Lengo la Serikali ya CCM ni kuona Mbowe akisalimu amri na kuomba msamaha kwa Kesi ya ugaidi inayomkabili?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Tulishuhudia hapo majuzi, Jaji Tigana akifanya uamuzi ambao umekuwa kinyume cha matarajio ya mamilioni ya watanzania, kuhusu Kesi ndogo inayohusu Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema na wenzake 2 ya kutaka kuchoma moto vituo vya mafuta na kutaka kupanga njama za kutaka kuwadhuru baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali hii ya awamu ya 6.

Kwa kuwa Kesi hiyo inafuatiliwa kwa karibu Sana na watanzania walio wengi na Jumuiya za kimataifa, watu wengi walidhani kuwa maamuzi ya Jaji Tigana, yatakuwa ya haki na kuyatupilia mbali madai ya mashitaka ya Jamhuri na kuachiliwa watuhumiwa wote.

Hata hivyo watanzania hao walishikwa na mshtuko baada ya kusikia maamuzi hayo ya Jaji Tigana!

Kwa waliofuatilia Kesi hiyo kwa muda wote wa miezi kadhaa tokea ianze, walishuhudia mashahidi wa Jamhuri namna walivyokuwa "wakihenyeshwa" kwa maswali magumu na jopo la mawakili wa utetezi, wakiongozwa na wakili msomi Kibatala, hadi baadhi yao kushindwa kuhimili vishindo hivyo na kupata homa za ghafla, hadi wengine kulazimika kukimbizwa hospitali kupata matibabu!

Lakini pamoja na mtiririko huo wa mwenendo wa Kesi, Jaji Tigana akaamua "kuziba masikio" na kuamua kuwa kina Mbowe Wana Kesi ya kujibu Katika Kesi hiyo ya ugaidi na hivyo wanatakiwa kuanzia tarehe 4 mwezi ujao waanze kijitetea wenyewe.

Ndipo hapo ninajiuliza hivi Mahakama kusema kuwa ni lazima Katika Kesi za jinai, kuwepo ushahidi usiokuwa na shaka yoyote Ili kumtia hatiani mtuhumiwa, hivi Katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa Jamhuri, ni kweli kuwa walitoa ushahidi usio na mashaka yoyote?

Hivi unadhani ni nini kilichokuwa kikisababisha baadhi ya mashahidi, kushikwa na homa za ghafla hadi kulazimika kukimbizwa hospitalini??

Hiyo haitokani na hao mashahidi, kuunga unga ushahidi wao na hivyo kufanya kuwa penye ukweli, uongo hujitenga??

Ndipo hapo ninadhani kuwa watawala wetu ingawa nafsi zao zinawasuta Sana kutokana na mateso ambayo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake 2 wanayapata kwa kusota rumande kwa zaidi ya siku 250, lakini wanachotaka wao ni kuwa Mbowe asalimu amri na kuomba msamaha Ili atoke jela.

Kwa hilo watawala wetu watasubiri Sana, kwani mategemeo yao ya kuwa Mbowe ataomba msamaha na hivyo kuhalalisha wao watawala watembeze propaganda yao kuwa chama cha Chadema ni cha kigaidi na hivyo kamwe Mbowe hataomba msamaha kama watawala wetu wanavyofikiria na atahakikisha kuwa anaendelea kukaa rumande hadi hatimaye haki itendeke Katika Kesi hiyo na kumwachia huru.

NO RETREAT NO SURRENDER
 
Kwa hilo watawala wetu watasubiri Sana, kwani mategemeo yao ya kuwa Mbowe ataomba msamaha na hivyo kuhalalisha wao watawala watenbeze propaganda yao kuwa chama cha Chadema ni cha kigaidi na hivyo kamwe Mbowe hataomba msamaha kama watawala wetu wanavyofikiria na atahakikisha kuwa anaendelea kukaa rumande hatimaye haki itendeke Katika Kesi hiyo na kumwachia huru.

NO RETREAT NO SURRENDER
 
Screenshot_20220222-001006.jpg
 
Kama shujaa Mandela alihukumiwa kifungo cha Maisha jela, kwa makosa ya kubambika ya uhaini.

Hatimaye akatoka jela baada ya kutumikia miaka 27 na akawa mwafrika wa kwanza mweusi kuwa Rais wa Afrika Kusini.

Kwa hiyo kuna ajabu gani kwa Mbowe kuendelea kusota rumande kwa makosa ya michongo, hadi pale atakapohakikisha kuwa Haki imetendeka?
 
Chief labda anaona aibu kuifuta kesi sababu alishamezeshwa matango pori akajikuta ameyatapika kwa salim BBC dunia ikayaskiza, au ni malengo yake tu aisumbue CDM kutoka na homa ya 2025 alonayo......anaujua ukweli ulivyo wakifanya uchaguzi wa haki
 
Chief labda anaona aibu kuifuta kesi sababu alishamezeshwa matango pori akajikuta ameyatapika kwa salim BBC dunia ikayaskiza, au ni malengo yake tu aisumbue CDM kutoka na homa ya 2025 alonayo......anaujua ukweli ulivyo wakifanya uchaguzi wa haki
Haya yote yanatokana na mapungufu makubwa yaliyopo kwenye Katiba yetu, hivyo Katiba mpya tunapaswa watanzania wote tuipiganie kwa kufa na kupona
 
Kuna aliyesema serikali ya CCM na viongozi wake wanatuona . ni wajinga. Sasa Nape kusema kuwa bei ya vifurushi haina matatizo bali watu hawajui kutumia simu. Wengine wanawapa simu watoto wao wanamaliza bundle.
Mungu wangu
 
HILO HALITATOKEA wafanye Wafanyavyo ila MUNGU ATAJIBU MAPIGO kwa UONEVU HUU MUNGU Siku zote yupo Upande wa HAKI kuna LAANA INATAFUTWA
 
Kama shujaa Mandela alihukumiwa kifungo cha Maisha jela, kwa makosa ya kubambika ya uhaini.

Hatimaye akatoka jela baada ya kutumikia miaka 27 na akawa mwafrika wa kwanza mweusi kuwa Rais wa Afrika Kusini.

Kwa hiyo kuna ajabu gani kwa Mbowe kuendelea kusota rumande kwa makosa ya michongo, hadi pale atakapohakikisha kuwa Haki imetendeka?
Historia haijirudii
 
Back
Top Bottom