Leo imetimia miaka 50 yangu kuuawa kwa mwanaharakati wa haki za weusi Marekani, Martin Luther King Junior.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Habari za pilika wadau wa JF.

Leo ni miaka 50 tangu kuuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mmarekani mweusi Martin Luther na kundi la wazungu waliochukia harakati zake za kupigania haki za weusi.

Aliuwawa tarehe 04/04/1968. Anakumbukwa kwa hotuba yake maarufu ya I have a dream yaani nina ndoto.
 
Kwa hio hii inatuhusu nini Wabongo? Au inatufunza nini?
Inatufunza kupaza sauti hata kama watawala hawataki, hawapendi, na hata kama wakitunga sheria kandamizi tusijunali. Ni bora kufa kwa kutetea haki na utaishi milele, kuliko kunyenyekea udhalimu ukafa kimoja na usikumbukwe hata na family yako.
 
Utakumbukwa si kwa magari, majumba wala hela ulizoacha bali ni jinsi gani Maisha yako yaliwagusa watu.

Martin ni miongoni mwa wanaharakati wengi walioishi kwa muda mchache sana Duniani ila wameacha legacy kubwa sana Duniani. Pamoja na kuwa inasemakana aliuwawa kwa maagizo ya FBI chini ya Murugenzi katili John Edgar Hoover miaka 50 iliyopita lakini amebakia kuwa mtu mashuhuri na maarufu sana na unaweza ukasema amefariki jana tu.

Pumzika kwa amani Komredi.
58794d07f10a9a51098b848b-1136-852.png
 
Anakumbukwa na atazidi kukumbukwa sana
 
Inatufunza kupaza sauti hata kama watawala hawataki, hawapendi, na hata kama wakitunga sheria kandamizi tusijunali. Ni bora kufa kwa kutetea haki na utaishi milele, kuliko kunyenyekea udhalimu ukafa kimoja na usikumbukwe hata na family yako.
Umejibu vyema
 
Habari za pilika wadau wa JF.

Leo ni miaka 50 tangu kuuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mmarekani mweusi Martin Luther na kundi la wazungu waliochukia harakati zake za kupigania haki za weusi.

Aliuwawa tarehe 04/04/1968. Anakumbukwa kwa hotuba yake maarufu ya I have a dream yaani nina ndoto.

Huwa namkubali sana huyu ndugu. Speech yake ya "I HAVE A DREAM" ni hii hapa;

VIDEO

PDF
 
Attachments

  • I Have a Dream Speech.pdf
    1.5 MB · Views: 20
Back
Top Bottom