Lembeli: J.K ndiye aliyetufikisha hapa

Bei Mbaya

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
2,262
843
Mhe. Mbunge Lembeli akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Urambo amefumba fumbo kwamba wasioishi hapa Tanzania na wasiojua kwa nini watanzania ni masikini ndiyo waliyotufikisha hapa tulipo.

Maneno hayo yakanikumbusha kauli ya mhe. J.K aliyoitoa safarini Ufaransa 'sijui kwa nini Tanzania ni masikini'. pia safari za nje ya nchi zinazolalamikiwa mara kwa mara ndicho mbunge huyo alichobainisha 'wasioishi hapa nchini'

kauli hiyo ilifuatiwa na maelezo ya Sitta ya nia yake ya kuwaunganisha watanzania wazalendo ili kupinga rasilimali za taifa kunufaisha wachache. Sherehe hiyo pia ilishuhudia wazee wa urambo wakimtunuku Mhe. Sitta heshima kwa kuvalishwa mashuka kama wanayovishwa wazee wa Urambo kwa mchango wao kwa kupigania haki za jamii yao

Source: Taarifa ya Habari ITV saa 2
 
Hiivi Lembeli ilikuwaje magamba wakamuacha apite kwenye chekeche lililomnyofoa shibuda
 
Hiivi Lembeli ilikuwaje magamba wakamuacha apite kwenye chekeche lililomnyofoa shibuda

Hofu ya chama kuonekana wazi wamenuia kuwamaliza waliojipambanua kuupinga ufisadi
Selelii na Kimaro wakawa chambo, ila walishapanga kuwashughulikia zaidi ya hao
 
CCM ilishakuwa sawa na mtaro wa maji machafu uliochafuka. Haiwezekani kuusafisha wala kuukarabati. Kwa wale wanaozipenda rasilimali za nchi hii ni bora wakajitoa CCM, wasione aibu, wawe wazalendo kwa nchi yao, wasiendelee kuukumbatia uzalendo wao kwa CCM. Ili hii nchi iweze kujikomboa na wakoloni weusi au makaburu weusi ni lazima kuiua kwanza CCM, ndipo Ukombozi wa kweli utapatikana.

Sita na Lembeli iueni CCM ili mtimize uzalendo wenu kwa Tanzania na Watanzania na ninyi mtaendelea kuwa Watanzania. Mtu unaweza kubadilisha uanachama na hakuna chochote kibaya au cha ajabu, lakini utaifa na uraia sio rahisi.

Ua CCM jenga Tanzania.
 
Hofu ya chama kuonekana wazi wamenuia kuwamaliza waliojipambanua kuupinga ufisadi
Selelii na Kimaro wakawa chambo, ila walishapanga kuwashughulikia zaidi ya hao

CCM can not easly take such a risk. Watashangaa majimbo mengi yanaenda upinzani
 
Huyu jamaa tangia bungeni alikuwa na msimamo mkali sana dhidi ya wachache wenye kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa yao!!!!asingestahili kuwa magambani!!!
 
Kumbe maandamano ya CDM hayahusiani na yanayoendelea nchini bali J.K?umeona sasa,sie tunadanganywa eti mara CDM...Ohoo sijuhi mara maandamano,kumbe ubaya unajulikana na chanzo kinajulikana pia...vry interesting!
 
Mhe. Mbunge Lembeli akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Urambo amefumba fumbo kwamba wasioishi hapa Tanzania na wasiojua kwa nini watanzania ni masikini ndiyo waliyotufikisha hapa tulipo.

Maneno hayo yakanikumbusha kauli ya mhe. J.K aliyoitoa safarini Ufaransa 'sijui kwa nini Tanzania ni masikini'. pia safari za nje ya nchi zinazolalamikiwa mara kwa mara ndicho mbunge huyo alichobainisha 'wasioishi hapa nchini'

kauli hiyo ilifuatiwa na maelezo ya Sitta ya nia yake ya kuwaunganisha watanzania wazalendo ili kupinga rasilimali za taifa kunufaisha wachache. Sherehe hiyo pia ilishuhudia wazee wa urambo wakimtunuku Mhe. Sitta heshima kwa kuvalishwa mashuka kama wanayovishwa wazee wa Urambo kwa mchango wao kwa kupigania haki za jamii yao

Source: Taarifa ya Habari ITV saa 2

Lembeli ni kati ya wazee wenye akili waliobakia CCM.....
 
Sijui niseme je lakini... Namshauri JK... afuate yale aliyofanya Tabo Mbeki: Anaweza ku-fanya version yake kulingana na mazingira yetu he must do something of that kind.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hapo amegusa penyewe kabisa,lazima atapewa onyo kwenye vikao vya NEC.
 
Back
Top Bottom