Leo hii waajiriwa wanakaa miezi kadhaa bila kupewa pesa ya kujikimu

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
2,926
3,054
Mimi niliajiriwa mwaka 2013 na nilipofika halmashauri (Kasulu) tulipewa pesa ya kujikimu palepale ndipo tukapelekwa vituoni.

Lakini leo hii waajiriwa wanakaa miezi kadhaa bila kupewa pesa ya kujikimu. Matokeo yake wanapigwa danadana na kuambiwa waombe ruhusa ya kurudi makwao mpaka pesa ya kujikimu itakapotoka.
Wengine wanaambiwa mfumo wa kulipa umegoma...n.k.

Mpaka leo waajiriwa wa julai hawajalipwa pesa ya kujikimu na wengi wao hawajapata mshahara.
Lakini serikali kila muda inajidai inajari watumishi.

Hivi ni kweli waziri wa TAMISEMI yupo serious?
 
Hicho kimama cha Tamisemi hakijisomi, yaani maneno mengi utendaji sifuri.
Waziri alijitapa mno wakati anatangaza ajira za hao vijana, wamefika vituoni wakurugenzi wamewatelekeza wanalia njaa na majibu wamatishiwa wakidai posho ya kujikimu.
Serikali hii ya Mama imejaa wazembe wengi
 
Back
Top Bottom