Lengai ole Sabaya akutwa na ukwasi wa Tsh. Bilioni 3 baada ya kupekuliwa

Gazeti la Raia Mwema la Jumamosi, 15 May 2021 limeripoti kuwa DC aliyefurushwa huko Hai, Lengai Ole Sabaya (34) amepekuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na kukutwa na ukwasi wa zaidi ya TZS 3 Bilioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo baadhi ya fedha zimekutwa nyumbani kwake na nyingine kwenye taasisi mbalimbali za fedha.

Hivi unazifahamu billion 3?
 
Mzee wa vijisent alipobainika kuwa na fedha nje ya nchi, alisema fedha zile(sikumbuki kiasi) zilkuwa ni vijsenti tu bila shaka akimanisha kuna wenzake ( probably mabosi wake) walikuwa na ukwasi mkubwa zaidi.

Sasa kwa concept hiyo hiyo, Kama Sabaya kakutwa na bilioni 3, je waliokuwa wanakingia kifua( pengine ndio walikuwa wakimtuma) watakuwa na fedha kiasi gani?

Bado kuna yule anaesuburi kuapishwa ambae nae anatuhumiwa kuchukua fedha za watu kinyume na utaratibu na kuziweka katika akaunti yake pale Benki Kubwa.

Hii nchi inachosha sana!

Na uchoke zaidi kwani licha ya hayo UJINGA umeongezeka mno ndani ya miaka 6 iliyopita. Kila kona wajinga kibao. Humo yumo Sabaya na wengi aina yake. MJINGA unampa rungu
 
Viongozi na waliokuwa viongozi wengi wanatakiwa kupekuliwa

Kuanzia Sabaya,Makonda, Polepole bashiru Biswalo na Dotto James

Hata makamo wa rais anatakiwa kufanyiwa uchunguzi

Hata kapilimba aliyeenda Namibia kuna ufisadi wa kutisha hawa jamaa cycle yao imefanya.

Diwani chunguza hawa watu walikusanya pesa nyingi sana na Magufuli.
 
Viongozi na waliokuwa viongozi wengi wanatakiwa kupekuliwa

Kuanzia Sabaya,Makonda, Polepole bashiru Biswalo na Dotto James

Hata makamo wa rais anatakiwa kufanyiwa uchunguzi

Hata kapilimba aliyeenda Namibia kuna ufisadi wa kutisha hawa jamaa cycle yao imefanya.

Diwani chunguza hawa watu walikusanya pesa nyingi sana na Magufuli.
Haya mambo yatawezekana tu siku upinzani ukikamata uongozi wa hii nchi na kamwe si vinginevyo.
 
Lengai Ole Sabaya alikuwa anatembea na dola za marekani tu, msaidizi wake ndiye alikuwa anapewa jukumu la kwenda kuzibadilisha mitaani, hizo fedha alizitoa wapi? ni dili la dhahabu alilowapiga wafanyabiashara fulani huko Hai ambao mapande ya dhahabu hayo walikuwa wameyaficha kwenye kiti na kuchomelea kisawasawa, kupitia vijana wake, sabaya alilikamata gari hilo na kumwamuru OCD gari hiyo ifanye doria kwa siku hiyo pasipo Sabaya kumweleza uwazi OCD wafanyabiashara hao walitaka kumuhonga milioni 50 hadi 100 OCD na kijana wa Sabaya ambaye aliwekwa kwenye doria katika gari hilo kimkakati kwa ajili ya kumpa sabaya taarifa zote zitakazojiri kutoka kwa wafanyabiashara hao, DSO alipopenyezewa taarifa hizo alianza kufuatilia taarifa hizo na dhahabu hiyo, lakini Ole Sabaya aliamuru DSO huyo ashughulikiwe na vijana wake, na DSO alipigwa sana hadi akapelekwa kulazwa hospitali, Sabaya aliichukua ile dhahabu yote ikawa mali yake binafsi, DSO alipotoka hospitali aliandaa report yake akaituma hadi kumfikia Rais, Magufuli alimuita Sabaya ikulu akamhoji kuhusu tuhuma hizo, lakini Sabaya ili kumfurahisha Magufuli akamweleza kwamba ni fedha siyo dhahabu zilizokuwa zimepelekwa Hai na Mbowe ili achukue jimbo yeye akawa amezikamata.....mambo ni mengi sana....lakini naona faili lake lilisahulika mezani kwa Rais hadi Samia kulikuta.

Vile vile, jiulize ni kwa nini wilaya ya HAI ilikuwa ni ya 5 -6 katika kukusanya mapato ya serikali, ukishajua ndo uelewe umafia mwingine wa sabaya aliowafanyia wafanyabiashara ili kumfurahisha Magu
Yani hawa vijana walikuwa wanamchezea kweli mwendazake,walikuwa wanajua kucheza na akili yake

Ova
 
Gazeti la Raia Mwema la Jumamosi, 15 May 2021 limeripoti kuwa DC aliyefurushwa huko Hai, Lengai Ole Sabaya (34) amepekuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na kukutwa na ukwasi wa zaidi ya TZS 3 Bilioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo baadhi ya fedha zimekutwa nyumbani kwake na nyingine kwenye taasisi mbalimbali za fedha.
Serikali ya Wanyonge katika ubora wake
 
Usishangae baada ya miaka kadhaa mbele akakugombea ubunge na akapewa ama akateuliwa tena kuwa kiongozi.
Hili linchi huwa halieleweki lipoje.
 
Tarifa hizi ili ziwe Sawa, ni Ile tume ya uchunguzi kuwa imemaliza kazi yake na kuiwasilisha Kwa aliyewatuma, hizi mambo za kujazana upumbavu zinatoka wapi?

Tume ya uchunguzi imeshatoa ripoti yake lini na Kwa nani Au ni upumbavu wa jamii ya Twitter na kusambazwa na wapumbavu wambea wasiotaka kutafuta ukweli?
 
Yaani tuliimbishwa nyimbo za uzalendo tukiwa na njaa, unashangaa wananchi tunakonda wao vitambi vinatoka kumbe walilia nasi mchana huku usiku wakitucheka huku wakigonga cheers glass za wine na nyama choma
Hawa vijana sijawahi kuwaamini
Wote walikuwa wanapiga mzee hajui

Ova
 
Hilo gazeti limekuwa msemaji wa polisi/takukuru na hata wa bandari mlipayuka hivi hivi, hilo gazeti la kufungia utumbo tu na hawa ndio waandishi Haji Manara anawaita taka taka tu.
Hivi Haji Manara anaweza kuwa chanzo cha habari yako kikaheshimiwa!
 
Back
Top Bottom