholanzi Leo Major alipewa kazi ya kwenda kutafuta taarifa za kiintelijensia kuhusu ngome za adui kwenye mji wa Schledt ila major hakuishia kwenye ujasusi tu bali alidhamiria kuyateketeza majeshi ya ujerumani akiwa peke yake!! Alisogea mpaka kwenye kambi ya kijerumani na kuanza kudungua mwanajeshi mmoja baada ya mwingine huku akibadilisha nafasi anapowalengea kiasi ikaonekana kama ni jeshi limevamia na sio mtu mmoja.
Wakati jeshi la Ujerumani likipanick alifanikiwa kumuwinda commander wa kikosi kile hapo kambini na kumteka ambapo alimpa sharti kuwa akubali surrender lasi hivyo ''vikosi'' vilivyozunguka kambi yake vitammaliza bila kujua "timbwili" lote hapo kambini lilisababishwa na mtu mmoja tu. Hivyo walisurrender kwa ujumla wao wanajeshi 93 wa Kijerumani na hata aliporudi kambini viongozi wake walipigwa na butwaa maana alitumwa kuleta taarifa za adui ila yeye sio tu alirudi na taarifa bali na maadui wenyewe. Kitendo hiki kilichukuliwa cha kishujaa sana hivyo alipewa medali ya juu ya ushujaa ''Distinguished conduct medal'' kwa sababu ya tukio hili.
USHUJAA #2
February 1943 wakiwa Uholanzi bado Leo major alikuwa anasaidiana na mwenzake kupakia miili ya wanajeshi waliofariki kwenye vita na mara baada ya kupakia miili hii wakawasha gari na kuondoka lakini ghafla ukatokea mlipuko wa bomu lililokanyagwa na gari yao hivyo likawajeruhi vibaya sana na aliponea ''chupuchupu'' kifo kwa mara nyingine.
Aliporudishwa kambini kwa ajili ya vipimo akaambiwa amevunjika mgongo mara 3, mbavu mara 4 na visigino vyote viwili hivyo akaambiwa kwa mara nyingine kuwa ushiriki wake kwenye vita umeishia hapo hivyo atarudishwa canada. Ila kabla hilo halijafanyika Major alifanikiwa kutoroka hapo kambini na kwenda mji wa Nijmegen ambako aliishi kwenye moja ya familia za Uholanzi na kupewa huduma za hapa na pale hata baada ya mwezi licha ya maumivu aliokuwa nayo hakukata tamaa na alirudi upya jeshini baada ya mwezi ingawa sijaona vyanzo vinavyoeleza aliwezaje kuruhusiwa kurudi jeshini akiwa na majeraha wala alikwepaje adhabu ya kutoroka jeshini.