Leo Hii Lowassa ni Mbunge wa Arusha/Monduli Hadi Aruhusiwe Maandamano na Mikutano?

Ukiwa SISIEMU kila kitu Sawa Mkuu,Upinzani kazi ngumu Wengi wanakimbia....Only The Strong will survive -PALANAWE.
 
Mara hii mmeshasahau kuwa alikua Rais wa mioyo yenu ??
Hata Mungu alimtambua Lucifer kama malaika mkuu lakini sasa kwake ni Mwovu shetani. Jee utamuuliza Mwenyezi Mungu mara hii umesahau kuwa huyu ulimwita Malaika mkuu?
Ukipata jibu hapo tulia
 
Lowasa mabadiliko mabadiliko Lowasa sasa ametakata katakata hana hata chembe ya Ufisadi bali mfumo ndo ulifanya ila siye yeye, makamanda zungusha mikono na kiuno, Nafanya Nukuu tu 2015 baada ya gia kubadilishwa angani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa alikuwa mgombea urais hivyo ni ruksa kuwashukuru wapigakura milioni 6.Hata Rungwe ruksa kuzunguka kamanda.

Sent using Jamii Forums mobile app

Bonge la aibu, tumewaambia jiwe ndio anapandikiza chuki za kiitikadi nchi hii mmebaki kutokwa mishipa. Lowassa alikamatwa Geita alipotaka kushukuru wapiga kura, lakini alikamatwa kisa alikuwa cdm wakati huo. Sasa nadhani nchi nzima imejionea hizo amri haramu za rais. Na nyie watetezi mliokuwa mnaunga mkono amri za kipuuzi mmebaki kuongea uhanithi tu humu ndani.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Hii ni aibu kwa Rais aliyepiga marufuku maandamano na mikutano ya wanasiasa katika maeneo ambayo sio Wabunge hata wawe viongozi wa chama. Ni aibu kwa vile anaonekana Muongo kama anaruhusu Lowassa wamruhusu eti kwa vile kahamia ccm afanye atakavyo kinyume na agizo lake. Au agizo ni kwa viongozi wa vyama vya upinzani tuu?
Haiwezekani kumbe eti Rais anaonekana na muongo na mtoa maagizo sio kwa manufaa ya Taifa bali kundi la chama chake. Kumbe kauli ya Lissu kuwa tupende Taifa letu ila sio serikali ya KIZANDIKI KAMA HII YA CCM ni sahihi kabisa bila chenga.
Nasi wananchi itafika mahali kwa sababu wanatubagua tuwabague nao, tukiona wana fanya jambo hata kama la kitaifa na wakaingiza uchama wao tunasema kwenda kuleee na kususia.
Lowassa karuhusiwa kufanyiwa mapokezi na maandamano Arusha wakati viongozi wanakataliwa. AIBU KWAKO BABA JESKA
Kibaya ni kwamba saizi nchi inaongozwa kwa maagizo na sio sheria tena. Agizo huwa linawahusu watu flani tofauti na sheria ambayo inawahusu watu wote, ili agizo lilikua linawahusu wapinzani sio wanaccm.
Lowassa saizi karudi nyumbani ko agizo hilo alimuhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema sasa hawana wanachama wala washabiki watatoka viongozi tu kwenda kwenye maandamano. Chadema sasa wapo kwenye mitandao ya jamii tu wana akaunti kumi kumi kila mtandao na wengi wao wapo nje ya TZ wanabeba mabox mkuu. Hivyo ukiitisha maandamano utapata watu kiduchuuu watz wa kawaida wameshawachoka na ulaghai wao. Juzi umeona wabunge wao kule Morogoro wamakosa wa kuwawekea dhamana wakarudi mlupango hiyo tu ni dalili mbaya sana kwao.
Umekomenti kishabiki na hisia. Watu wanao wengi sana.
Mwambie aliyepiga marufuku aruhusu siku moja tu uone kama hata wale wa NYUMBA nyeupe hawatatoka barabarani. Nikuhakikishie kuwa watu wapo kuliko unavyofikiria,tatizo hakuna viongozi jasiri anayeweza amua hata kutoa uhai wake.
Viongozi wa upinzani hawapo tayari kwa hilo,ni maneno tu IPO siku IPO siku. IPO siku lini? Kwani kesho na kesho kuitwa siyo siku? Pumbafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilipoletwa thread kuwa lowasa atazunguka nchi nzima kuongea na wananchi.

Nilikomenti na kumshauri kuwa,ikitokea hivyo wapinzani ANZIENI hapo kufanya mikutano.
Lowasa akifanya arusha siku hiyo hiyo na muda huo huo ninyi fanyeni eneo lingine. AMINI NAWAAMBIA KAMA WANAAKILI HAWATAWAKAMATA. Kwani wakifanya hivyo mtakuwa na hoja yenye nguvu. Pia Jumuia za kimataifa zitaingilia kati.

ILI IOTE NI LAZIMA IFE.
Ili mbegu yoyote iote inapopandwa,nilazima ife ndipo iote.
MTALALAMIKA SANA,NA KUSEMA IPO SIKU,KAMA HAMTACHUKUA HATUA . Mungu hata shuka kuwaletea ukombozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wasio na akili hata ukiwashauri ni ngumu kuelewa wanachojua ni matusi tu ndo maana wanaitwa nyumbu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna kitu ambacho CDM na wapendahaki inatakiwa kubadilika ni kulalamika! Imeandikwa Jino kwa jino inatakiwa!
 
