Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
2,186
2,455
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

WASIFU WA OLE SABAYA

Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).

Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.

Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.

Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.

Zaidi soma...

HAKIMU Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema mshtakiwa Lengai Ole Sabaya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai amekutwa na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na wenzake. Hakimu amesema hayo Oktoba 15, 2021 wakati akiendelea kuchambua hoja wakati akisoma hukumu ya Sabaya na washitakiwa wenzake watatu.

Sabaya baada ya kukutwa na hatia anaiomba mahakama imuonee huruma kwani sio yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya Mamlaka yake ya Uteuzi, pamoja na hayo mshtakiwa huyo anabainisha ana mchumba walikuwa wafunge ndoa na mahari ameshatoa.

Awali Hakimu Amworo amesema hakuna shaka washitakiwa watatu walifika dukani kwa Mohamed Saad siku ya tukio. Ameongeza kuwa amethibitisha mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya na mshitakiwa wa pili Sylivester Nyegu walikuwa wanafahamiana.

Ameeleza kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

Hata hivyo, amesema hakuna silaha iliyotumika katika tukio hilo, hivyo hakuna shambulizi la kutumia silaha. Hakimu amesema kati ya mashahidi 11 waliotoa ushahidi wao dhidi ya Sabaya, ni mashaidi wawili tu ndio ambao ushahidi wao haukuwa na mashiko.

Sabaya amekutwa na hatia kabla ya kupewa nafasi na watuhumiwa wenzake wajitetee ili Wapungiziwe adhabu.
 
Kuonekana lina Kesi ya Kujibu tu ni kwamba Mahakama ilijiridhisha ni Jambazi lakini haliwezi kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya walau kujitetea,ile kuwekwa Kisongo tu tayari ni dalili kwamba ni Jambazi,leo kitavalishwa rasmi gwanda la Jela,hakika What Goes Around Comes Around
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.


Ole ole leo ole wake.
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.
Atapata si chini ya kifungo cha miaka mi 3 mpaka mi 5 au kulipa faini.

Atalipa faini ambayo haitazidi hata milion 6 then ataachiwa.. kuzuga atakamatwa tena kwa ajili ya mashtaka mapya.

hii case ni ya mkakati.
ni heri ufuatilie ugali wako..

Hukumu yake naifahamu.
 
Back
Top Bottom