Leo huenda ikawa siyo siku nzuri kwa Rais wa TFF Malinzi kwani Mapacha hawa kuchukua Fomu rasmi

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Katika kile kinachoonyesha kwamba Watanzania hasa wapenda Soka / Kandanda wamechoka na Uongozi / Utawala wa sasa wa Rais wa TFF Jamal Malinzi hatimaye leo asubuhi mida ya Saa 5 Viongozi wanaotakiwa kuiongoza TFF wanachukua Fomu rasmi ili kupambana na kumtoa Malinzi madarakani.

Na ili kuonyesha kuwa huenda hawa Watu wawili wakawa ni mwiba mchungu kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi ni kwamba wamepata baraka zote kutoka kwa Wadau wengi wa Soka nchini na hata Serikalini na kuna uwezekano mkubwa mno kwa jinsi mikakati yote ilivyopangwa huu ukawa ndiyo mwisho wa Jamal Malinzi ndani ya TFF.

Watu hao ni Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Yanga FC, Mchambuzi mahiri wa Soka, Mdau mkubwa wa Soka na Msomi mzuri wa masuala ya Biashara na Uongozi Ndugu Ally Mayai Tembele ambaye amepangwa kugombea nafasi ya Urais wa TFF na Makamu wake inasemekana amepangwa kuwa ni Mchezaji wa zamani wa Kiungo wa Simba SC na aliyekuwa na mafanikio makubwa, Mdau mkubwa wa masuala ya Soka na Kiongozi wa zamani wa TFF Mzee Mtemi Ramadhan.

Kinachowafanya hawa Watu akina Ally Mayai na Mzee Mtemi Ramadhan wakubalike na Wadau wengi wa Soka / Mpira nchini Tanzania ( GENTAMYCINE inclusive ) ni kwamba kwanza wamecheza mpira katika Kiwango cha juu kabisa hivyo wanajua nini maana ya Soka na Maendeleo yake. Lakini pia hawa Watu wawili ni kweli kuwa mmoja wapo ni mwana Yanga na mwingine ni mwana Simba ila uzuri wao ni kwamba huwa hawana Unafiki na hawatangulizi mapenzi kwa hivyo Vilabu vyao pindi vinapokuwa na matatizo bali wao husimamia Ueledi na Ukweli hasa katika Utendaji wao.

Watoto wa mjini tunasema kwa Kauli mbiu yetu mpya isemayo “ Malinzi pisha njia wenye Mpira wao wamekuja “. Nianze tu kutoa pongezi zangu za dhati kwa hawa Wadau wangu wakubwa wa Soka Kaka yangu Ally Mayai Tembele na Mzee wangu Mtemi Ramadhan kwa kuamua kuwa Viongozi wa TFF na nina uhakika kama Wajumbe wa TFF wataacha Upopoma / Upumbavu wao basi Rais mpya wa TFF atakuwa ni Ndugu Ally Mayai Tembele na Makamu Rais mpya wa TFF ni Ndugu Mtemi Ramadhan.

Nami namalizia kwa kusema “ Malinzi pisha njia wenye mpira wao wamekuja “.

Nawasilisha.
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,389
2,000
Malinzi anamuhofia Athumani Nyamlani sio hao. Vita ilishaandaliwa na kupiganwa miaka miwili nyuma hapa ni kuenda kupandisha bendera.
Mpira una fitina sio kama watu wanavyojua. Kampeni zilishaanza kwenye chaguzi za mikoa na ndio maana migogoro mingi ilikuwepo kwenye chaguzi mikoani.
 

Mussolin5

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,421
2,000
Malinzi anamuhofia Athumani Nyamlani sio hao. Vita ilishaandaliwa na kupiganwa miaka miwili nyuma hapa ni kuenda kupandisha bendera.
Mpira una fitina sio kama watu wanavyojua. Kampeni zilishaanza kwenye chaguzi za mikoa na ndio maana migogoro mingi ilikuwepo kwenye chaguzi mikoani.
Sidhani kama umemuelewa Komredi GENTAMYCINE vizuri.

Labda nikuibie tu siri, nyuma ya Ally Mayai wapo watu wengi sana na wenye nguvu ya ushawishi. Mmoja wapo ni Mbunge na mtoto wa Rais wa zamani.

Nitarudi baadae!
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,919
2,000
Malinzi anamuhofia Athumani Nyamlani sio hao. Vita ilishaandaliwa na kupiganwa miaka miwili nyuma hapa ni kuenda kupandisha bendera.
Mpira una fitina sio kama watu wanavyojua. Kampeni zilishaanza kwenye chaguzi za mikoa na ndio maana migogoro mingi ilikuwepo kwenye chaguzi mikoani.
Huyo Nyamlani ana lipi la kujisifia alilolifanya kama kiongozi. Kama uchaguzi uliopita alipigwa upper cut ndio huu atashinda?

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom