Lengo la Kuiondoa CCM Madarakani Lipo Palepale

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kama CCM mna ota kuwa mtaitawala nchi hii milele ,kwa kweli mtakuwa mnaota ndoto za mchana aka Day Dreams na nawaomba sana msijidanganye kuwa JP ameuwa au anauwa upinzani zaidi anauimarisha upinzani kwa kasi ya ajabu.

Nia,lengo na madhumuni ya kuipapatua CCM lipo palepale na ni kama linazaliwa kila kukicha ,wataoapkufa watakufa ila 2020 haipo mbali ,Zanzibar tayari CCM imeshaondolewa hilo halina mjadala ,kinachoendelezwa ni ule ugumu wa kutoka roho haswa roho yako inapokuwa mbaya ,lazima utaleta makeke na kurusha madaluga,ukweli CCM imepigwa na chini.

Huku Tanganyika CCM imepenya kwenye tundu la sindano na pumua pumua yake imeenda kuvamia nyumba za masikini na kuvunja na si utekelezaji bali ni hasira ,nchi inakusanya kodi kwa tamaa kuwa itawaokoa na kuwaweka katika hali isiyohitaji misaada ,sasa jiulize hizo njia za kodi zikifungiwa na kufungwa ?

Kama ni kuabudu basi CCM muabuduni Lubuva kwani amewapitishaa njia ya shetani na mtaendelea nayo hio hadi 2020 ,ushindi wa magufuli unatiliwa shaka sijui waliojiandikisha ni wangapi kura zikijumlishwa za Lowasa na magufuli zinatokea ngapi linganisha utaona kitu kisichowezekana kimetokezwa ni Lubuva na wenzake anaowajua yeye ,uzuri ni kuwa maamuzi ya tume yaheshimiwe na ndipo tulipo ,goli la mkono tumeliona ,sheria imeachwa kufuata mkondo wake sasa tunampa heshima Magufuli as our president ,vipi ameshinda hilo si tatizo .

Tume huru ndio itakayosema kweli ila sio hii ya Lubuva na jecha,
 
  1. Uchaguzi wa Zanzibar na Bara unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
  2. Mawakala wa vyama ndio hao hao hakuna wakala wa Zanzibar wala wa Bara
  3. Vituo vya uchaguzi ndiovyo hivyo hivyo
  4. Maafisa wa uchaguzi ndio hao hao wanao simamia chaguzi zote mbili ya Zanzibar na Bara.
  5. Hesabu ya kura za Zanzibar na Bara zinafanya katika kituo hicho hicho.
Leo inakuwaje uchaguzi wa Zanzibar ni Batil na wa Bara ni halali wakati matokeo yametolewa katika utaratibu mmoja?
 
  1. Nani kamteka nyara Jecha, utekaji nyara umefanywa na nani na kwa amri ya nani?.
  2. Nani kaamrisha umeme uzimwe na generate isiwashwe wakati majumlisho wa matokeo.
  3. Nani katoa amri ya kuzingirwa hoteli ya Bwawani na majeshi. Nani kayapeleka hapo na kwa madhumuni gani.
  4. Nani alimficha Jecha na kumtaka akiwa mafichoni kutoa tangazo la kufuta uchaguzi.
  5. Ushahidi gani na ameupata lini na kuwasilishwa na nani hata ukamfika Jecha na kuamua kufuta uchaguzi kwa tangazo ambalo hana uwezo kisheria.
  6. Kwanini hatua ya Jecha imekuja baada ya siku tatu kupita bila ya kuwepo malalamiko yoyote kutoka si kwa mawakala wa vyama au maafisa wa Tume.
  7. Tamko la Jecha linaungwa mkono na kifungu gani cha sharia
 
Sharia ya uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11/1884 na kauli ya Jecha.

