Leo hii nashawishika kupingana na mitazamo ya watu wengine juu ya kiongozi wa CHADEMA Freeman Mbowe

Acha kujitekenya mkuu usihamishe magoli, hakuna asiyejua kuwa uliowataja hapo sio wapinzani na wala hatujawahi kuwasikia wakilalama kuhusu kuminywa kwa demokrasia.... hoja mezani ni Mbowe ambaye kama KUB anao wajibu kuonesha mfano na ikibidi kuwakemea hao wapinzani wenzake kama wapo.

Umemkejeli jamaa hapo juu eti senior nini bla blah, hata mimi nimejiunga jana basi labda wakongwe tu ndo wenye haki ya kukosoa.... jikite kwenye hoja acha madharau.
which urgument??? i can see from you poor analysis of thread based on post! lack of objectivity and particularity!

I have never seen any premissess to support urgument and you have reached wrong conclussion! being senior expert member means member has given accreditation.

You and the one whom you support you Will have very long journey and tiresome ,if you post thread of that nature. 😁😁😂😂
 
Kudadeeki ccm hamlali wala kula mkashiba kisa mh Mbowe.
1.Mmeharibu shamba lake la mazao ili kumkwamisha kiuchumi lkn mmenoa

2.Mmemnyang'anya sehemu ya kufanyia biashara zake pale billicanas....hakusalimu amri

3.Mmeuza vifaa vyake vya kutendea kazi haikufaa kitu

4.Mmemfungulia makesi kibao lkn bado hajasalimu amri .

Sasa naona mmeamua kuhamia mitandaoni kumnanga na kumchafua kwa wananchi na wananchama wa cdm lkn bado hamtafanikiwa.
Utakufa bure ukweli ni huo uliowasilishwa na mleta uzi na chadema wengine wanaunga mkono!
 
Tindo saa zingine huwa unanikonga sana, hapo umeusema ukweli bila kupindisha, hayo ndo mawazo mazuri ya kujenga, nadhani ni vyema chadema walifanyie kazi hilo.
Hata kama mleta uzi umeuleta uzi kinazi lakini una hoja za msingi. Mimi kama mimi naamini kiongozi yoyote hasa wa kiafrika akikaa madarakani zaidi ya miaka kumi, huishia kuharibu mazuri yake au kuishia kuvuruga mazuri yote aliyoyapata ndani ya hiyo miaka kumi ya mwanzo. Kimsingi Mbowe amefanya makubwa ndani ya cdn, lakini ameshavuka miaka kumi ya ubora wake, kinachoendelea sasa hivi ndani ya cdm ni yeye kuharibu yote mazuri aliyofanya. Ni vyema akae pembeni kiroho safi waingie wengine waendeleze alipoishia.
 
BAWACHA acheni kutetea mambo ya hovyo, Mbowe aoneshe kwa vitendo demokrasia anayoililia.... ni uroho wa madaraka.
Kuendelea kushikilia ofisi eti kisa hakuna mwingine mwenye SIFA ni dhahiri kuwa chama hakina watu makini, kwa mwendo huu ni vigumu kuaminisha raia kuwa CHADEMA ni chama na sio MALI ya Mtei & Co...!!
Pallangyo wewe!
 
Hata kama mleta uzi umeuleta uzi kinazi lakini una hoja za msingi. Mimi kama mimi naamini kiongozi yoyote hasa wa kiafrika akikaa madarakani zaidi ya miaka kumi, huishia kuharibu mazuri yake au kuishia kuvuruga mazuri yote aliyoyapata ndani ya hiyo miaka kumi ya mwanzo. Kimsingi Mbowe amefanya makubwa ndani ya cdn, lakini ameshavuka miaka kumi ya ubora wake, kinachoendelea sasa hivi ndani ya cdm ni yeye kuharibu yote mazuri aliyofanya. Ni vyema akae pembeni kiroho safi waingie wengine waendeleze alipoishia.
Uko sahiihi .
 
