G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Nikukumbushe tu Rais Magufuli mwaka 2017 wakati unapokea taarifa ya Prof. Mruma lalamiko lako kubwa sana na hata watanzania wakakuamini (Isipokuwa mimi) ni kuhusu kuchenjulia makinikia nje ya nchi.
Nakumbuka sana ulimlaumu sana Prof. Muhongo ukafikia hatua yakumwambia kuwa Prof. mwenzake yaani Mruma amem prove wrong kwa ripoti aliyowasilisha. Hatimaye Prof. Muhongo ukamtengua uwaziri huku Simbachawene aliyekuwa TAMISEMI akajiuzulu eti kulinda heshima yake kwakuwa alikuwa msaidizi wa Muhongo enzi ya Kikwete.
Nakumbuka sana ulimlaumu sana Prof. Muhongo kwa kile ulichodai eti amekaa kwenye hiyo wizara kwa muda mrefu bila kushauri serikali inunue Smelter na hivyo ukamuona hafai anashirikiana na mabeberu. Kikubwa ulitueleza pia kuwa kuna madini mengine yanaibiwa yakienda huko kuchenjuliwa hayawepewi thamani hivyo kinachothaminiwa ni gold pekee.
Kama kawaida yetu mawakala wa mabeberu tukaja na threads zetu humu tukielezea ugumu wa Smelter unayotaka iwepo hapa nchini. Kwakuwa wakati Prof. Mruma anawasilisha ile ripoti yake ilifikia hatua akawa anatokwa na machozi basi sisi mawakala tulipopolewa mawe kweli kweli. Hakuna mzalendo ambaye angetuelewa wakati ule.
Leo miaka miwili imepita, umesaini makubaliano ya hovyo hovyo kuwahi kutokea, ACACIA wamepata mgao wao bila kwenda mahakamani. Barrick anapeleka makinikia nje kuyachenjua kiulaini kabisa na mambo yanaendelea vyema huku Barrick akipiga bao la nguvu.
Sisi tunakuuliza kuwa, lengo lako hasa lilikuwa ni lipi? Au ulikuwa tu hulipendi jina ACACIA? Lilikukosea nini?
NB. Watanzania subirini hayo makubaliano yaje kuwekwa wazi ila kimsingi muliowaona kuwa wana akili hawajafanya kitu zaidi ya kupoteza muda na kuingia hasara.