Leo Kisonge wamepatia Kweli kuandika kuwa kunguru hafugiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo Kisonge wamepatia Kweli kuandika kuwa kunguru hafugiki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Aug 25, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KWA zaidi ya wiki mbili,Maskani ya Kisonge, Ungujailiweka bango linalosema kuwa"Kunguru hafugiki."

  "Swadakta, Kisonge safarihii wamesema kweli kabisa,Wazanzibari hawataki mtamawa kurushiwa ndani ya kibandawakiwa wamefungiwa, wanatakakupumua, kama alivyosema MzeeKarume kwamba Wazanzibariwanataka uhuru wa kujitawalawenyewe.

  "Amesema mwananchi mmoja baada ya kusoma bango hilo laKisonge wiki iliyopita.Hata hivyo, baadhi ya watuwameanza kujiuliza nini hatmaya vuguvugu na mchakato huuwa kutaka Zanzibar huru hukuwengine wakitafsiri hali hiyokuwa ni kuwa na muungano wakimkataba.

  Katika mazungumzo yakena wandishi wa habari sikukadhaa zilizopita, MzeeHassan Nassoro Moyoalisema kuwa haamini kuwaMzee Aboud Jumbe alikuwahakukosea alipopigania hakiya Zanzibar na mamlaka yakekatika muungano. Alisema kuwa Mzee Jumbealikuwa na maoni kuwa kuwena "Serikali tatu, ndio vuruguzikatokea na kudaiwa anatakakuvunja Muungano maana ndiomatatizo yetu hayo."Hata hivyo Mzee Moyoakasema kuwa yeye haoni kuwaJumbe alikuwa na makosa. Kwakauli yake alisema:"Mimi nasema Aboud hakuwana kosa, na yeye yupo hai nasina wasiwasi na ninayo yasemasimsingizii.

  "Lakini pamoja na imanihiyo kuwa Mzee Aboud Jumbehakuwa na kosa, Mzee Moyoalieleza pia kuwa hiyo haikuwasababu ya kunusurika."Ndiyo hivyo tena likaendalikapasuka kule, kwa hiyo (MzeeAboud Jumbe) hakupata msaadawa watu, kina Moyo wakakaakimya tu hivi hivi, na walewaliokuwa wakimsaidia kule, Nyerere akawatia ndani wote."Watu wanajiuliza, Je,Mheshimiwa Jakaya MrishoKikwete akiwa kavaa kofia kamazilezile za Mwalimu Nyerere,kwa maana ya Rais wa Nchina Mwenyekiti wa CCM, nayeatafuata nyayo za Nyerere kwakuwachukulia hatua wazeewapigania Uhuru wa Zanzibar nawanamapinduzi wanaotaka sasaZanzibar iachiwe ipumue?Je, nini itakuwa hatma yawazee kama Mzee Hassan Nassoro Moyo wanaosema wazikuwa wanataka muungano wamkataba?

  Je, nini itakuwa hatma ya walewanaomuunga mkono ambaowapo tayari kurejesha kadiza CCM kama itakuwa ndiyogharama ya kutetea uhuru naDola kamili ya Zanzibar?Wakati Mzee Aboud Jumbeanasulubiwa Dodoma mwaka1984, tunaambiwa kuwa "kinaMoyo walikaa kimya tu hivihivi."Leo miaka 28 baadae hojazilezile za Aboud Jumbekudai haki ya Zanzibar katikamuungano zimeibuka kwa nguvuna kwa uwazi zaidi.Je, wakati makomredi, makadana waasisi akina Mzee Moyowanapaza sauti, yakiwakutahali itakuwa ileile ya viongoziwengine na umma kukaa kimyatu hivi hivi?Baada ya utangulizi huu,ifuatayo ni sehemu ya mwisho yamaelezo ya Mzee Hassan Nassor Moyo alipokutana na wandishiwa habari hivi karibuni katikaHoteli ya Bwawani, Zanzibar.

  Aboud Jumbe hakukosea

  "Sasa nije katika kisa chaAboud Jumbe, mi nasemahakufanya makosa, maanayeye alikuwa akizungumza kilekifungu ambacho kinasemakutakuwa na Serikali mbili, mojani ya Zanzibar itakayoshughulikiamambo ambayo siyo yaMuungano na moja ya Muunganoambayo itashughulikia mambo yaMuungano, na pia itashughulikiamambo ya Tanganyika ambayosiyo ya Muungano.Aboud akafasiri mambo hayaya Muungano na mengine yaTanganyika, kwa hiyo tuwena Serikali tatu, ndio vuruguzikatokea na kudaiwa anatakakuvunja Muungano maana ndiomatatizo yetu hayo.

  Mimi nasemaAboud hakuwa na kosa, na yeyeyupo hai na sina wasiwasi naninayo yasema simsingizii, nivile tu alilichukua suala hilikama lake yeye na RamadhaniHaji Waziri Kiongozi, baadalaya kuwashirikisha wenzao waBaraza la Mapinduzi na hililinawezekana maana alikuwakiongozi wetu. Ndiyo hivyo tena likaendalikapasuka kule, kwa hiyohakupata msaada wa watu, kinaMoyo wakakaa kimya tu hivi hivi,na wale waliokuwa wakimsaidiakule, Nyerere akawatia ndaniwote.
  Inaendelea Uk. 4
   
   
  Inatoka Uk. 3
  Bahati mbaya sana, kilalinalofanywa jambo ambalo sila Muungano likafanywa ni laMuungano, basi ni kudhalilishaupande wa Muungano ambao niwa Zanzibar.Mfano ushirikiano wakimataifa, halikuwa ni jambola Muungano katika hapawakaliongeza la Ushirikianowa kimataiafa, hilo limeingiakinyemela tu, kwa sababu hiyohata Rais wetu akienda Nairobihapo hawezi kutia hata sainikununua unga wa ngano, hawezimpaka ruhusa ipatikane Bara.

  Hoja za Vijana zisikilizwe

  Mambo haya ndio katikamatatizo ya Muungano. Lingineni kwamba Mzee ile siku ya Chai,aliwambia vijana wote wote walewaliokuwa YASU, kwa kuwasisi hatutaki uhuru wa elimu baliuhuru wa kujitawala wenyewe,nyinyi ndio mtakaosoma.Tumepata Serikali yaMapinduzi vijana wetutumewasomesha, wameelimikatunao wengi hapa, hata kazihatuna za kuwapa. Na haowaliokuwa ndani ya Serikalikwa kuwa wote wamesoma, sasaule mkataba ambao tulitia saini,ninao mie hapa, hii ni nakala yamkataba halisi uliotiwa saini, naKurume na Nyerere.Sasa vijana wetu hawawaliosoma wameusomahuu mkataba, leo wanakujawanamwambia Mzee Hassan Nasoro Moyo, wewe umetiasaini Mkataba huu, mbona komahii hapa imewekwa mahalisipo?

  Mbona sentesi hii imekaasipo? Waniambia mimi Mzeewao ambao nilitia mimi sainimkataba, baada ya mika 48, nawameshaona mambo yoote yamatatizo ya hapa na pale tokeakuingia katika Muungano.Hawa vijana nimewafundishamimi wameelimika wanajuasasa wanaona makosa wanasematubadilishe, tubadilike hawasemihawataki Muungano hapana,wataukataa Muungano tu kamahauendi sawa sawa.Mzee Karume alisema,Muungano wetu sio sheria,Muungano wetu sio wa katiba,Muungano wetu sawa sawana Boti, maana yake nini,kwamba kuna siku boti linawezakuteteleka hali alitoa mfano wanguo, kwamba Koti likikubanavua.

  CCM imekuja baada yaMuungano

  Sasa vija ndiyo lugha hiyowanayosema wanataka kuonaMuungano unaoendana nawakati wao, ugomvi uko wapi.Sasa ukisikia watu wanasematunakwenda kinyume na sera yaCCM, nataka nikuambieni kitukimoja sera ya CCM, imekuja baada ya Muungano wa vyamamwaka 1977.Huu ni Muunagano wa nchi,mimi nimezaliwa mwaka 1933,nimeikuta nchi tayari hapasikukuta Muungano, sikukutaChama, sasa leo kwa ninitusizungumze Muungano.Kwa hiyo vijana hawawanapotaka Muunganoubadilike wanataka Muunganowa mkataba wana haki si ndowanafikiri hivyo, mtawazuiahata kusema wasiseme? Sera yaCCM, imekuja kuunga mkonouamuzi wa Serikali zao, leowanakuja kutaka kuligeuza tufatewanavyotaka wao, haiwezekani,hatuwezi kuchanganya mamboya Chama na nchi.