Utakufa bure ukweli ni huo uliowasilishwa na mleta uzi na chadema wengine wanaunga mkono!
Utaishia kuvalia manguo ya lumumba tu
tapatalk_1567627458569.jpeg
tapatalk_1567662891357.jpeg
 
Ndugu wanabodi ninachoeleza hapa ni uhuru wangu kifikra. Leo hii nashawishika kupingana na mitazamo ya watu wengine juu ya kiongozi wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Naomba ieleweke kwamba sikatai kwamba Mbowe amekuwa na mchango mkubwa katika kukiimarisha chama lakini huwa inatokea malaika akageuka kuwa shetani na kudumaza imani za waaamini.
Naomba niweke hapa kinachonifanya nimuone Mbowe kuwa kirusi na tatizo ndani ya CHADEMA na upinzani kiujumla.

1. Sababu ya kwanza ni uking'ang'anizi wa madaraka. Mwenyekiti Mbowe amekaa madarakani kwa muda mrefu mno kiasi kwamba itatuwia vigum kudhibit harakati za JPM kutaka kubadili katiba ili aendelee kubaki madarakani.Ikumbukwe kuwa Mbowe amekuwepo madarakani zaidi ya miaka kumi na hii inafanya CHADEMA kutokuwa mfano mzuri katika dhana nzima ya kupokezana madaraka.

2. Ujio wa Lowassa. Ninaamini kwa kiasi kikubwa kuwa Mbowe alitumia ushawishi wake kuhakikisha chama kinampokea Lowassa bila kujali athari ambazo chama kitazipata. Matokeo yake ujio wa Lowassa ukasababisha kuuwawa kwa ajenda kuu ya chama (UFISADI) na kuzalisha mamluki ndani ya chama kama wakina Mgeja.

3. Uteuzi wa katibu mkuu Mashinji. Haieleweki ni vigezo gani vilivyotumika kumpa nafasi ya ukatibu mkuu Dr. Vincent Mashinji. Chama kilihitaji mtu anayekijua , mtu anayefahamika katika mapambano ya demokrasia ili kuendeleza pale ambapo Dr Slaa aliishia. Wapo wakina Lissu, Mch Msigwa n.k lakini ajabu chini ya Mbowe Chama kikamleta Dr Mashinji na kimeendelea kumkingia kifua ilihali haifahamiki anafanya nimi ofisini. Inavyoonekana ni kama Mbowe alihakikisha anapatikania katibu mkuu ambaye hawezi kumzidi umaarufu.

4. Kushindwa kutoa mwongozo na kusimamia masuala muhimu ya wabunge wa chama. Tumeshuhudia baadhi ya wabunge wakipoteza ubunge wao kwa sababu za kitoto kabisa na Mbowe kama mwenyekiti ameshindwa kuonyesha ni namna gani chama kinashiriki kuwajengea uwezo wabunge wake. Mathalani Tukio la Nassari na Lissu.

Baada ya Lissu kushambuliwa ilitegemewa kwamba chama kitashika hatamu katika kushughulikia mambo yote muhimu ya kibunge ikiwemo kulitaarifu bunge kimaandishi kuhusu masuala yote yanyomhusu Lissu na ikiwezekana chama kuteua mbunge ambaye angesimama kama mfariji wa wana Singida mashariki kwa kuwasilisha kero zao bungeni.

Kwa kumalizia niseme kuwa pamoja na mchango mkubwa alioutoa Mbowe CHADEMA wakati umefika kwa yeye kukaa pembeni na kuwa mshauri tu wa chama vinginevyo ataendelea kukiua chama maana ni dhahiri uwezo wake kukiongoza chama umefika kikomo.
kama alivyo Pombe ndani ya ccm
 
CCM kingekuwa chama cha siasa na kikajitegemea kwa kujiendesha bila shaka yoyote kingekuwa hakipo kwenye ulingo wa siasa.

Shida iliyopo ni kuwa vyama vya pembeni vimejaa mamluki kutoka nje huko na kukosa kuaminika na wanaokiwezesha ccm kuendelea kusurvive hadi leo.

Nchi hii siku ikiamua kutenganisha siasa na dola wa kwanza kufa atakuwa Ccm.

Tuiombe Tanzania kama Taifa na nchi pia.
 
Back
Top Bottom