a)
Jecha ameeleza katika maelezo kuhalalisha kitendo chake kisicho cha kisheria, kwamba kulikuwa na fujo katika kituo. Ni kituo kipi hicho taarifa ya fujo kaipata wapi Jecha na yeye anao uwezo kushugulikia hilo. Jibu tunalipata chini ya kifungu 74. Kinachoeleza kuwa endapo kutatokea fujo katika kituo ch kupigia kura basi afisa wa Tume anaweza kuahirisha uchaguzi mpaka siku ya pili baada kuwasiliana na Tume. Hivyo Jecha hakuwa na haki na uwezo wa kuchukua hatua alochukua.Ukweli wa mambo hakukuwa na fujo yoyote iliyo ripotiwa. Jecha amejichukulia madaraka yasiyo yake kisheria
 
Kama kungalikuwa na fujo ambapo halikuwapo. Wakala angaliweza kwa mujib wa sheria kuwasilisha malalamiko kwa kujaza fomu na kuwasilisha malalamiko hayo chni ya kufungu 76. Hapakuwa na fujo na pia hapokuwepo fomu ya malalamiko iliyowasilishwa katika Tume. Hilo la kuwepo fujo ni usanii wa Jecha tu kutaka kuhalalisha hukumu yake. Hivyo Jecha ametoa hukumu pasi na kuwepo malalamiko na bila ya kuwa na uwezo way eye Jecha kutoa hukumu hiyo.

c)
Jecha amedai katika taarifa yake kuwa idadi ya wapiga kura ilizidi idadi iliyo sajiliwa. Sheria inampa uwezo wakala kwa kujaza fomu na kupeleka malalamiko kwa Tume chini ya kifungu 86. Si Jecha wala tume inaweza kufuta uchaguzi kwani wao Tume sio Mahakama ya kuhukumu kesi hiyo. Hapa Jecha kajichukulia tena uwezo na kujidhihirisha kuwa mchezaji na hakimu. Jecha hakuwa na uwezo huo wa kufuta matokeo kwa sababu hiyo na zilizotangulia.Kubwa Tume uwezo wao ni kutoa barua tu kwenda mahakamani, Kwani Tume inakuwa ni sehemu ya kesi katika kesi ya uchaguzi.

d)
Jecha amedai kwamba kulikuwa na udanganyifu. Kama kweli kulikuwa na udanganyifu basi sharia haiimpi Jecha wala Tume kufuta uchaguzi kesi za uchaguzi zinahukumiwa na mahakama na sio Jecha wala Tume kama inavyoeleza na vifungu 85 na 86, na Tume inakuwa sehemu ya kesi.Mahakama ndio mwamuzi baada ya kufunguliwa kesi na kuwasilishwa ushahidi na sio Jecha wala Tume. Kuhukumu kesi na kuamuliwa na Jecha ni kujionyeshwa rangi zake halisi Jecha na kuwa mcheza na refa.

e)
Jecha amedai kwamba kuna kura hewa. Kiifungu cha 84. Kinaeleza kwamba kamba iwapo kura zimehesabiwa kituoni mbele ya mawakala na hakuna malamiko basi kura hizo zitajaaliwa kuwa sahihi na halali. Hivyo si Tume wala Jecha hana uwezo wa kisheria kukataa hesabu ya kura hizo. Wenye kulalamika ni chama na mgombea kupitia mawakala wao na si Jecha wa Kubuni kesi kwa niaba yao na kuihukumu kwa kuzikataa kura hizo yeye mwenyewe Jecha. Lakini hii ni ile ile ya Jecha refa na mchezaji kusaidia timu yake.

f)
Jecha kafuta uchaguzi, hana uwezo huo kisheria hivyo uchaguzi kisheria haukufutwa kisheria. Tume pale inapofanya maamuzi ni lazima yawe yanafanywa kwa mujibu wa sharia. Uamuzi wa Tume lazima upate thuluthi mbili za wajumbe wa Tume kama inavyoelezwa na Sheriaa Nam. 9/199 chini ya kifungu 119(1). Hivyo maamuzi ni ya Jecha si ya Tume na hata ingalikuwa maamuzi ni ya Tume ambayo kwa kweli siyo na haina uwezo huo yasingalikuwa halali yatabaki maauzi ya Jecha na mchezo wake mchafu wakusaidia lazima CCM ishinde kwa vyovyote vile.
 
kilicho fanyika Zanzibar ndicho hich0hicho kitafanyika Tanganyika kwa tume hizi za kina Jecha na Lubuva mabadiliko ni lazima.
 
