Leo kumbukizi ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika, utaratibu upo vipi?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Tuliisha zowea sikukuu za kiserikali kutaarifiwa gharama ( pesa ) kuelekezwa kwenye miradi mingine sasa sherehe hii ya leo imekaaje?
 
Shujaa alikuwa TAPELI wa maneno tu, kuna sikukuu za kitaifa lazima zienziwe kwa utaratibu walioacha awamu zote zilizopita.
Yeye akajiona anao uchungu na nchi kuliko mtu yoyote yule, alikuwa MSHAMBA.
 
Kongamano la wasomi UDOM, Mgeni mwalikwa Makamu wa Rais, TBC live, watu wanajimwaga kwa hoja za kisomi. Hamna mauno ya akina Steve Nyerere. Now tunarudi kwenye mijadala, siyo ule upuuzi wa Jiwe na uoga wake wa hoja. Hadi Jafo leo anaongea points.
 
Utasikia wanataja Tanzania bara na Zanzibar!!

Lakini jina Tanganyika ni mfupa mgumu kwa viongozi!!
 
Upo hapo Chimwaga?
 
Tuliisha zowea sikukuu za kiserikali kutaarifiwa gharama ( pesa ) kuelekezwa kwenye miradi mingine sasa sherehe hii ya leo imekaaje?

Wazanzibar ndio muda wao wa kurekebisha kero zote za muungano au kuuvunja kama hamuutaki maana mkishindwa sasa hivi kuja kupata rais wa jamhuri 100% mzanzibar ni ngumu labda itokee kama ya MEKO.
 
Tazama TBC1 LIVE sasa hivi....

Viongozi wenyewe wa serikali wamejiandalia kitu kinaitwa "KONGAMANO LA MIAKA 57 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR" kujadili mafanikio na changamoto za muungano huu..

Mgeni rasmi ni VP - Dr Mpango Isdori Philip..

Watoa mada pamoja na wengine ni Prof. Palamagamba Kabudi..

Sina tatizo na kongamano hili kwa jina la "Kongamano"...

Tatizo langu ni kuwa, hili haliwezi kuwa kongamano huru bali ni kusanyiko la viongozi wa CCM kupongezana kupeana kitakachoitwa " MAFANIKIO YA MUUNGANO" bila kugusa changamoto...

Pamoja na kuwa wapo waalikwa wengine wakiwemo viongozi wa dini, wanafunzi wa vyuo vikuu na raia wengine, mtu asitegemee kusikia zikitajwa changamoto za muungano huu...

Binafsi ningependa taasisi huru kabisa ingeandaa kongamano kama hili na kualika watu wote waje wajadili kwa Uhuru mafanikio ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na bila kusahau changamoto za muungano huu pamoja na kupendekeza hatua za kuchukua...

Lakini kwa mtindo huu, ni kuendeleza utamaduni uleule wa miaka yote wa kushindwa kuwa wawazi na kuendelea kujifariji kuwa mambo yako shwari huku ukweli kuwa mambo siyo shwari kivile...

Wahenga walisema hivi "mficha uchi hazai". Na wengine wakasema, "afichae maradhi mauti humuumbua..."
 
Utasikia wanataja Tanzania bara na Zanzibar!!

Lakini jina Tanganyika ni mfupa mgumu kwa viongozi!!
Hata mie huwasangaa mno. Jina Tanzania ikilinyambua ni TANganyika na ZANzibar hiyo IA mdosi aliiongezea tu kuliboresha.
 
Tazama TBC1 LIVE sasa hivi....

Viongozi wenyewe wa serikali wamejiandalia kitu kinaitwa "KONGAMANO LA MIAKA 57 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR" kujadili mafanikio na changamoto za muungano huu..

Mgeni rasmi ni VP - Dr Mpango Isdori Philip..

Watoa mada pamoja na wengine ni Prof. Palamagamba Kabudi..

Sina tatizo na kongamano hili kwa jina la "Kongamano"...

Tatizo langu ni kuwa, hili haliwezi kuwa kongamano huru bali ni kusanyiko la viongozi wa CCM kupongezana kupeana kitakachoitwa " MAFANIKIO YA MUUNGANO" bila kugusa changamoto...

Pamoja na kuwa wapo waalikwa wengine wakiwemo viongozi wa dini, wanafunzi wa vyuo vikuu na raia wengine, mtu asitegemee kusikia zikitajwa changamoto za muungano huu...

Binafsi ningependa taasisi huru kabisa ingeandaa kongamano kama hili na kualika watu wote waje wajadili kwa Uhuru mafanikio ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na bila kusahau changamoto za muungano huu pamoja na kupendekeza hatua za kuchukua...

Lakini kwa mtindo huu, ni kuendeleza utamaduni uleule wa miaka yote wa kushindwa kuwa wawazi na kuendelea kujifariji kuwa mambo yako shwari huku ukweli kuwa mambo siyo shwari kivile...

Wahenga walisema hivi "mficha uchi hazai". Na wengine wakasema, "afichae maradhi mauti humuumbua..."
Ahsante, nipo moja kwa moja mkuu.
 
Tuliisha zowea sikukuu za kiserikali kutaarifiwa gharama ( pesa ) kuelekezwa kwenye miradi mingine sasa sherehe hii ya leo imekaaje?
Alikuwa mwizi tu huyu mwendazake. Hela alikuwa anazipiga na kijengea Chato. Tena nachukia Sana ukiongelea Mambo ya mwendazake.
 
Back
Top Bottom