Lengo la kujaza fomu yoyote ni kupata taarifa siyo kutegana

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Injinia Kagoshaki kutoka Japan ameshangaa inakuwaje mtu anayegombea uongozi wa serikali anajaza fomu kwa mkono!

Kagoshaki anasema Japan unapojaza fomu yoyote hata ya kuomba chumba cha kulala Hotelini utatumia kompyuta ambayo itakuwa inakupa mwongozo ili usikosee. Lengo la kujaza fomu ni kupata taarifa tarajiwa siyo " kumtega" mjazaji ili umuhukumu, amenielimisha mjapani.

Kule Japan mtu hawezi kukosea kujaza fomu hata kama amelewa kwa sababu fomu haikosewi.

Nawatakia mchana mwema!

Maendeleo hayana vyama!
 
I tend to agree. Huku africa kujaza fomu ni kama unafanya mtihani, mitego miingi.

Lengo la kujaza fomu ni kupata taarifa tarajiwa siyo " kumtega" mjazaji ili umuhukumu, amenielimisha mjapani.
Kumbe akikuambia mjapani somo linatengamaa, lakini akisema Masiya hauelewi. Ndio maana nilisema wastarabu kwenye mambo ya msingi ya kitaifa hawategani.
 
I tend to agree. Huku africa kujaza fomu ni kama unafanya mtihani, mitego miingi.
Hata mimi nakubaliana na wewe. Lengo la kujaza fomu ni kupata taarifa unayoitaka kutoka kwa mhusika. Fomu inatakiwa ieleweke kwa urahisi na mjazaji. Ukiona wajazaji wengi wanafanya makosa basi ujuwe wewe uliyeitoa fomu ndiyo mwenye kasoro. Na hata akama imekosewa lazima mtoa fomu atoe muda wa kufanya marekebisho. Baadhi ya makosa ambayo yanaweza kufanya fomu iwe batili ni fomu iliyokosewa/kujazwa taarifa za uongo au ilicholeweshwa kurudishwa baada ya muda uliowekwa kufika.
 
Inachekesha sana mtu kuenguliwa kwa kukosea fomu. Kwan, msimamizi wa uchaguzi alikuwa wapi kuwaelekeza wanaojaza fomu.

Mbona tukienda ofisi zingine kama vile benki ukiwa unajaza fomu unauliza na unaelekezwa?
 
Kuna wale waliokosea kujaza fomu za kuomba mkopo wa elimu ya juu, majina yalitolewa ili warekebishe walipokosea. Kujaza fomu za siasa nadhani itakuwa ni INTERVIEW
 
Back
Top Bottom