Chakaza wapinzani wa CCM wameruhusu haya yatokee bro. Hawajawa tayari kufia Imani na itikadi yao. Ikitokea hivyo serikali na CCM hawawezi kuwachezea wapinzani na kuwachokonoa machoni.

Lakini pia wanasiasa aina ya Lowassa ni wa kuogopwa. Amesahau kuwa kuna wananchi wameuawa, wamelemazwa, wamefungiwa biashara zao, wengine wameshushwa vyeo kwa ajili yake !!!!. Leo yeye pengine amerejeshewa gharama zake na kuahidiwa heshima kubwa, amesahau yote na wote walionitolea kufa kwa ajili yake. Wanavunja moyo na wakati mwingine kuwavuruga wananchi .


Alizuiliwa kuwashukuru wapiga kura akiwa upinzani. Lakini leo anaandaliwa maandamano sijui naye ni mbunge wa wapi ?!. JIBU NI KUWA KATIBA NI MBOVU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ulikua hufaham ni kuwa lowasa kwasasa hana shida na wahuni kama chadema tena. Aliwashauri mbadilishe aina ya siasa zenu mkakataa. Akagundua mliwahi mwita fisadi Tanzania nzima na kwaujingawenu mkamsafisha wenyewe sasa kaamua kurudi akiwa msafi kwani mlimtuhumu na kumsafisha wenyewe. Kaona home kumenoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema kaeni mtandaoni tu.siasa hamuwezi hamjawa tayari kuchukua nchi mngekuwa taasisi msingeuzà kiti cha rais kwa Lowasa. Lowasa kawapima akili zenu kagundua hamnazo bora arudi alikotoka

Sent using Jamii Forums mobile app

Angekuwa na akili angekamatwa na mgambo huko Geita alipoenda kusalimia wapiga kura wakati yuko cdm? Lowassa hawezi kufanya siasa nje ya vyombo vya dola kwani hakuwahi kufanya bila msaada wa dola.
 
Hii ni aibu kwa Rais aliyepiga marufuku maandamano na mikutano ya wanasiasa katika maeneo ambayo sio Wabunge hata wawe viongozi wa chama. Ni aibu kwa vile anaonekana Muongo kama anaruhusu Lowassa wamruhusu eti kwa vile kahamia ccm afanye atakavyo kinyume na agizo lake. Au agizo ni kwa viongozi wa vyama vya upinzani tuu?
Haiwezekani kumbe eti Rais anaonekana na muongo na mtoa maagizo sio kwa manufaa ya Taifa bali kundi la chama chake. Kumbe kauli ya Lissu kuwa tupende Taifa letu ila sio serikali ya KIZANDIKI KAMA HII YA CCM ni sahihi kabisa bila chenga.
Nasi wananchi itafika mahali kwa sababu wanatubagua tuwabague nao, tukiona wana fanya jambo hata kama la kitaifa na wakaingiza uchama wao tunasema kwenda kuleee na kususia.
Lowassa karuhusiwa kufanyiwa mapokezi na maandamano Arusha wakati viongozi wanakataliwa. AIBU KWAKO BABA JESKA
Lowassa ni rais wa mioyo yenu. Tangu lini rais akazuiliwa mikutano kuongea na raia wake?
 
Mikutano ya kutuambia nini? Acheni watu wafanye kazi. Lowasa ni mzee was ukoo huko Monduli na anapokelewa Kama hivyo. Kwanza ni mgonjwa hamtaki akapumzike kwake na wazee wenzake wampokee?

Kaanza uzee wiki iliyopita? Jiwe ana siasa za kishamba mno. Amegundua yuko chama analojia imebidi atumie nguvu kuhakikisha chama digital hakisikiki. Mtu kapata madaraka kwa kupiga pushup unategemea nini?
 
Kwa sinema za lowassa zilivyo ni za Kishamba anaweza kujamba au akala waandishi wa habari nao wakaifanya ni habari
Ana zile siasa za kudanya wale watu kijijini wasijua ulemwengu unaendaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ulikua hufaham ni kuwa lowasa kwasasa hana shida na wahuni kama chadema tena. Aliwashauri mbadilishe aina ya siasa zenu mkakataa. Akagundua mliwahi mwita fisadi Tanzania nzima na kwaujingawenu mkamsafisha wenyewe sasa kaamua kurudi akiwa msafi kwani mlimtuhumu na kumsafisha wenyewe. Kaona home kumenoga

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao unaowaita wahuni walimstiri alipotoswa na kudhalilishwa na CCM !!!. CCM ndiyo wahuni walipomwambia AMEJINYEA, Je watamtawaza sasa ?!.

Hao unaowaita wahuni imebidi Lubuva arekebishe mahesabu ili kuwadhulumu, kwa sababu hawana bunduki.

Hawa unaowaita wahuni ni waTz kama wengine na ni walipa kodi.

Ushauri wa Lowassa hauna nafasi ktk siasa za Africa na especially Tanzania . Uanaharakati ni muhimu. Pili Lowassa amefika bei ukizingatia ni mtu mzima sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom