Lengo la sisi kuwa hapa duniani ni nini?

Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!

Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?

Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??

Kwa nini tunazaa watoto?

Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??

Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???

Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?

Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??

NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?

Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!

Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?

JeTunaishi ili tufe???

Nini maana ya maisha???View attachment 1575137
Sasa mbona umeweka majibu yote hapo au hujaona hilo?
 
Soma kwa uelewa..usinilazimisheni nimjadili yeye wakati mimi nipo na wewe hapa.!

Kwani katika maisha ni lazima tutumikie kitu ili tuwe na furaha.?
Lazima nikuhoji sababu usiandike andike mambo ambayo huwezi kuthibitisha, wewe umesema Mola amedai, sada ndiyo uniambie amedai hili wapi ? Sasa usikwepe tatizo ulilolileta wewe.

Kama unajua upo na mimi kwanini unamuhusisha tena kwa mara nyingine tena kwa kumzulia uongo ? Sasa utaona kati yangu na wewe nani haelewi.
 
Umenikumbusha juzi nilimwambia mama moja anamiliki mgahawa kuwa hapa duniani hakuna haja ya kuzaa watoto maana anagalia wanapitia mapito unayoyapitia na mwisho wake ni kifo.

Yule mama kwa wakati ule aliniambia nimeanza kuchanganyikiwa nilipo rudi Jana take kunywa chai akaniambia ila jana umeongea point moja HV niliifikiria sana-kweli upo sahihi.

Leo nimeona Uzi wako utadhani ulikuwa kwenye ubongo wangu.
 
....hongera dada ndo mwanzo wa kujitambua uko...

Na ukishajua hilo utajiona tofauti sna...

Binadamu huwa tunajitoa ufahamu Sana kuhusu lengo letu la kuishi apa duniani, kuna watu hawataki ata kusikia hii mada sio tu kusoma....ipo sababu ya wao kufanya hvyo....

Lipo kundi la watu linafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linawapumbaza wanadamu wasijue lengo la uwepo wao apa dunia....na lipo kundi la watu linapambana kutaka watu wajitambue lengo la kuumbwa kwao japo hili kundi lapigwa vita Sana.

Kwaufupi lengo kuu la kuumbwa wanadamu na majini ni kumuabudu mola wao...na neno kumuabudu ni kumpwekesha yeye (kumtukuza na kumtegemea yeye) ktk kila kitu...

Dunia ni mapito....dunia ni njia...dunia ni kituo
Mwanadamu tunapitia vituo mbalimbali kila kituo kinaradha yake na machungu yake ila kituo cha mwsho inategemea na jinsi ulivyoishi kituo cha duniani...

Kituo 1:- maji yenye kuchupa (manii)
Kituo 2:-. Ndani ya matumbo ya mama zetu
Kituo 3:-. Duniani
Kituo 4:- Kaburini
Kituo 5:- Peponi au motoni inategemea na matendo yako ya duniani na huruma ya Muumba wako.

Maisha ya duniani ndo maisha ambayo yamebeba siri kubwa sana na hatma ya mwanadamu....na apa ndo tumepewa ule uwezo wa nguvu za kujicontrol....Ila baada na kabla ya apo ni out of our control ni amri tu ya Muumba wetu...

Mtu akifa hazikwi na yale aliyoyachuma isipokuwa matendo yake tuu...
Sasa Mungu anapata faida gani kuabudiwa na mwanadamu?? ana pungukiwa na nini asipo abudiwa??.hizi hoja zako zimekaa ki imani za kidini na hazithibitiki.
 
Sasa Mungu anapata faida gani kuabudiwa na mwanadamu?? ana pungukiwa na nini asipo abudiwa??.hizi hoja zako zimekaa ki imani za kidini na hazithibitiki.
Labda hujui maana ya kuabudiwa...

Hii inajumlisha sheria zote ambazo ameziweka ili wanadamu wazifuata...kwanini tuzifuate?

Hii ni kawaida kwa sababu yeye ndiye alietuumba na kuiumba hii dunia.....ni sawa na mfano wa machine au simu lazime kwa alieitengeneza aweke utaratibu wa kukitumia hcho kifaa na endapo utaenda against na utaratbu uliowekwa kuna risks zinaweza kutokea atimaye kuharibu kifaa.

Natumia hoja ya kiimani coz adi leo hii sayansi haijathibitisha asili ya dunia na uumbaji wake.
 
Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!

Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?

Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??

Kwa nini tunazaa watoto?

Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??

Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???

Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?

Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??

NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?

Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!

Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?

JeTunaishi ili tufe???

Nini maana ya maisha???View attachment 1575137
Hata kuku anajiuliza hivo hivo...ila mfugajj ndio mwenye jibu

Same kwa mungu..jiweke wewe position ya kuku na mungu mfanye ndio mfugaj..

So jibu la faida ya kufuga kuku analo mfugaj na sio kuku.
 
Dah mi mwenyewe huwaga nachoka hapo tu,nahangaika ili nipate kitu cha kula leo na kuweka akiba ya kesho na ukisema ukae tu bila kuls chochote unakufa njaa!sasa sijui lengo letu hapa duniani ni kula tu?maana yote wanayosema ndio lengo la kuletwa duniani ukiyaacha kuyafanya haufi sasa acha kula kama week nenda kasali uone.
Kweli kabisa yaani! Lakini hata ukila pia unakufa vile vile dahh
 
Back
Top Bottom