Mwiba kwa kawaida dhambi mbaya kwa nafsi zingine huonekana hata kwenye paji la uso wako. Nimejaribu ku upload picha za Lubuva kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na za sasa baada ya uchaguzi nimeshindwa natumia simu sasa hivi. Lakini zitafute utaelewa nasema nini.
Sura ya sasa ya Lubuva imekosa mvuto kabisa. Ni sawa na ya mchawi aliyekamatwa na tunguli mtaani, imejaa aibu badala ya bashasha kama angekuwa ameimaliza kazi hiyo ya uchaguzi kwa haki na mafanikio. Kusimamia uchaguzi na ukatenda haki ni jambo la fahari na la kihistoria mtu unapaswa kutembea kifua mbele na sura yenye kila hali ya fahari lakini kama hukufanya haki nafsi yako itasutwa usoni
 
Kama CCM mna ota kuwa mtaitawala nchi hii milele ,kwa kweli mtakuwa mnaota ndoto za mchana aka Day Dreams na nawaomba sana msijidanganye kuwa JP ameuwa au anauwa upinzani zaidi anauimarisha upinzani kwa kasi ya ajabu.

Nia,lengo na madhumuni ya kuipapatua CCM lipo palepale na ni kama linazaliwa kila kukicha ,wataoapkufa watakufa ila 2020 haipo mbali ,Zanzibar tayari CCM imeshaondolewa hilo halina mjadala ,kinachoendelezwa ni ule ugumu wa kutoka roho haswa roho yako inapokuwa mbaya ,lazima utaleta makeke na kurusha madaluga,ukweli CCM imepigwa na chini.

Huku Tanganyika CCM imepenya kwenye tundu la sindano na pumua pumua yake imeenda kuvamia nyumba za masikini na kuvunja na si utekelezaji bali ni hasira ,nchi inakusanya kodi kwa tamaa kuwa itawaokoa na kuwaweka katika hali isiyohitaji misaada ,sasa jiulize hizo njia za kodi zikifungiwa na kufungwa ?

Kama ni kuabudu basi CCM muabuduni Lubuva kwani amewapitishaa njia ya shetani na mtaendelea nayo hio hadi 2020 ,ushindi wa magufuli unatiliwa shaka sijui waliojiandikisha ni wangapi kura zikijumlishwa za Lowasa na magufuli zinatokea ngapi linganisha utaona kitu kisichowezekana kimetokezwa ni Lubuva na wenzake anaowajua yeye ,uzuri ni kuwa maamuzi ya tume yaheshimiwe na ndipo tulipo ,goli la mkono tumeliona ,sheria imeachwa kufuata mkondo wake sasa tunampa heshima Magufuli as our president ,vipi ameshinda hilo si tatizo .

Tume huru ndio itakayosema kweli ila sio hii ya Lubuva na jecha,
naona povu limekutoka maneno ya leo sherehe za kuzaliwa CCM hotuba ya JPM rais imekuchangini
 
Kule Singida, rais kasema wasahau kuingia madarakani. Ngosha huwa anazo kauli ambazo ukipenda zisikilize usipozipenda zima TV au badilisha channel au zima radio yako. Neno huwa halirudii mdomoni, linatoka moja kwa moja, likikuuma pole, likikufurahisha basi unayo ruhusa ya kucheka. Mkwere aliwastahi sana wapinzani, aliwavumilia kama vile babu anavyomuachia kidevu mjukuu wake ili akichezee halafu akichoka asinzie kwa amani.

Maana yake muda huu ni wa kazi, na kitakachompima Ngosha ni matokeo ya kazi. Siasa za majukwaani, vijembe na utafutaji wa kick, huu sio muda wake. Siasa nyingi hazijatusaidia zaidi ya watu fulani fulani kupata umaarufu kupitia matatizo ya walio wengi.
 
Pamoja na kuwa na kero nyingi kuhusu utawala wa kinafiki na kifisadi uliojengwa na CCM kwa muda mrefu, naposoma uzi wa aina hii huwa napata shauku kubwa sana ya kujua ni mikakati ipi mipya waliyo nayo wapinzani ya kuweza kuitoa CCM madarakani kupitia chaguzi za "vikaratasi?

Tangu 1995 hakujawa na kitu mipya kinachoonyesha mwelekeo mpya zaidi ya kupeana hamasa zinazoishia kwa mafanikio haba ya kuongeza wabunge, madiwani, n.k., kiduchu lakini Ikulu zikibakia ndotoni.

Sipuuzi juhudi za wapinzani makini. Tena nawasifu sana kwa ujasiri wao. Natambua sana kuendesha siasa ukiwa mpinzani Tz ni kujiweka katika mazingira ya hatari. It is a real health hazard. Lakini mahali ambapo siasa inakuwa na gharama kubwa ikihusisha hata uhai na uzima wa binadamu ni vyema kuweka mahesabu sawa wananchi wajue undani wa mradi wanaoshirikishwa.
 
Mwiba kwa kawaida dhambi mbaya kwa nafsi zingine huonekana hata kwenye paji la uso wako. Nimejaribu ku upload picha za Lubuva kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na za sasa baada ya uchaguzi nimeshindwa natumia simu sasa hivi. Lakini zitafute utaelewa nasema nini.
Sura ya sasa ya Lubuva imekosa mvuto kabisa. Ni sawa na ya mchawi aliyekamatwa na tunguli mtaani, imejaa aibu badala ya bashasha kama angekuwa ameimaliza kazi hiyo ya uchaguzi kwa haki na mafanikio. Kusimamia uchaguzi na ukatenda haki ni jambo la fahari na la kihistoria mtu unapaswa kutembea kifua mbele na sura yenye kila hali ya fahari lakini kama hukufanya haki nafsi yako itasutwa usoni
....exactly....nami nimeliona hili la Lubuva linavyomsuta rohoni....badala ya kujisifia kufanya kazi yenye mafanikio kwa taifa nimeona muda mwingi anajitetea yeye na tume yake dhidi ya shutma zinazoelekezwa kwao.....hakika hawana amani rohoni kwa matendo yao na hili litawatafuna hadi 2020 kama watakuwepo (baadhi yao)....wanaoonekana kuwasifia tume ni ccm walioibeba kwenye urais....hii inasikitisha na kuuzunisha sana...

...labda niseme tu...katika TZ hii ni wazi kuwa sasa imedhihirika kuwa daima tume inayoteuliwa na watawala haiwezi kutenda haki kwenye uchaguzi....na hivyo ni kosa kubwa na janga kuu kwa wanasiasa wa upinzani kukubali tena kujiingiza kwenye uchaguzi na tume hii...hili kosa kamwe lisirudiwe maana kwa wenzetu (mfan Nigeria)walikoshinda wapinzani kulikuwa na tume huru kabisa....na ndio maana watawala waliangukia pua kule...ni kwa kuikataa tume hii tu ndipo wapinzani wataiona ikulu....vinginevyo wataendelea kuisoma namba kwa kejeli za ccm....maana hata rais JPM ameshawabip wapinzani kuwa waisahau ikulu kabisa....anajua 2020 atafanya nini kubaki madarakani....
 
Kama watu kama Dr. Slaa na ajenda zao za kupinga ufisadi hawatakiwi kwenye upinzani, Basi CCM haitoki. Na mziki wa Magu nao ndio fungakazi.
 
JPM ameanza kushindwa taratiiiibu, hana concrete plan taratibu anaelekea alikoishia aliyemtangulia ,ndiyo maana Lowasa kasema Tutaingia Ikulu bila kumwaga damu,kama huamini niambie chenye tija alichofamya jpm mpaka sasa kwa mapana yake-CCM ni ile ile
 
Back
Top Bottom