Lengo la nyerere lilikuwa nini hasa kwenye muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lengo la nyerere lilikuwa nini hasa kwenye muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Jan 2, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi sielewewi, na ninaomba sana kama yupo mwenye data za uhakika anijuze ni nini lilikuwa lengo la Mwl. Nyerere kuutaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nikilifahamu hili pengine linaweza kunisaidia kufikiria nini sababu ya haya ambayo yanatokea na kwa nini viongozi wote wa serikali wanakuwa wakali watu wanapotaka kuzungumzia Muungano.
  Jussa ni mtu mzima. Pamoja na uzima wake wa umri na akili yake kuwa timamu, anaongea kile anachokiamini na kikubwa zaidi, anaongea akiwa na akili zake timamu. Japo sijapendezwa na aina ya lugha aliyoitumia katika kujibu hoja za Samwel Sitta, na hata kama Sitta naye anamapungufu yake ya kiutendaji na kibinadamu, bado, hakustahili kutukanwa hadharani namna ile.
  Swali la msingi: Ni kipi cha muhimu Nyerere alikiona lulu kutoka Zanzibar ambacho kinatufaa Watanganyika hadi leo tunaung'ang'ania Muungano? Tukisema usalama wa Nchi, mbona Kenya hawana muungano na Zanzibar na bado wanaishi?
  Hata kama ni kweli Jussa anatumiwa na RA kama ambavyo nimesoma reply ya mjumbe mmoja, bado, alichokiongea ukiacha lugha ya matusi aliyoitumia, ni point. Kwa asilimia 100 Watanganyika tunaulazimisha Muungano, na kikubwa ninachokiona, hakuna Rais anayetaka Muungano ufe mikononi mwake.
  Inapotokea mtu unayemuheshimu (Siyo lazima Sitta au Nyerere) anatukanwa mbele yako, ni aibu sana. Jussa alikuwa anaongea kwa kujiamini kwa sababu alikuwa anafahamu fika kuwa hakuna ambaye atamfanya chochote na aliamini nyuma yake kuna Wazanzibar ambao wanamuunga mkono. Huku kwetu ni tofauti kabisa. Akisimama Tundu Lissu kudai serikali ya Tanganyika irudishwe, tunagawanyika kutokana na itikadi za siasa na dini. Kwa nini tunaweka vyama na dizi zetu mbele ilihali tunakufa maskini? Mbona sijaona kwenye harusi ya wakristo waislamu wakishindwa kuhudhuria, na mbona kwenye harusi za waislamu wakristo wanahudhuria? Hata kwenye misiba, sijashuhudia msiba wa kiislamu ukihudhuriwa na waislamu peke yao wala ule wa wakristo ukihudhuriwa na wakristo peke yao. Tofauti zetu zinaanzia wapi Lissu anaposema Tanganyika imemezwa na Muungano? Ina maana hawa CCM ambao wanajitenga wakisikia kuhusu Tanganyika, wanapata faida gani kwenye serikali ya Muungano?
  Wazanzibar wapo sahihi kuitetea nchi yao, na sisi huku bara tunatetea nchi gani ambayo haina serikali? Mbona tunakuwa vipofi ilihali macho yetu hayana velema? Kwa nini tunashindwa kuungana kwenye mambo ya msingi na kupaza sauti moja ambayo itasikika kwa viongozi? Kama hawatatusikia, hakuna ambacho kitatushinda, Wananchi ndiyo wenye mamlaka ya mwisho, Muungono ni wa Watanganyika na Wazanzibar, kama upande mmoja wa Muungano hawautaki, hakuna muungano hapo!! Tunalazimisha kitu gani?
  Leo hii Jussa anasema kwa kujiamini kabisa kuwa watahakikisha kuwa mambo ambayo wanayataka yanaingia kwenye muswada wa sheria ya kutengeneza katiba, na kweli yameingia, Lissu akajitahidi kuongea, tukagawanyika, nini tatizo? kwa nini Wanzibar wanakuwa na sauti kwenye serikali ya Muungano kuzidi sisi?
  Yule jamaa ambaye aliuchana muswada wa sheria ya katiba mpya hadharani hakuna ambacho alifanywa. Naamini kabisa, huku kwetu mtu angethubutu kufanya vile, askari polisi wangelikuwa vihere here kumshika na kumsweka lupango. Haya matusi ambayo aliyaongea Jussa, yangeongelewa na Tundu Lissu kuhusu Zanzibar au waziri yoyote wa SMZ angeitwa "mjinga" yangeitishwa maandamano ya Wazanzibar wote na hata mtu huyo angelichukuliwa hatua za kisheria.
  Ni siri gani ambayo viongozi wa Tanganyika waliachiwa na Mwalimu Nyerere kuhusu Muungano kiasi ambacho wako tayari kuulinda kwa gharama yoyote hata kama ni kwa matusi kama haya ambayo tumeanza kutukanwa?
  Tusipoweka kando tofauti zetu za kiitikadi za vyama, makabila yetu na dini zetu, tutaendelea kutukanwa kama watoto wadogo hati akili zitakapotusogea. Leo hii katiba ya Jamuhuri yenye vipengele vichache sana vinavyohusu mambo ya Muungano, inaweza kukataliwa na Wazanzibar na ikashindwa kupitishwa, bila kujali sehemu kubwa kuna mambo ya Tanganyika. Tundu Lissu akiliongea hili, tunasema CDM hawana nia njema na Muungano, mbona inapofika CUF hakuna anayeinua kinywa kusema? Tumelogwa sisi, sio bure....
  Tuchukue hatua za haraka, vinginevyo kuna siku tutajadili habari za mgodi wa North Mara, Wazanzibari watakataa, tutakosa maamuzi.....:eyebrows:
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Soma historia ya miungano. Manufaa yake na matatizo yake. Humo utapata jibu.
   
 3. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  kujenga daraja toka dar mpaka zanzibar ila akashindwa kujenga ile neno muungano likamilike.
   
 4. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,061
  Likes Received: 417
  Trophy Points: 180
  Acha hasira. Kwa kweli Muungano ni kitu kizuri sana. Lakini, ili kupata faida za muungano, inabidi muungano huo ufikiriwe kwa marefu na mapana na washirikishwe watu katika hili. Hilo ndio kosa kubwa la kwanza ambalo lilitokea katika muungaano wa Tanganyika na Zanzibar. Ulikuwa muungano wa wanasiasa tu na si wananchi. Kibaya zaidi, baaada ya muungano hakukuwa na utashi wowote au juhudi ya kuueleza.
  Haya ndiyo mambo ambayo yanapasa yafanyike hivi sasa. Kwanza kabisa kuwepo na kura ya maoni ya wananchi kuchagua ni aina gani ya muungano watakaoutaka? (angalia: siyo unataka au hutaki, hiyo imepitwa na wakati, tunazungumzia kitu kilichopo) Federalism, confederal, union or a unitary state. Katika baadhi ya aina za muungano nchi zote mbili zinaweza kuwa na bendera, sheria zake, rais, kodi etc, mkashirikiana katika mambo machache tu. Nadhani haya yakielezwa vizuri, Watanganyika na zaidi Wazanzibari watakubali muungano unaowafaa. Sidhani kama watapinga muungano kabisa.
  Kurejea swali lako: wakati Nyerere na Karume walipofanya muungano sababu kubwa zilikuwa za kiusalama. Kwamba Zanzibar isije ikapinduliwa na wanaopendelea ufalme. Kulikuwa pia na hofu ya Marekani kuwa Zanzibar itakuwa Marxist, kwa hiyo ikashinikiza uongozi wa bara kufanya muungano ili kuitohoa. Huu pia ulikuwa wakati wa mazungumzo mengi juu ya umoja wa afrika, kwa hiyo si ajabu kwamba viongozi hao wawili walikuwa pia wanaona wanapanda mbegu ya umoja huo.
  Utaona katika sababu zote hizo, hakuna hata moja inayomgusa Mzanzibari na Mtanganganyika katika maisha yake ya kila siku, moja kwa moja.
  Lakini, mavi ya kale hayanuki: kwa nini baada ya mwanzo huo mbaya, wakuu wasikae chini na kusawazisha mambo hadi tukatokea huku? Hapo kwa kweli yanadhihiri mapungufu ya Nyerere na viongozi wote waliokuja baadaa yake, kwa vile kama ulivyosema wengine walikataa kuona muungano unakufa katika mikono yao, na wengine, kwa kweli, waliutumia kwa manufaa yao ya kisiasa (kupata kura).
  Kuvunjika kwa muungano kutakuwa balaa kubwa kwa Zanzibar na Tanganyika, hasa kwa Zanzibar kutokana na sababu za dhambi hiyo alizozitaja Nyerere na vile vile kwa sababu za kimantiki, kwamba mahusiano yoyote yatakapovunjika mahali pake hurithiwa na hisia za chuki. Hata baina ya waliokuwa wapenzi wawwili.
  Kama ukivunjika, basi usisituke siku moja Zanzibar ikadai ufuo wote wa pwani ya Tanganyika kuwa ni sehemu ya Zanzibar kwani ulikuwa chini ya Mfalme. Tena wanaweza kuleta documents na makabrasha hasa na wakapeleka suala hilo Umoja wa Mataifa! Na jee, nchi gani itakuwa inamiliki sehemu kubwa ya Bahari ya Hindi?
  Haya ni masuala ambayo hayapo hivi sasa, lakini thubutu kuvunja muungano, utakuja niambia. ( Zanzibar na majeshi yake yakisaidiwa na Misri, Iran, Saudi Arabia n.k. Tanganyika ikisaidiwa na nchi za 'Afrika' na pengine.....)

  Afadhali tubanane hapa hapa!
   
Loading...