Lengo la kuzalisha tani 75,000 za tumbaku lakwama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lengo la kuzalisha tani 75,000 za tumbaku lakwama

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,619
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  Venance George, Morogoro
  TANZANIA katika kipindi cha huu wa fedha, imezalisha kiasi cha tani 60,741 za tumbaku badala ya lengo la kuzalisha tani 75,000.

  Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Frank Urio alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro.

  Urio alisema katika kipindi cha mwaka jana, uzalishaji wa zao hili ulikuwa tani 50, 784 na kwamba hali hiyo inaleta matumaini ya kufikia malengo la kuzalisha tani 100,000 kwa mwaka.


  Mkurugenzi huyo alisema kutofikia kwa lengo la kuzalisha tani 75,000 katika kipindi cha mwaka huu, kutokana na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza katika uzalishaji wa zao hilo la biashara.

  Alitaja matatizo hayo kuwa ni pamoja na uhaba wa wataalam, zana duni za kilimo, elimu ndogo kwa wakulima na miundobinu duni.

  Urio alisema matatizo hayo na mengine, yameilazimisha Bodi ya Tumbaku Tanzania, kuitisha mkutano wa wadau wa zai hilo mkoani Tabora, ili kujadili namna ya kuyapatia ufumbuzi.

  Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,mkutano huo utawajumuisha pia wakuu wa mikoa na wilaya 23 zinazozalisha tumbaku.

  Hali kadhalika wenyeviti wa halmashauri za wilaya hizo, wawakilishi wa idara na wizara za serikali, wawakilishi wa mashirika ya umama na binafsi na wanunuzi wa tumbaku.
  .

  Alisema mkutano huo utafanyika katika ya Machi 17 na 18 mwaka huu katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), mjini Tabora.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18486
   
 2. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa na Mamlaka ktk nchi hii maskini ningelipiga marufuku kabisa kilimo cha tumbaku. Wajua kwa nini?
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Omutwale, kwa nini?
   
 4. d

  damn JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Heri wamefeli, unajua ni wangapi wangeathirika na tumbaku hiyo. Ningekuwa na uwezo ningepiga marufuku kilimo cha tumbaku. kinaharibu mazingira kwani uchomaji wa tumbaku unatumia miti mingi sana, mbolea ya tumbaku inaharibu ardhi, na tumbaku yenyewe inasababisha kasa.
   
Loading...