  Nchi ni mali yetu sisi wananchi,kwa hiyo tusichanganye mambohaya mawili kwa wakatimmoja. Chama ni Chama,kinaweza kuondoka, sasa leotumeunganisha nchi mimi natakakuzungumzia nchi, unaniambianakwenda kinyume na sera zaChama, ala.Mimi niwaombe viongoziwetu wa CCM watuachietuzungumzie nchi yetu, mimikama mtaniambia nakwendakinyume na sera, ahlanwasah'alan, mimi nipo katikamsimamo uleule, mimi nimkereketwa wa CCM safi kabisasiwezi kupinga Muungano hatamara moja lakini nasema bilakificho, bila kificho lazimaMuungano tuubadilishe,hatuwezi kwenda nao hivi, hiliwala silionei haya kwa sababuni haki yangu. Nilichotaka kusema ni hichokwamba tuzidi kuelewanakwamba tulikotoka ni huko natunakotaka kwenda tuwe nanchi nzuri tuwe na MuunganoMzuri kabisa na tuzungumzemazungumzo haya hukumnakunywa soda, kahawa kamawazee wetu ndio walifanyahivyo, bila ugomvi, bila vitishondio walifika hapa.

  Na sisi wengine ambao niwazee ambao akili zetu zinafanyakazi tunasema hivyo, kweliinafaa tukae kitako Muunganohuu tuuangalie isiwe tu huuinatosha, miaka 48, inatoshakukaa kitako na kuungalia.

  Muungano kwanzaKatiba ije baadae

  Mimi natofautiana kitu kimojatu, huwezi ukafanya jambo lamwanzo ukalifanya kuwa lamwisho, nimefurahi kusikiaTume ya Warioba kwambaatapokea mambo ya Muungano,lakini kupokea haimo katikahadidu rejea.Kwa hiyo ni muhimu sanakwa Serikali yetu kuliona hilokwamba tusichuke jambo lamwisho kuliweka mwanzo.Karume na Nyerere kwanzawalizungumza Muungano,ndio likaja je Muungano huoutashughulikia mambo ganindiyo hayo 11, la pili hilo. JeeMuungano huo utashughulikaKatiba gani ya Tanganyika yamuda si la tatu hilo.Sasa tusichukue jambo latatu la mwisho tukalifanyala mwanzo, unatengenezaKatiba unamtengenezea nani,unatengenezea madogoli?

  Auunatengenezea Muungano, sasatuzungumzie Muungano kwanzatunataka Muungano gani, hii nihaki yetu wala tusiogope, kwanini tuzungumze Katiba kablaya Muungano.Mimi nafikiri mabadilikoya Muungano hayana budikufanyika. Pili nasemaMuungano usiwe katika namnahii. Tatu Muungano bwanatushauri uwe wa mkataba. Nnekila nchi iwe na vyake. Tanokuwepo na mambo maalum yakushirikiana.Sita tusifungike, kwa mamboambayo tunazungumza kwambatusizungumze mambo ya zamani.Saba tukubali mabadiiko. Nane,mawazo haya ambayo watuwanayatoa ya kutaka mabadilikoyasije kufasiliwa kuwa tunatakakuvunja Muungano, laa. Lengoni kuutengeneza Muungano,ambao utakidhi haja kwa nchizote mbili.

  Nane na Tisa, huko tulikotokatulikubaliana uzuri sana kwakucheka kwa furaha, sasanadhani tukizungumza swalahili kwa kucheka na vigeregere,kusiwe na ghadhabu tutafika.Baada ya hayo nashukurukwa kunisikiliza, nadhaninimejitahidi kukusaidieni kwa jambo hili la Muungano, asantenisana."

  (Mzee Hassan NassorMoyo-Mwandishi aliyetiamazungumzo yake katikamaandishi ni BakariMwakangale)
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Weka paragraph............Ukiweka hivyo inachosha kusoma
   
 3. S

  Safhat JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!kichwa kinauma kwa kusoma gazeti.subiri nkatafute action kwanza nimeze.ntapta badae.
   
 4. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  wallah nimeshindwa kusoma, JF bana!!!
   
 5. M

  Mbofu JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muungano wa mkataba wa nin,c wajitoe tu jamani! Mi nataman tar 31,dec,2012 tuwe tmeshajitenga.
   
 6. Eddie8

  Eddie8 Senior Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huu muungano tokea tarehe 26/4/1964 una manung'uniko hadi leo hivi watanganyika wanang'ang'ania nini katika muungano huu . Tuwacheni tupumue.
   
 7. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nitarudi baadaye kwani nikisoma nashindwa kuelewa JF si mahala pa kuweka kitabu
   
Loading...