Leo hii ni Januari 2021, hivi gesi ya Mtwara imefikia wapi?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,114
35,118
Ni miaka isiyopungua tisa sasa toka sakata la uchimbaji wa gesi ya Mtwara lilipoibuka hapa Tanzania. Matumaini yalikuwa makubwa, mbwembwe kibao, nguvu ikatumika na watu kupoteza maisha ili gesi itoke Mtwara.

Kuna kitu mpaka sasa nimeshindwa kukielewa kuhusu gesi ya Mtwara, nacho ni Ukimya. Ukimya ni mkubwa na hakuna kiongozi yoyote wa serikali iliyopo madaraka na iliyopita inayejitokeza kulizungumzia. Na hakuna chombo chochote cha habari kinachotupa updates au kumbukumbu ya gesi ya Mtwara.

Nini kinaendelea kuhusu gesi ya Mtwara?
 
Watu wa gwara again walituambia kua hatuwezi kuitumia gesi yetu kwa uhuru kwa kua imeshatekwa na mabeberu
Yaliletwa mashtaka kwetu wadanganyika kuwa gesi si mali yetu tena, ilishachukulia na mabeberu zile dk za mwisho za lele mama, walopopitisha ule mswaada kwa dharula usiku kwa usiku mjengoni.

Ingawa mshtaki alikuwa miongoni mwao, hakuwa na la kufanya zaidi ya kutii agenda za kikundi.

Na kwakweli, tumeamua kwa dhati, maji yanakuwa mbadala, sitigila inakamilika, mwanga bwelele siku zijazo.
 
Tusibiri 2026. Utawala huu hauna interest na hayo mambo.

Bahati mbaya hili jambo ni time sensitive. Kadri siku zinavyoenda ndio mahitaji ya nishati zinazochafua mazingira yanavyopungua.

Hatujui tukianza kuuza gesi tutakuwa na muda wa kutosha kuuza mpaka iishe na kama tutauza bei yake itakuwaje mida hiyo.
 
Hili swala huwa linaniuma sana mkuu! Tulipotajiwa mita za ujazo trilioni ,52 tukashukuru Mungu kuuaga umasikini ndani ya miaka 10 iliyofuata. Lakini sasa mwaka wa 9 tunazidi kuwa wanyonge kwa kukamuliwa kodi za kila aina
 
Tayari makampuni ya uwekezaji yalijiandaa kuwekeza dola bilioni 30 kwenye mradi wa ujenzi wa LNG. Huu ungekuwa mradi mkubwa wa uwekezaji ambao haujawahi kuwepo katika kanda ya Afrika.

Alipoingia Kivuruge, kama kawaida, miradi yote iliyosainiwa na watangulizi wake, akasimamisha kwa madai kuna ufisadi. Kama alivyofanya kwenye SGR. Wenzake walisaini ungejengwa kwa dola dola bilioni 11, yeye mpaka Singida tayari ni bilioni 9. Kufika Mwanza utajengwa kwa dola bilioni ngapi? Na bado anawadanganya wajinga kuwa anapiga vita ufisadi. Wachina aliowakataa, sasa anawapigia magoti.

Wawekezaji wa gas waliamua kuondoka na kwenda kuwekeza Mozambique. Huko wanajenga LNG, ni uwekezaji wa dola bilioni 28, na ni uwekezaji wa pili kwa ukubwa Duniani kwenye sekta ya gas kwa mwaka 2020/2021.

Wameombwa sana kurudi lakini wamekataa. Muda wa karibu kabisa kuweza kufikiria kuwekeza tena Tanzania, wanasema ni baada ya miaka 5.

Kwa hiyo uchumi wa gas umeyeyuka. Nchi tajiri kabisa Duniani kwa kuzingatia wastani wa mapato ni Qatar. Kinachosababisha wawe matajiri hivyo, ni gas. Sheria yetu ya gas kabla ya 2016, ilikuwa ni copy and paste ya Qatar na Norway. Lakini jamaa akasema ni ya kifisadi. Kama Qatar na Norway, sheria hiyo hiyo imewatajirisha, inakuwaje ya kifisadi kwetu?

Kutafuta umaarufu kwa kisiasa kwa mtu mmoja kumeliletea hasara isiyoelezeka Taifa.

Kiongozi atakayefuata atakuwa na kazi kubwa ya kurekebisha mambo mengi ili kuirudisha nchi kwenye uchumi wa kisasa na kistaarabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom