3 Angels message
JF-Expert Member
- Aug 3, 2017
- 4,890
- 13,626
Serikali kupitia kwa waziri wake wa Nishati Mh Makamba ilitoa taarifa kwa umma kuwa kutokana na uhaba wa mafuta ambao ulipelekea nishati hiyo kupanda bei ilitarajia kutoa ruzuku ya bilioni 100 ili kupunguza athari ambazo zilitokana na kupanda kwa bei ya mafuta kama bei za usafiri, bei za bidhaa nk
Taarifa ya waziri ilikuwa wazi kuwa ruzuku hiyo ingelikuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao ni wa 6 pekee na kweli mwanzoni mwa mwezi huu ahadi hiyo ilitimia
Jambo ambalo ndiyo hoja ya uzi huu ni nini athari za ruzuku hiyo ambayo serikali imetoa ili hali mambo yako vilevile wakati wa bei ilivyopanda? Bei zilizotangazwa za nauli na Latra mbona bado zipo vilevile hata baada ya kutolewa kwa ruzuku? Bei za bidhaa nazo mbona zimebaki vilevile pia? Lengo la serikali lilikuwa kupunguza makali kwa wafanyabiashara peke yao tu na siyo kwa wananchi?
Au wafanyabiashara wameamua kuigomea serikali kutoshusha bei, au mamlaka husika zimeamua kuwa upande wa wafanyabiashara, waziri husika haoni pia?
Maana hata kwa akili ya kawaida tulitarajia kupungua hata kwa sh 10 tu lkn mpk leo tunaenda katikati ya mwezi hatusikii cha Latra kupunguza bei wala yeyote mambo yako vilevile shida iko wapi?